saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
LUHAGA MPINA, Mbunge wa Kisesa ametumia takribani masaa 7 mfululizo kuanzia saa 11 jioni hadi saa 6 na nusu usiku akizungumza na watanzania juu ya matatizo mbalimbali yanayolikabili taifa letu ikiwemo maonevu wanayofanyiwa wachimbaji wadogo wa madini kufukuzwa na maeneo yao kupewa raia wa kichina kinyume na sheria za nchi.
Amezungumzia makato makubwa waliyowekewa wakulima wa mazao kama pamba, choroko, mbaazi na kusababisha kunufaisha walanguzi na wakulima kubaki masikini, Amezungumia suala la viongozi ambao siyo raia wa Tanzania hali inayochangia kushamiri kwa rushwa, wizi, ufisadi wa mali za umma na kuwaonea wananchi wakiamini kuwa hii sio nchi yao na siku yoyote wataondoka kurudi makwao. KWA KIREFU Hotuba ya masaa saba imewafumbua macho watanzania wengi ambao wako gizani wakishabikia mipira ya simba na yanga huku taifa lao likizidi kutafunwa na kikundi cha watu huku watanzania wengi wakilia umasikini wa kutupwa.
Pia nilipomsikiliza anasema hotuba yake hiyo wakati akiiandaa amezingatia pia ushauri uliotolewa na Mzee Warioba, Mzee Butiku, Mbunge Kishimba, Mzee Kasori, Rostam Aziz, Mzee Charles Gishuli, Mzee Christopher Liundi, Padri Kitima na watanzania wengine wa kada mbalimbali.
Swali la muhimu Hotuba ya Masaa 7 ya Luhaga Mpina ina ujumbe gani kwa watanzania?