Hotuba ya masaa 7 mfululizo ya Luhaga Mpina ina ujumbe gani kwa watanzania?

Hotuba ya masaa 7 mfululizo ya Luhaga Mpina ina ujumbe gani kwa watanzania?

ila je ina ujumbe gani kwa watanzania?
Tujitambue tubadilike
SmartSelect_20250203_061211_Samsung Internet.jpg
 
LUHAGA MPINA, Mbunge wa Kisesa ametumia takribani masaa 7 mfululizo kuanzia saa 11 jioni hadi saa 6 na nusu usiku akizungumza na watanzania juu ya matatizo mbalimbali yanayolikabili taifa letu ikiwemo maonevu wanayofanyiwa wachimbaji wadogo wa madini kufukuzwa na maeneo yao kupewa raia wa kichina kinyume na sheria za nchi.

Amezungumzia makato makubwa waliyowekewa wakulima wa mazao kama pamba, choroko, mbaazi na kusababisha kunufaisha walanguzi na wakulima kubaki masikini, Amezungumia suala la viongozi ambao siyo raia wa Tanzania hali inayochangia kushamiri kwa rushwa, wizi, ufisadi wa mali za umma na kuwaonea wananchi wakiamini kuwa hii sio nchi yao na siku yoyote wataondoka kurudi makwao. KWA KIREFU Hotuba ya masaa saba imewafumbua macho watanzania wengi ambao wako gizani wakishabikia mipira ya simba na yanga huku taifa lao likizidi kutafunwa na kikundi cha watu huku watanzania wengi wakilia umasikini wa kutupwa.

Pia nilipomsikiliza anasema hotuba yake hiyo wakati akiiandaa amezingatia pia ushauri uliotolewa na Mzee Warioba, Mzee Butiku, Mbunge Kishimba, Mzee Kasori, Rostam Aziz, Mzee Charles Gishuli, Mzee Christopher Liundi, Padri Kitima na watanzania wengine wa kada mbalimbali.

Swali la muhimu Hotuba ya Masaa 7 ya Luhaga Mpina ina ujumbe gani kwa watanzania?
Wewe ndiyo umeisikiliza, badala ya kuweka summary ya ulichosikia unauliza maswali. So frfr you're expecting answers kutoka kwa ambao hawajasikia chochote, strange world.
 
Wewe ndiyo umeisikiliza, badala ya kuweka summary ya ulichosikia unauliza maswali. So frfr you're expecting answers kutoka kwa ambao hawajasikia chochote, strange world.
mbona makasiriko hotuba ya masaa 7 unawezaje kuweka summary
 
CCM watakuwa wanajuta tu kumfahamu huyu jamaa. Tangu Magufuli alipofariki, hajawahi kuwapa muda wa kupumzika. Yaani ni mwendo tu wa kuwacharaza bakora CCM wenzake.
Tangu aondolewe kwenye u-Waziri na mama imekuwa taabu mno. Wanasiasa wa Tz ni kichefuchefu sana. Mbona wakati wa utawala wa mwendazake hatukuwai kumsikia au alipokuwa bado waziri undet SSH regime??
 
Back
Top Bottom