Hotuba ya Mbowe: Huwezi ukaiandika historia ya Lowassa ukaacha kuitaja CHADEMA. Ni kujidanganya kuua historia ambayo huwezi kuiua

Hotuba ya Mbowe: Huwezi ukaiandika historia ya Lowassa ukaacha kuitaja CHADEMA. Ni kujidanganya kuua historia ambayo huwezi kuiua

Povu la Nini, mbona wale wengine ukuwaambia hivyo?

Ujumbe uwafikie wote. Siasa misibani ni kukosa kuwajali wafiwa. Maana katika kipindi hicho kigumu familia inafurahi sana kusikia kauli zenye faraja kuwaelekea wao.
 
Monduli sio Longido tafadhali!

Kati ya hotuba nzuri zilizojaa busara, ujasiri, ukweli na weledi wa kisiasa basi ni hii ya leo kule Monduli ambapo Mheshimiwa Freeman Mbowe amezungumza juu ya ukweli wa maisha ya kisiasa ya hayati Lowassa.

Hotuba hii iliyojaa ujasiri na umahiri mkubwa imegusa watu wengi na kujikuta wakipiga makofi mengi kwa Mh Mbowe. Mbowe amemtaja Lowassa kama mgombea urais wa CHADEMA aliyeipaisha demokrasia ya nchi na kuwaweka wapinzani katika ramani mpya ya siasa, kuwezesha wabunge zaidi ya 120 wa upinzani na madiwani zaidi ya 2,000 kutoka upinzani ikiwa ni karibu nusu ya madiwani wote nchini.

Mbele ya rais Samia na viongozi wakubwa kote nchini, Mbowe amehoji kwanini ukweli huu unafichwa? Huu ni unafiki wa kisiasa na Mbowe ameonekana kusikitishwa na kukasirishwa na unafiq huu mkubwa. Mbowe amemtaja Lowassa kama mhanga wa mifumo hovyo ya kidemokrasia nchini.

Hongera sana Freeman Mbowe kwa ujasiri huu!
 
Hivi CCM hakuna hata mmoja mwenye afadhali? Hizi aibu zina ulazima gani?
Historia ya Marehemu huidhimishwa na familia kipi wanataka kiwepo kwenye Risala na kipi kisiwepo

Mbowe kasimama na mihasira na CCM na Serikali na Familia kuwa Mbona kwenye Historia hawajaweka kuwa alikuwa Chadema

Wwenyewe Familia wameamua hivyo
 
Kati ya hotuba nzuri zilizojaa busara, weledi, ukweli na weledi wa kisiasa basi ni hii ya leo kule Longido ambapo Mheshimiwa Freeman Mbowe amezungumza juu ya ukweli wa maisha ya kisiasa ya hayati Lowassa.

Hotuba hii iliyojaa ujasiri mkubwa imegusa watu wengi na kujikuta wakipiga makofi mengi kwa Mh Mbowe. Mbowe amemtaja Lowassa kama mgombea urais wa CHADEMA aliyeipaisha demokrasia ya nchi na kuwaweka wapinzani katika ramani mpya ya siasa, kuwezesha wabunge zaidi ya 120 wa upinzani na madiwani zaidi ya 2,000 kutoka upinzani ikiwa ni karibu nusu ya madiwani wote nchini.

Mbowe amehoji kwanini ukweli huu unafichwa? Huu ni unafiki wa kisiasa. Mbowe amemtaja Lowassa kama mhanga wa mifumo hovyo ya kidemokrasia nchini.

Hongera sana Freeman Mbowe kwa ujasiri huu!

Longido? Uko dunia ipi wewe
 
Mhe Mbowe amezitendea haki dakika 6 alizotumia katika kutoa salaam katika mazishi ya Hayati Edward Lowassa, kijijini Ngarash Monduli.

Mhe Mbowe anasema, huwezi kuielezea historia ya Hayati Edward Lowassa bila kuitaja Chadema.

Dakika sita za Mbowe zimeniletea hisia kali hadi nimetoa machozi.

Asante sana Mhe Mbowe
Leo ccm kimewaramba. Wanaandika history fake.
 
WASIFU WA LOWASSA UNAMUELEZEA ALIWAHI KUTIA NIA YA KUGOMBEA URAIS CCM LAKINI HAIMUELEWEZEI ALIWAHI KUGOMBEA URAIS CHADEMA

MBOWE ANAWACHANA LIVE NA KUWAAMBIA HAWAWEZI KUIFUTA HISTORIA YA LOWASSA KWAMBA ALIWAHI KUWA MJUMBE WA CC-CDM NA KUGOMBEA URAIS CHADEMA
 
Iligundulika kuwa ufisadi wake ni wa kimfumo ndani ya CCM na siyo wake binafsi.

Wewe unadhani Ile ishu ya Richmond aliweza kuifanya bila ya ruhusa ya Rais wa wakati ule Jakaya Kikwete kuhusika??

Au unadhani zile bilioni 360 ingewezekana kutolewa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow bila ya ruhusa ya Ikulu chini ya Jakaya Kikwete??

Umeshasahau kuwa Jakaya alisema zile Hela za Tegeta Escrow hazikuwa za Umma?? Unadhani alisema vile bila ya kuwa na sababu za msingi kujilinda??
Kwa hiyo iligundulika baada ya kuwa udhalilishaiji ulishatokea......???
 
Sijui huwa wanafikiria nini lakini hata mm nilishangazwa kutosikia yeye kugombea Urais na kuwa candidate tofauti na CCM kupata Kura 6m+........
Na kwenye shukrani familia inawatambuwa wengi na Kwa kipekee mama Samia, ila jina la Kikwete halijatajwa popote, Huyu Mzee ajitafakari atubu mapema kabla hajafa.
 
Historia ya Marehemu huidhimishwa na familia kipi wanataka kiwepo kwenye Risala na kipi kisiwepo

Mbowe kasimama na mihasira na CCM na Serikali na Familia kuwa Mbona kwenye Historia hawajaweka kuwa alikuwa Chadema

Wwenyewe Familia wameamua hivyo
Kuna haja gani ya kuficha kitu ambacho kinajulikana? Kwani mkisema aligombea kupitia chadema mtapungukiwa nini?

Ona sasa dk 5 tu mtu kaharibu sifa zote mlizozitaka.
 
Back
Top Bottom