Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,425
HOTUBA YA RAIS VLADMIR PUTIN KUIDHINISHA KUTWALIWA KWA DONBASS.
Watu wa Donbass wamefanya chaguo lao, chaguo lisilo na utata, Tutawakumbuka daima mashujaa wa "Russian Spring".
Hakuna Umoja wa Kisovieti, zamani haziwezi kurudishwa, na Urusi ya kisasa haihitaji hii, hatujitahidi kuirejesha kwa hili, lakini Urusi mpya yenye kuongoza mwelekeo mpya wa dunia ni wajibu wetu ulio mikononi mwetu.
Watu wanaoishi katika DPR, LPR, Kherson na Zaporozhye wameamua kuwa raia wetu. Milele na milele!
Tunatoa wito kwa Kyiv kuja katika meza ya mazungumzo tujadili mstakabali mpya wa Ukraine, lakini hatutajadili uamuzi huu uliofanywa na watu wa Donbass, Urusi haitasaliti watu hawa daima. Tutailinda ardhi yetu mpya kwa njia zote. Tutaijenga upya miji na majiji yote yaliyoharibiwa. Tutaendeleza biashara, miundombinu, mifumo ya afya. Tutalinda maadili yetu na Nchi yetu ya Mama Russia dhidi ya Magharibi.
Magharibi wanataka kutuona kama koloni, umati wa watumwa wasio na roho. Kwao, tishio la moja kwa moja ni falsafa yetu, ndio maana wanaingilia wanafalsafa wetu. Nawaeleza wazi kwamba, "utaratibu wa msingi wa utawala wa sheria" uliopendekezwa na Magharibi ni "upuuzi". Wasomi wa Magharibi daima wamekuwa na tabia na fikra za wakoloni dhidi yetu.
Vikwazo havitoshi kwa Anglo-Saxons, walibadilisha hujuma, kwa kweli walianza kuharibu miundombinu ya Ulaya, hii ni miundombinu yetu, lakini ni uhai wa Ulaya, Tunaamini ni ugaidi wa Marekani, Tutalishughulikia hili kigaidi kwa sheria za kimataifa. Marekani inaikalia Ulaya leo hasa Ujerumani, Korea na Japan, lakini inazungumza kuhusu haki sawa nazo. Pesa za karatasi (dola na euro) haziwezi kulisha watu wetu. Marekani inajaribu kuchukua kila kitu kwa kiburi na usaliti, inadanganya bila kujali kama Goebbels.
Ninataka mamlaka ya Kyiv na mabwana wao halisi huko Magharibi wanisikie, ili kila mtu akumbuke hili: Watu wa Donetsk, Luhansk, Zaporozhye na Kherson wameamua leo rasmi wawe raia wetu na ardhi yao kuwa yetu. Hii ni Milele na milele. Wanaofikiri tunatania basi wajaribu. Sasa kuna kizuizi cha Washington kwa Urusi, Uchina na Iran, nchi zingine zinafuata mstari, na pia washirika wa sasa wametekwa na Washington. Sisi kama taifa kuu lenye historia ya ushindi duniani tumekataa, Moscow inataka na itaiweka Dunia pawe mahali salama kwa binadamu wote.
Magharibi inakanusha viwango vyetu vya maadili, dini, familia. Hivi kweli tunataka Warusi wawe na "mzazi namba moja, mbili, tatu" badala ya "mama na baba" na kwamba upotovu unaosababisha uharibifu na kutoweka maadali uwekwa kwa watoto shuleni, eti kuna baadhi ya jinsia, isipokuwa wanawake na wanaume. ? Kwa sisi, hii haikubaliki. Ushoga na usagaji hautakuwa sehemu ya ardhi ya Urusi na Warusi.
Uwanja wa vita ni wa watu wetu, kwa Urusi kubwa ya kihistoria. Tunahitaji uimarishaji wa jamii nzima. Maadili yetu ni ubinadamu, rehema na huruma. Kama Ilyin alisema, "Ninaamini katika nguvu za kiroho za watu wa Urusi, roho yao ni roho yangu, hatima yao ni hatima yangu, mateso yao ni huzuni yangu, kushamiri kwao ni furaha yangu."
Ukweli uko nyuma yetu! Urusi iko nyuma yetu:
Uraaaaaa Uraaaa!
Baadaa ya Hotuba hii, Rais Putin akasogea katika meza maakumu akiongozana na Kiongozi wa Donetsk Bwana Denis Pushilin walitia saini makubaliano ya kukubaliwa kwa Jamhuri ya Donetsk DPR kuwa sehemu ya Urusi.
Akafuatia Kiongozi wa Mkoa wa Zaporozhye Yevgeny Balitsky akasongea hadi alipo Rais Putin nae wakatia saini makubaliano ya Mkoa wa Zaporozhye kujiunga eneo hilo kwenda Urusi.
Akafuatia kiongozi wa Mkoa wa Kherson Volodymyr Saldo akasogea alipo Rais Putin nae kwa pamoja wakatia saini makubaliano ya Mkoa wa Kherson kujiunga eneo hilo na Urusi.
Mwisho alikuwa ni kiongozi wa Jamhuri ya Luhansk Bwana Leonid Pasechnik, alisongea mezani alipo Rais Putin, na kisha walitia saini makubaliano ya kujumuishwa kwa LPR nchini Urusi.
Na Yericko Nyerere
OFA MAALUMU.
Pata kitabu cha UJASUSI kwa HARD-COPY kwa 25,000 tu badala ya bei halisi ya 80,000/=.
Kwa Dar free Delivery. Nje ya Dar nauli 8,000/=.
Wahi Lipia kwa
0715865544 au
0755865544
(Yericko Nyerere)
Kwa watumiaji wa ANDROID nenda Play Store pakua YerickoNyerereApp uweze kujisomea vitabu vyote kwa 5,000/= tu. Link kwenye BIO: Yericko Nyerere App - Apps on Google Play