Hotuba ya Rais Magufuli haikuwa hotuba ya Mgombea Urais, ilikuwa Hotuba ya Mgombea Uwaziri wa Miundombinu. Imekosa mvuto mpaka mwisho

Magufuli ana wrong priorities kwenye kununua hiyo midege.

Tena bila kufuata tender process.
 
MH LISSU PITIA HIZI SERA / AHADI, WAELEWESHE WATANZANIA KWENYE KAMPENI UDHAIFU WA HAYA. WATANZANIA WENZETU WAELEWE. AMEZIDI KUKURAHISISHIA KAMPENI.
 
Wakati mwingine wafwasi wa Lissu oneni hata aibu kuongea vitu ambavyo hata Boss wenu anawaona machizi JPM alikuwa anaeleza kile alichofanya miaka 5 ambapo aliwekeza zaidi kwenye miundombinu na anaeleza atakachofanya miaka mingine 5
Watanzania wamesema wanahitaji madege makubwa matatu ya kwenda Ulaya?
 
Awamu ijayo ya 5years Raisi awaongezee watu uwezo wa kulipa kodi.
 
Kwenye kilimo nini kimefanyika zaidi ya kuwasomesha namba wakulima?
Kwenye elimu nini kimefanyika?
Kwenye biashara?
Kwenye afya nini kimefanyika zaidi ya majengo? Afya si majengo.
 
Waziri hawezi toa hotuba ya Hovyo namna ile, ile ilikuwa Fiesta na Diwani ndio anaweza toa hotuba kama ile.
 
Sisi hapa leo tutaonekana tunapiga porojo ila kiukweli kwa mambo aliyofanya Magufuli basi ukimpigia kura ni aibu juu ya nafsi yako!
Nimeyapenda sana haya maandishi yako. Natamani kila mtanzania ayasikie. Kumpigia kura Magufuli ni sawa na kutafuta kifo kwa ndugu jamaa na marafiki zako.
 
Kwa hiyo Akili ya Lissu Hamuijua kuwa ni Kibaraka Wa Mabeberu Wacha Twende na Magufuri Anatutosha Tumeridhika hautaki Kutawaliwa na Wakoroni tenaaa yaani Kwangu Tanzania Kuna Amani Sanaaaaaaa mpka naona watu wanavimbiwa amani hiyo
 
Kwa akili zako finyu ulisikia wapi waziri anagombea .poor you


USSR

Magufuli ana miradi miwili ya 15t+, mpaka sasa kwenye miradi hiyo hakuna hata mmoja uliofikia robo, na kama ni kuweka pesa huko hajafikisha 7t tena zote za mkopo, japo anaongopa kuwa ni fedha zetu za ndani. Iwapo tume isiyo huru ya uchaguzi itamtangaza kuwa rais tena, ndani ya hiyo miaka mitano anapaswa kukopa au tuseme kupata 10t ili miradi hiyo miwili pekee ikamilike kwa 100%. Ni wapi anaweza kupata tena 10t kwa hiyo miradi miwili tu, huku miradi na mambo mengine yakiendelea? Ni wazi kuwa kutakuwa na kodi nyingi kandamizi, ili afakie matamanio yake. Na kikubwa ninachoona ni yeye na genge lake ambalo analazimisha kuliunda sasa, kwa kuchezea uchaguzi ili akae madarakani zaidi ya miaka mitano, lengo hasa ni kutaka kutimiza ndoto zake. Ifahamike yeye ameshinda hivyo hawajui wenye njaa.

Rais anatoa 2t kwa ununuzi wa ndege, na 1t+ ili kujenga madaraja kwenye maji ya kupendezesha, badala ya pesa hiyo kujengea viwanda na kukuza kilimo, halafu anajisifu kuwa ni rais wa wanyonge.
 
Acha kutukana wenzio bwan,kuwa mstaarabu anayoeleza yanaubaya gani kwako?
 
Ni yeye....
Akitoka kwenye kikao cha wafadhili wake. Akiwa ameshibishwa njia mbalimbali za kuiharibu nchi yetu
 
Watanzania wamesema wanahitaji madege makubwa matatu ya kwenda Ulaya?
Kazi ya serikali yeyote Duniani si kukuletea chakula mezani kwako ila ni kuweka mazingira ya kiuchumi,kijamii na kisera sasa unapozungumizia uchumi ni pamoja na miundombinu ,Usafirishaji na mawasiliano sasa kwenye Usafirishaji ni pamoja na Ndege si lazima wote tupande ndege ila Ndege zinaweza kuwa na tija ambapo leo tukiwa na ndege ya mizigo wale wakulima na wavuvi watafaidika sijui chadema mnashindwa vipi kujua vitu vidogo kama hv wakt mnajitapa kuwa chema chenye wasomi
 
Kiitikio: tumeibiwa kura...
Shuka mistari mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…