Hotuba ya Rais Magufuli haikuwa hotuba ya Mgombea Urais, ilikuwa Hotuba ya Mgombea Uwaziri wa Miundombinu. Imekosa mvuto mpaka mwisho

Hotuba ya Rais Magufuli haikuwa hotuba ya Mgombea Urais, ilikuwa Hotuba ya Mgombea Uwaziri wa Miundombinu. Imekosa mvuto mpaka mwisho

Ama kweli Rias Magufuli ana kiburi.

Haiingii akilini anakuja na mipango ambayo kwa namna moja ama nyingine, kwa kiongozi wa nchi ni mipango ya upande mmoja. Alishindwa kuweka mzani wa alipotoka na vitu vyake vs watu aliowaongoza ili ajue afanye nini. Kushindwa kufanya hivyo ni tafsiri kuwa yeye ndiye mpangaji na ni lazima watu wafuate.

Kwanza hii tabia amekuwa nayo kwa miaka mitano iliyopita. Kinachonishangaza ni yeye kuonyesha waziwazi kuwa mwendo ni uleule kwa miaka mitano ama zaidi ijayo. Hii ni hatari sana hasa ukizingatia ishara ambazo zimeanza kujitokeza za kulazimisha ushindi.

Hotuba nzima ya Rias Magufuli imejikita katika kununua ndege na kuongeza kipande cha reli ya kisasa kutoka Dodoma hadi Isaka-Makutopora.

Tuwe wakweli, Rais alipora haki muhimu za wafanyakazi kwa miaka mitano iliyopita na kubebesha mzigo mzito wa kodi kwa watanzania masikini ili kugharamia miradi ambayo mingi ni kama analazimisha ikamilike ndani ya muda mfupi huku akijua athari zake. Kwa jana alipaswa japo kuongea jambo jipya kwa watanzania ambalo linagusa maisha yao moja kwa moja ili ajadiliwe vinywani mwao. Amefeli kabla ya safari ya kampeni.

Mradi wa SGR kwa hesabu zangu mpaka ufike Isaka itagharimu si chini ya trilioni 8. Kwa awamu ya miaka mitano iliyopita mradi umeelea elea tu vipande hadi Morogoro na amefanikiwa tu kulipa trilioni 1.2

Hali hii inanifanya niamini kuwa mabavu anayotumia Magufuli kwenye huu uchaguzi ni ili apate wabunge wote wa CCM na yeye ashinde ili mradi huu ambao nina uhakika ili ukamilike kutoka tarehe ha leo hautachukua chini ya miaka 8! (Ana mpango wa kuongeza muda? Ana mpango wa kupendekeza kodi kandamizi zaidi ili apate fedha?)

Hayo ni yenu watanzania ila kiukweli ukitoka kwako tarehe 28 kwa nia ya kumpigia Rais Magufuli kura basi ni sawa na mtu umetoka kwako na kamba kwa lengo la kuingia porini ili ukajinyonge ufe!

Sisi hapa leo tutaonekana tunapiga porojo ila kiukweli kwa mambo aliyofanya Magufuli basi ukimpigia jura ni aibu juu ha nafsi yako! Nyie sikilizeni wasanii na baadhi ya wafuasi wake ambao wamejitoa kumeza akili za watu ila mjue wanafanya hivyo kwa maslahi yao! Sisi tulimpinga Magufuli mwanzoni kabisa mwa utawala wake kwakuwa tunamjua vyema! Tunaijua akili yake!
Ila yule anaelazimisha kushambuliwa kwake watanzania wamuhurumie uraisi, hotuba yake ni safiiii.
 
Sekta ya afya hajafanya kitu, sekta ya elimu hajafanya kitu, sekta kilimo hakuna chochote...yaani ufipa bwana, akili kisoda. Unadhani serikali inaendeshwa one-dimensional? Lissu anakuja na maendeleo ya watu, maendeleo ya watu bila vitu? Hata Mungu hakuanza kuumba mtu, alianza na mazingira atakayoishi mtu ndio akamalizia na mtu.
 
Kazi ya serikali yeyote Duniani si kukuletea chakula mezani kwako ila ni kuweka mazingira ya kiuchumi,kijamii na kisera sasa unapozungumizia uchumi ni pamoja na miundombinu ,Usafirishaji na mawasiliano sasa kwenye Usafirishaji ni pamoja na Ndege si lazima wote tupande ndege ila Ndege zinaweza kuwa na tija ambapo leo tukiwa na ndege ya mizigo wale wakulima na wavuvi watafaidika sijui chadema mnashindwa vipi kujua vitu vidogo kama hv wakt mnajitapa kuwa chema chenye wasomi
Sio kazi ya serikali kununua madege ya abiria na mizigo.
Madege ya kivita ni sawa.
Na hapo ndipo tofauti ilipo...
 
wakati umekaa nyuma ya keyboard unaandika kuhusu sukari, unga na mchele watu wanapanga namna ya kukuza uchumi kupitia kuboresha mazingira ya utafutaji ardhini, majini na angani.

haileti uhai kuwaza miaka yote utaishi kwa kushindwa kununua kilo moja ya sukari ya kutumia siku 5,mpaka uombe serikali kuipunguza bei.

ndio sababu mgombe wenu anazungumzia kuhusu bima ya afya kwa kila mtu, badala kujenga hospitali kila tarafa na kupunguza kabisa gharama za matibabu,yaani yeye pia mawazo yake juu ya kukua uchumi yamekufa.
Mawazo yako mfu na nahisi funza wameshatafuna kila kitu katika ubongo wako. Lakini ndio Uhuru wenyewe huo.!

Wewe Kama umeshapata kijinafasi Cha kukuwezesha kubadilisha mboga hapo kwako Basi usiwazungumzie watanzania wengine waliopo wilayani na vijijini au hata town.

Huyu Magufuli Ni Rais wa Tanzania nzima na majority hawana uwezo wa kuafford hiyo unayooita kilo tano ya sukari,sembuse kilo moja.
Magufuli anataka kutengeneza gap kubwa Sana ya walionacho na wasionacho yaani wananchi wake watopee kwenye umasikini huku Yeye na familia yake wakineemeka na mema ya nchi.
Hatuwezi kuishi kama kibera.!
 
Sekta ya afya hajafanya kitu, sekta ya elimu hajafanya kitu, sekta kilimo hakuna chochote...yaani ufipa bwana, akili kisoda. Unadhani serikali inaendeshwa one-dimensional? Lissu anakuja na maendeleo ya watu, maendeleo ya watu bila vitu? Hata Mungu hakuanza kuumba mtu, alianza na mazingira atakayoishi mtu ndio akamalizia na mtu.
Hiyo one-dimension ndiyo anayoiapply huyo bwana wako, ndege ndege ,Hana jipya mawazo yalishazikwa na unduli wake.
 
Mawazo yako mfu na nahisi funza wameshatafuna kila kitu katika ubongo wako. Lakini ndio Uhuru wenyewe huo.!

Wewe Kama umeshapata kijinafasi Cha kukuwezesha kubadilisha mboga hapo kwako Basi usiwazungumzie watanzania wengine waliopo wilayani na vijijini au hata town.

Huyu Magufuli Ni Rais wa Tanzania nzima na majority hawana uwezo wa kuafford hiyo unayooita kilo tano ya sukari,sembuse kilo moja.
Magufuli anataka kutengeneza gap kubwa Sana ya walionacho na wasionacho yaani wananchi wake watopee kwenye umasikini huku Yeye na familia yake wakineemeka na mema ya nchi.
Hatuwezi kuishi kama kibera.!
una hasira sana na mtu ambaye hana makosa kwenye maisha yako.

ungeyakasirikia maisha namna hii, ungekuwa na furaha tu na watu wengine.
 
Hoja zake ndio zinaleta hitimisho alilisema muheshimiwa hapo juu.
Hajajikita kwenye ustawi wa jamii hata kidogo,amejikita kwenye materials( vitu visivyoongea), vitu ambavyo havina athari za moja kwa moja kwenye maisha ya wengi.

Je alitakiwa azungumzie nini??
1. Afya ya watu wake, atafanya nini kuboresha afya za watu kama kuongeza hospital na bajeti ya dawa.
2. Haki -atasimamia amani na haki hapa nchini, kwasababu awanu yake ya kwanza tumeshuduia uvunjifu mkubwa wa mifumo yote ya haki kama mahakama.
3. Elimu - ili nalo awamu yake ya kwanza alikuwa nyuma sana, amepunguza pesa za mikopo wa wanafunzi, hajafanya project yeyote ya maana kwenye elimu yetu akitathiminisha na awamu za nyuma zilizopita.
4. Ajira - na ili nalo ameliluka, sina cha kuongeza kwano wote munalifahamu ili.
5. Diplomasia - awamu hii kama munavyojua amegombana na kila jirani unayemjua wewe.
6.
7.
8.
Mutaongezea nyinyi

..katika maeneo yote uliyoyataja anatakiwa aeleze amefanya nini ktk awamu ya kwanza, halafu aeleze atafanya nini ktk awamu yake ya pili.

..sasa hapo ndipo mgogoro unapokuja, kwamba rekodi yake ya kushughulikia mambo hayo siyo nzuri, hivyo haitoi imani kwa wapiga kura kumpa nafasi nyingine.

..Uchaguzi huu ni bora kuchagua wapinzani, ili tupate aina mpya ya viongozi, na kutuma ujumbe wa watawala wote kwamba wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho nchi hii.
 
Sawa basi... Kwenye hotuba ijayo tutamshauri akuahidi kumletea mkeo taulo za kike bure maana kidume umeshindwa kazi hiyo.. I hope hili litakufurahisha sana!
 
Sio kazi ya serikali kununua madege ya abiria na mizigo.
Madege ya kivita ni sawa.
Na hapo ndipo tofauti ilipo...
Hahahahaha kwa nini Ndege za vita iwe sawa?????Chadema bhana but najua wengi wa wapenzi wa Lissu ni wale wanaomchukia JPM kama JPM so hawana option zaidi ya kumpenda Lissu
 
una hasira sana na mtu ambaye hana makosa kwenye maisha yako.

ungeyakasirikia maisha namna hii, ungekuwa na furaha tu na watu wengine.
Itoshe kusema Magu Hana jipya zaidi ya kujitengenezea empire ale mema na ndugu zake, na siku akigusa hicho unachodhani wewe kinakufurahisha katika maisha yako utaomba hallelujah kuu.
 
Akili yako imeishia hapo
Ni kawaida ya viongozi wengi ambao kuwepo madarakani kwao hakutegemei sanduku la kura!!!, siku zote huwa wanakuwa na jeuri tu!!!! Hata aseme zamu hii nitawabuluza kweli kweli!! Cha ajabu Watu watashangilia kweli kweli!! Kuwa huyu ndio mwaume kweli!! Jamani wasomi kuna sehemu nzuri ya kufanyia utafiti huku(uwezo wa akili ya mtz) kama sio mwafrika kabisa!!!
 
..katika maeneo yote uliyoyataja anatakiwa aeleze amefanya nini ktk awamu ya kwanza, halafu aeleze atafanya nini ktk awamu yake ya pili.

..sasa hapo ndipo mgogoro unapokuja, kwamba rekodi yake ya kushughulikia mambo hayo siyo nzuri, hivyo haitoi imani kwa wapiga kura kumpa nafasi nyingine.

..Uchaguzi huu ni bora kuchagua wapinzani, ili tupate aina mpya ya viongozi, na kutuma ujumbe wa watawala wote kwamba wananchi ndio wenye mamlaka ya mwisho nchi hii.
Kabisa
 
Naona wa kurudisha nchi hii kwenye misingi yake ni jeshi tuu.
 
Back
Top Bottom