Hotuba ya Rais Rais Bunge la 12 ni nzuri lakini sikuipenda

Hotuba ya Rais Rais Bunge la 12 ni nzuri lakini sikuipenda

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Imejaa mambo mengi sana ya kutimiza kwa miaka 5. Inatia mashaka kuwa huenda akaanzisha miradi mingi sana itakayolazimu aongezwe muda ili aikamilishe mwenyewe vizuri na kwa ubora kama alivyokusudia.

Ningetamani kama angejikita kwenye umalizaji wa reli, bwawa la umeme, uchimbaji wa chuma na makaa ya mawe na ununuzi wa meli za uvuvi kina kirefu tu.

Ningetamani kama angesema kwa miaka 5 ijayo Gesi yetu itatumika kuendesha magari yooote madogo ya majiji makubwa ili kuokoa pesa tunazonunulia mafuta.

Ningetamani kusikia watu wa Nyumbu kwa kushirikiana na UDSM, VETA, TIRDO, COSTECH wanashirikiana kutegeneza/kuunda mashine za kilimo kama matrekta ya bei nafuu kwa wakulima.

Anamaliza kaabiisa shida ya umeme na maji vijiji vyooote nchini 100% iliyodumu tangu wakati wa mkoloni.

Twende kidogokidogo bila kuumiza sana sehemu nyingine.
 
Sijawahi kuona nchi imeendelea bila elimu na teknolojia yahali yajuu. Kwakweli hajaeleza ataiboreshaje elimu, hajaweka wazi serikali itainuaje kilimo chakisasa chaumwagiliaji kwa nguvu,haongei mbegu na mifugo yakisasa.

Hataji atavyosapoti tafiti na taasisi za tafiti mbalimbali nchini, anaeleza ataitunza amani bila kueleza haki zitakavyotimilizwa,haelezi gesi yetu itatusaidiaje,hasemi mbinu kuzuia magonjwa Bali kujenga Hosp. na kununua madawa,hajaweka wazi atavyoboresha maisha ya watu,ajira zitavyopatikana hasemi anataja tuu idadi yakusadikika.

Anaongea kujenga mameli,mabarabara kununua madege treni namavituvitu mmmno vinavyotoa hela kwenda nje ya mzungukk nchini bila kueleza tutajizatiti kuexport kitugani!

Binafsi sijaisapoti hotuba ile kwenye mia ningeipa 35 yaani D (dhaifu)
 
Paraphrasing the father of Optimality (Pareto) said, you can not be well-off without making someone worse-off unfortunately it is possible to be well-off without making someone worse-off'.

Yote hayawezi kutokea bila kuumiza wananchi lakini inawezekana sana kutimiza yote bila kuumiza wananchi. Ni utashi tu wa kiongozi wetu.
 
Usijali sana,Yale yatakayoweza kufanyika yatafanyika na yatakayo baki atakuja kuyaendeleza atakae kuja mpokea Magufuli tuombe uhai Maisha ni mipango na kupanga ni kuchagua! Hata wwe hapo kichwani mwako unamipango mingi sana ,sema unasubiri upate ma fedha tu tuanze kuwona mipango yako iliyokua kichwani ukiitimiza!!
 
Kwanini umsikilize sana mtu ambaye anaweza kutekeleza ambayo hajaahidi na yale ambayo ameahidi asiyatekeleze, akafanya vitu kwa jinsi anavyojisikia alivyoamka siku hiyo?

Mtu katoka kuiba kura mpaka kipofu anaona, halafu anaongelea utawala bora na demokrasia.

Unamsikiliza ili iweje?
 
Kwa nini umsikilize sana mtu ambaye anaweza kutekeleza ambayo hajaahidi na yale ambayo ameahidi asiyatekeleze, akafanya vitu kwa jinsi anavyojisikia alivyoamka siku hiyo?

Mtu katoka kuiba kura mpaka kipofu anaona, halafu anaongelea utawala bora na demokrasia.

Unamsikiliza ili iweje?
Chapa kazi mkuu usiangalie nyuma Wala kushoto, kulia na mbele yako Hadi 2025, ukija kuangalia kipindi hicho, unaweza usjue hata mahali ulipokuwa, Maana patakuwa pameshabadrika kinoma,

JPM Twende kazi
 
Chapa kazi mkuu usiangalie nyuma Wala kushoto,kulia na mbele yako Hadi 2025, ukija kuangalia kipindi hicho, unaweza usjue hata mahali ulipokuwa, Maana patakuwa pameshabadrika kinoma,

JPM Twende kazi
Kazi ukiiona utaijua hii kazi uweze kuitenganisha na propaganda ya kuhusu kazi?

Hususan kama huangalii pembeni wala nyuma?
 
Paraphrasing the father of Optimality (Pareto) said, you can not be well-off without making someone worse-off unfortunately it is possible to be well-off without making someone worse-off'.

Yote hayawezi kutokea bila kuumiza wananchi lakini inawezekana sana kutimiza yote bila kuumiza wananchi. Ni utashi tu wa kiongozi wetu.
Kwa bahati mbaya sana kiongozi wetu anataka kujiumiza yeye na wananchi.

Ama kwa kujua, ama kwa kutokujua.

Even with good intentions, assuming he has those.

The English have a saying, "The road to hell is paved with good intentions"
 
Usijali sana,Yale yatakayoweza kufanyika yatafanyika na yatakayo baki atakuja kuyaendeleza atakae kuja mpokea Magufuli tuombe uhai Maisha ni mipango na kupanga ni kuchagua! Hata wwe hapo kichwani mwako unamipango mingi sana ,sema unasubiri upate ma fedha tu tuanze kuwona mipango yako iliyokua kichwani ukiitimiza!!
Tunaweza kuwa na mpango wa miaka 100 lakini tukaugawanya katika vipindi vya miaka 5 au 10. Sio mtu mmoja atekelezo yoooote kwa muda mmoja. Ukifanya hivyo nyufa zitakuwepo tu hata kama upendi
 
Kwa nini umsikilize sana mtu ambaye anaweza kutekeleza ambayo hajaahidi na yale ambayo ameahidi asiyatekeleze, akafanya vitu kwa jinsi anavyojisikia alivyoamka siku hiyo?

Mtu katoka kuiba kura mpaka kipofu anaona, halafu anaongelea utawala bora na demokrasia.

Unamsikiliza ili iweje?
Uhodari uko kwenye kusikiliza sio kuongea. Sikiliza zaidi kukiko kuongea, soma zaidi ya wengine kuliko kuandika ya kwako
 
Kujenga kujenga kujenga kujenga tyuuu! Kama tehama ingeimarishwa vema hadi ngazi ya wilaya kuhamia dodoma isingekuwa kipaumbele kwa sasa. Does not add any value to our economy, democracy or social services
Hatujawa na uwezo wa kumiliki teknolojia ya tehama moja kwa moja pili sababu za kuhamia Dodoma bado hazijawa obsolete!
 
Sijawahi kuona nchi imeendelea bila elimu na teknolojia yahali yajuu. Kwakweli hajaeleza ataiboreshaje elimu, hajaweka wazi serikali itainuaje kilimo chakisasa chaumwagiliaji kwa nguvu,haongei mbegu na mifugo yakisasa.

Binafsi sijaisapoti hotuba ile kwenye mia ningeipa 35 yaani D (dhaifu)
Wewe ndio ungepata Rudi kaisikilize Tena.

Kaongelea ufugaji wa kisasa wa kibiashara uongezaji maeneo ya ufugaji na kaongelea viwanda vya nyama kaongelea Hadi ufugaji wa kisasa wa wanyama pori wa kibiashara na ufugaji samaki wa kisasa

Kaongelea Hadi mabwawa ya umwagiliaji uvuvi wa kisasa meli nane za uvuvi bahari kuu kununuliwa

Elimu ya tehama kaongelea vizuri na msisitizo wewe masikio yako ulipeleka wapi imo humu Kama masikio Huna Soma hotuba yake iliyoandikwa Basi

Kaongelea scheme Hadi za umwagiliaji wewe vipi? Una matatizo ya kusokiliza au Kama unayo kasome hotuba iliyoandikwa

You are zero in listening
 
Sijawahi kuona nchi imeendelea bila elimu na teknolojia yahali yajuu. Kwakweli hajaeleza ataiboreshaje elimu, hajaweka wazi serikali itainuaje kilimo chakisasa chaumwagiliaji kwa nguvu,haongei mbegu na mifugo yakisasa.

Binafsi sijaisapoti hotuba ile kwenye mia ningeipa 35 yaani D (dhaifu)
Wewe ndio ungepata Rudi kaisikilize Tena

Kaongelea ufugaji was kibiashara uongezaji maeneo ya ufugaji na kaongelea viwanda vya nyama kaongelea Hadi ufugaji wa kisasa wa wanyama pori wa kibiashara na ufugaji samaki wa kisasa

Kaongelea Hadi mabwawa ya umwagiliaji

Elimu ya tehama kaongelea vizuri na msisitizo wewe masikio yako ulipeleka wapi imo humu Kama masikio Huna Soma hotuba yake iliyoandikwa Basi

Kaongelea scheme Hadi za umwagiliaji wewe vipi? Una matatizo ya kusikiliza au Kama unayo kasome hotuba iliyoandikwa
 
Back
Top Bottom