kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #41
Mkuu uko vizuri. Hayati Rais Mandela alisemaga huko nyuma kuwa Elimu ndio kitu kinachomkutanisha mtoto wa masikini na wa tajiri kwenye meza na ofisi moja. Kama kuna mtu mwenye uchungu sana na walala hoi basi awasomeshee watoto wao na sio kuwapa bodaboda ili wavunje miguu yao. Elimu lazima iwe ile inayoweza kumkutanisha mtoto wa tajiri na maskini sehemu moja darasani na kazini. Sasa hivi mtoto wa maskini hawezi kushindana na mtoto wa tajiri kupata nafasi ya kusoma chuo kikuu. Watoto wanaopata alama za juu za ufaulu kwenye mitihani hawatoki kwenye shule za kata. Watoto wengi wa maskini wanasoma vyuo binafsi vyenye ada kubwa kwasababu ya kushindwa kushindana kupata nafasi kwenye vyuo kama Muhimbili na UDSM.Mkuu 'kavulata', wewe ni GT (Great Thinker) wachache tuliojaliwa kubaki nao hapa JF.
Ni watu kama wewe mnaofanya hata tuliokata tamaa na jamvi hili, tunapokutana na mada kama hii yako, tuzidi kuendelea kuchungulia hapa hata kama ni kwa mara moja moja, tukitegemea tutakuta vito ya thamani kama hii yako.
Umeandika kifupi sana, lakini ni andiko linalojitosheleza kabisa; na kama pangekuwepo na vuguvugu linalopaswa kuwepo kwa mambo mazito kama haya, uzi huu ungechukua nafasi ya kipekee kabisa ndani ya jukwaa hili.
Sasa sijui mjadala huu kweli utafika wapi! Hii ndiyo JF ya sasa.
Umetaja mambo muhimu sana, na kama hotuba iliyabeba yote hayo, hiyo ni ishara mojawapo kwamba hata aliyeiwasilisha hotuba hiyo hakuwa makini. Haya siyo mambo ya kuyazungumzia kiujumla jumla, na juu juu tu. Hiyo ni agenda ya miongo kadhaa sio mambo ya miaka mitano au kumi.
Hiyo pekee ni ishara ya kuonyesha kwamba, hata anayenuia kuyafanya mambo hayo, hajui uzito wa mambo yenyewe upoje.
Sasa mimi ngoja nami nitoe matamanio yangu, kama ningekuwa kwenye nafasi ya kushauri au kusimamia mambo machache kabisa ambayo pengine ndio ungekuwa msingi imara wa kuyatimiza hayo matamanio yaliyotajwa hapo juu kwa ufanisi zaidi.
Katika miaka hii mitano, ningerudi kwenye 'basics' kabisa za kuimarisha ELIMU yetu na KILIMO chetu viwe vya ufanisi mkubwa kabisa.
Kilimo chetu ndio tegemeo kubwa la kuwaondoa waTanzania wengi katika rindi la umaskini. Imarisha kilimo kiwe cha tija, wakati huo huo ukijenga viwanda vya kusindika mazao ya wakulima na kuimarisha soko.
ELIMU yetu imeporomoka sana katika ngazi zote. Tunahitaji kuimarisha elimu isiwe ya kukaririsha tu watu ili waweze kwenda Bungeni kwenda kupiga stori. Tunahitaji elimu wezeshi, ya kuwafanya waTanzania kuitumia elimu katika kutatua matatizo yanayowakabili. Tunataka watafiti wanaoweza kufanya tafiti za nyanja zinazoinukia. Hatuhitaji watafiti kwenda kutafiti dawa za kienyeji, kuloweka mizizi kwenye maji na kutegemea kua dawa humo. Huu ni utafiti uliokwishapitwa na wakati wake. Hili nilinuia kulianzishia mada kabla sijasoma hii ya kwako, na pengine nitalitolea ufafanuzi zaidi kama mjadala huu utakuwa wa mvuto kwa wengi.
Wakati wataalam wanakuna vichwa kuhakikisha mgonjwa atibiwe kwa mahitaji yake na ugonjwa wake (individualized medicine) sisi kwanza ndio tunakumbuka mizizi/magome na majani? Hata Kitengo cha Dawa Asili kilichopo Muhimbili ambacho sasa kina umri wa zaidi ya miaka 30, tafiti kama hizi tayari hazina mvuto tena. Na sio swala la mvuto tu, ni kwamba hakuna kitu cha ziada huko! Nitakueleza kinachotakiwa kufanywa huko, ambacho bila shaka sio alichokusudia mtoa hotuba alipozungumzia swala hili.
ELIMU na KILIMO, hivi viwili vilitakiwa viwe vipaumbele vyetu vya kudumu tokea tupate uhuru wetu. Ingetokea ikawa hivyo, wakati huu, haya mengine yote muhimu uliyoorodhesha hapo kwenye mada na mengine yangekuwa yanatekelezwa vizuri sana hatua kwa hatua wakati huu.
Angalizo hapa ni kwamba sijaandika hapa hayo yasitekelezwe wakati tukiimarisha vipaumbele vyetu. Yatakuwa yanatekelezwa hatua kwa hatua. Kiongozi mmoja hawezi kamwe kutekeleza mahitaji yote muhimu katika ngwe yake, hata kama anayomipango ya kujiongezea miaka ya kudumu kwenye utawala wake.
Hata elimu inayotolewa haitoi wahitimu wanaoweza kushindana kwenye free market ya ajira. Hata maprofessor wetu ni wepesi sana kiviwango na hata kupambanua mambo. 99.1% ya maprofessor wetu wako kwenye payroll za serikali na wale waliostaafu wako kwenye payroll za taasisi binafsi wameajiliwa tena. Professor anashindwa kutoa ajira kwa watu japo 20. Elimu yetu lazina itazamwe upya.