Hotuba ya Rais Rais Bunge la 12 ni nzuri lakini sikuipenda

Mkuu uko vizuri. Hayati Rais Mandela alisemaga huko nyuma kuwa Elimu ndio kitu kinachomkutanisha mtoto wa masikini na wa tajiri kwenye meza na ofisi moja. Kama kuna mtu mwenye uchungu sana na walala hoi basi awasomeshee watoto wao na sio kuwapa bodaboda ili wavunje miguu yao. Elimu lazima iwe ile inayoweza kumkutanisha mtoto wa tajiri na maskini sehemu moja darasani na kazini. Sasa hivi mtoto wa maskini hawezi kushindana na mtoto wa tajiri kupata nafasi ya kusoma chuo kikuu. Watoto wanaopata alama za juu za ufaulu kwenye mitihani hawatoki kwenye shule za kata. Watoto wengi wa maskini wanasoma vyuo binafsi vyenye ada kubwa kwasababu ya kushindwa kushindana kupata nafasi kwenye vyuo kama Muhimbili na UDSM.

Hata elimu inayotolewa haitoi wahitimu wanaoweza kushindana kwenye free market ya ajira. Hata maprofessor wetu ni wepesi sana kiviwango na hata kupambanua mambo. 99.1% ya maprofessor wetu wako kwenye payroll za serikali na wale waliostaafu wako kwenye payroll za taasisi binafsi wameajiliwa tena. Professor anashindwa kutoa ajira kwa watu japo 20. Elimu yetu lazina itazamwe upya.
 
Basi ujue, karibu kila mhadhiri na wasomi wengine wote ndoto zao zimeelekezwa huko! Wengi wa hawa watu ;aspirations' zao kubwa ni kuwa kama Kabudi. Ni wachache, kama wapo wana-'commitment' ya kweli na kazi zao.
👍👍👍
 
Hata tafiti wanazofanya vyuoni ni kwaajili ya kupata hela za utafiti lakini hawamaanishi hasa kutatua tatizo kwenye jamii. wanapika matokeo yatakayosaidia wahisani wampe pesa. Tafiti zao zinazingatia kwenye kupata pesa za wafadhaili na kutokuwaudhi watawala
 
Mkuu uko vizuri. Hayati Rais Mandela alisemaga huko nyuma kuwa Elimu ndio kitu kinachomkutanisha mtoto wa masikini na wa tajiri kwenye meza na ofisi moja
Ni vizuria kabisa kumkumbuka Mandela kwa msimamo huo; lakini usisahau sisi wenyewe hapa Tanzania tulikuwa na kiongozi aliyeamini hivyo na akatimiza aliyaoyaamini juu ya hali hiyo.

Mwalimu Nyerere alihakikisha ufukara wa mzazi kamwe usingekuwa kikwazo cha mtoto kutofaidika na elimu kwa kadri ya uwezo wake, bila ya kuwepo tofauti na yule anayetumia utajiri wake.

Matokeo yake ndio hao akina Kabudi wengi waliopata elimu kutokana na juhudi hizo. Kwa bahati mbaya hawa vijana wa wakati huo waliopewa "akiba ya mwisho ya chakula kijijini kwao ili kukinusuru kijiji na janga la njaa", leo hii ndio wanawakandamiza wanakijiji waliotakiwa kuwasaidia kuleta neema ya kijiji. Leo hii wanawanyima haki zao kwa visingizio vya 'kuwaletea maendeleo'. Wanasahau kuwa maendeleo hayaletwi na wao, bali wananchi wenyewe ndio watakaojiletea maendeleo.
 
Hata elimu inayotolewa haitoi wahitimu wanaoweza kushindana kwenye free market ya ajira.
Unaongelea fani zipi za arts ? kama ni hizo hata mtu asome kenya au ulaya akija Tanzania hawezi compete

Fani za sayansi aliyesoma aweza compete popote mfano daktari ,engineer ,mwalimu wa hisabati,fizikia ,kemia,biologia nk ni moto wa kuotea mbali ila kama ni hayo masomo ya porojo hata usome ulaya ukija Tanzania kwenye free makert kibarua unacho kwenye competition
 
Hata usome nini hapa Tanzania kwenye vyuo vyetu utapata tabu sana kwenye competition, lazima utahitaji msasa. Tulikuwa na dk pekee wa moyo tanzania lakini akakubali kwenda kuwa katibu mkuu wizara ya maji.
 
Hapo kwenye elimu, amefanya yafuatayo miaka 5 iliyopita:
1) Utoaji elimu bila malipo, elimu isiyo na viwango, msingi hadi form 4
2) madawati kwa kiasi fulani, lakini upungufu mkubwa wa majengo, na idadi kubwa ya watoto wanaketi chini
3) Uvurugaji mkubwa wa elimu ya chuo kikuu:
i) Wenzetu profesa anaendelea kutumika mpaka atakapochoka kabisa. Magu kaleta utaratibu unaowakatisha tamaa kabisa.
ii) Magu anadai vyuo vikuu vitoe gawio kwa serikali badala ya fedha hiyo kidogo kuelekezwa kwenye tafiti.
iii) Serikali ya Magu haiajiri, na amevuruga sekta binafsi. Mikopo anayotoa kapandisha riba, ajira hakuna. Atakuja nyonga watu kwa msononeko

4) Maslahi kwa walimu na wafanyakazi wote ni sifuri.

Sasa miaka 5 ijayo hakuna dalili ya maboresho yoyote. Hajui alipokosea, hakuna wa kumwambia atakapokosea sasa maana hakuna upinzani, vyombo vya habari kavididimiza, nchi nzima sasa ni kumwimbia mapambio. Atajenga mabarabara ba kununua madege kwa kasi na nguvu zaidi, bila kujali ulinganifu wa uchumi
 
Hali vyuo vikuu ni mbaya sana, walimu na wanafunzi wote hawajui kiingereza wala kiswahili. Mitaala ya vyuo vikuu ina somo la English course (eti wanaita communication skills), vijana wanaotoka shule za umma hawajiwezi kabisa katika lugha ya kufundishia na wale wanaotoka shule za private wamekaririshwa majibu ya maswali hawawezi kujisomea wenyewe na kudadavua walichokisoma wanapofika vyuoni.
 
Kavulata hayo yooooote uliyotaja yatafanyika na kukamilishwa kwa umakini na usahihi wa AJABU. Hayo yote yamo kwenye ILANI YA CCM, tena in very detailed notes na kwa kila mkoa. Pata muda uisome baada ya kui - download kutoka tovuti ya CCM. Kila kitu kiko HADHARANI ndugu yangu. Halafu, utekelezaji wa ILANI hiyo ndiyo TEKE JINGINE LA MAUAJI litakalotumika dhidi ya wapinzani come 2025 elections kwa sababu haitaacha kufukua kila jiwe, yaani itafukua kila jiwe la kiutekelezaji.
 
Hizo details nyingine wanazotaka, ZIMO KWENYE ILANI JAMANI! Nendeni mkayasome huko.
 
Mimi sikuelewa kauli hii aliyeielewa anieleze: "Uhuru na haki bila wajibu ni bure. Nahisi wamenielewa".
 
Nenda pale UDSM, maabara ya kemia ya wanafunzi 40 sasa wanahudhuria 200, utazania wapo kwenye mkutano wa ccm.

Kule Engineering, wataalamu mafundi wa kuongoza practicals za wanafunzi wanastaafu hakuna watu wa kuwaachia ujuzi walionao, ambao utausomea wapi? Maana hawa wapo toka enzi mjerumani amezifunga na kuwafundisha, na wakaenda ujerumani kwa mafunzo zaidi. Leo Magu haajiri technicians wapya, waliopo wanaondoka na ujuzi wao. Hakuna anayejali.
 
Hajazungumzia katiba mpya ambayo itatoa dira ya jinsi ya mfumo wa utawala utakao endana na karne hii ya tehama. Bila mfumo wa kiutawala unaoendana na matakwa ya karne hii ya tehama yote aliyotaja kutekeleza ni kusadikika.
 
We need a full and comprehensive Constitutional Reform to ensure freedom and justice prevails to all. Not "Mateke ya mauwaji" to the opposition.
 
Mnapomsifu mkiambiaji usisahau kumsifu na anaemkimbiza. Kama CCM itafanya vizuri kwaajili ya 2025 basi sisi wananchi hatunabudi kuisifu CCM lakini bila kusahau kuisifu Chadema. Huu ni ushahidi kuwa upinzani umekomaa nchini kiasi cha kuisukuma ccm itende yale ya wananchi. Na hii ndiyo sababu ya baba wa Taifa kupigania uwepo wa vyama vingi vya siasa hata baada ya 80% ya wananchi kuvikataa. Bila ya chadema imara 2015 CCM isingempendekeza Rais JPM kuwa mgombea wake. Hivyo hata JPM atalazimika kuishukuru chadema na Lowassa waliosababisha yeye apewe nafasi hiyo kukabiliana na Lowassa.

Pamoja na hayo ni heri kufanya vitu vichache kwa ubora wa hali ya juu kuliko vitu vingi vya juujuu. Mfano, tulijenga vituo vya afya vingi lakini hakuna dawa, vifaa tiba, watumishi, maji na fedha za uendeshaji. Tumejenga shule nyingi lakini hakuna walimu, viti, maabara, mabweni, na ukaguzi
 
Hana Mpya unapata wapi muda wa kumsikiliza mtu ambaye hakuchaguliwa kihalali.
 
Walimu vijana wa vyuo vikuu kwa kweli wanatisha. Ni Doti Komu ya kufa mtu. Ni kweli wazuri wapo, lakini wabovu ni asilimia kubwa zaidi.

Ni vicious circle inayoteremka chini. Hili ni Bomu la Nuclear
 
Walimu vijana wa vyuo vikuu kwa kweli wanatisha. Ni Doti Komu ya kufa mtu. Ni kweli wazuri wapo, lakini wabovu ni asilimia kubwa zaidi.

Ni vicious circle inayoteremka chini. Hili ni Bomu la Nuclear
Eti kigezo cha kuwa mwalimu chuo kikuu ni GPA, kigezo hiki pekee sio halisia hasa katika katika kuwapata walimu hasa katika mataifa maskini ambayo rushwa za aina zote zipo. Waweza kuta MTU ana GPA kubwa lakini hajui kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…