Novemba 2020 wakati Rais wa awamu ya Tano Hayati Magufuli akihutibia bunge katika ufunguzi wa bunge la 12 MATAGA waliibuka na kumsifia Rais Magufuli kwamba ameweza kukariri hotuba yote, MATAGA walimsifia kuwa Rais Magufuli alikuwa haangalii wala kusoma popote hotuba yake wakati akihutibia bunge.
MATAGA waliendelea wakisema Magufuli ana rekodi ya muda mrefu ya kukariri mambo wakirejelea akiwa waziri wa Uvuvi kuwa aliweza kuwataja samaki wa ziwa victoria, MATAGA walisisitiza na kuongeza kuwa akiwa waziri wa ujenzi alikuwa na uwezo wa hali ya juu wa kutaja barabara zote zilizo jengwa ikiwa ni pamoja na kilometa zote bila kusoma popote, huku wakisema kuwa anachokifanya bungeni siyo mara yake ya kwanza na hivyo amekariri HOTUBA YOTE naam hao ndiyo MATAGA.[emoji1787][emoji119]
Jana Kama kawaida yao wameibuka tena na kusema Samia naye ameweza kukariri hotuba yote bila kusoma popote.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23], Hakika MATAGA ni Wavivu Sana wa kufikiri.
Vioo angavu vilivyokuwa vinaonekana mbele ya Rais Samia Suluhu vinaitwa Teleprompter ndiyo ni TELEPROMPTER, hiki ni kifaa ambacho humsaidia mtu anayezungumza na maandishi ya elektroniki ya hotuba, kifaa hiki huelekeza lensi ya maandishi moja kwa moja kwenye macho ya mzungumzaji kwa kutumia vioo hivi angavu vilijulikanavyo Kama teleprompter, naam hiki ndicho kifaa kiitwacho teleprompter.
Hii siyo mara ya kwanza marais wa nchi yetu kutumia kifaa hiki kusomea hotuba, Kwa mara ya kwanza kifaa hiki kilitumika na Rais Kikwete mwaka 2014 wakati wa ufunguzi wa bunge la Katiba, wakati huo Anna Semamba Makinda akiwa spika wa bunge la Tanzania. (Pangusa picha kulia kuona, Swipe right to see). Kifaa hiki kilitumika na Rais Hayati Magufuli katika ufunguzi wa bunge Nov 2020 Kama nilivyosema awali, na jana kifaa hiki kimeweza kutumika na Rais wa awamu ya Sita mama yetu Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia bunge na Watanzania bungeni Dodoma. Sasa MATAGA utasikia wakisema rais amekariri hotuba....AJABU!!
Teleprompter ni kifaa kilicho gunduliwa rasmi mwaka 1950 na Fred Barton Jr, Hubert Schlafy pomoja na Irving Berlin Kahn.
Kwa mara ya kwanza Rais wa Marekani Bwana Lyndon Johnson alitumia teleprompter wakati akitangaza Sheria ya Haki za Kiraia ya 1964.
Ndugu zangu MATAGA tumeelewana?? Wasukuma pele nyuma je??
Acheni kutuletea stori za abunuwasi hapa kuwa rais anajua kukariri na hasomi popote...Tumeelewana???.
[emoji2398] Kumbusho Dawson Kagine
View attachment 1761674View attachment 1761675View attachment 1761671View attachment 1761672View attachment 1761673View attachment 1761676