Uchaguzi 2020 Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Juni 08, 2020

Alieandika hii taarifa aliyosoma TL Mungu anamuona.

Hotuba gani ya Rais haina mvuto? Haisisimui? Imeegemeea Wanasiasa, Mahakama na Wateswaji tu?

Ina maana Kipaumbele cha TL ni Sheria na Magufuli?

Nimeshindwa kuelewa. Bora mamvi alijisemea ELIMU, ELIMU, ELIMU.
 
Zile ni sihu za nguvu, one has to bank on flaws Jiwe is making. Unadhani wau wana amani? Hata kwa Jameh, walikuwa wanamuimbia mapambio kama hapa!

Jameh tofauti kbsa jamaa saikolojia imeyumba, ardhi hii hagusi kamwe mwaka huu
 

Kumbuka hii ni hotuba ya kutia nia kuomba ridhaa ktk chama kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais.

Kama alivyosema Rais Mtarajiwa Mh. Tundu Antipas Lissu, baada ya kupitishwa ataendelea kutoa hotuba motomoto ktk miezi, wiki, siku na masaa kuelekea October 2020.

Hii ni kuujulisha umma, CHADEMA na ni mvua za rasharasha, mambo bado .
 
Jameh tofauti kbsa jamaa saikolojia imeyumba, ardhi hii hagusi kamwe mwaka huu
Chukulia hypothetical scenario kama hii: Akigusa ardhi hii akauawa , "mabeberu" wakasema tunalipiza kisasi, Je ya Quasem Soleimani mtayamudu? Nasema kwa mfano tu... mfano tu maanana Jameh aliapa kutoondoka, majeshi ya ECOWAS yaliposogezwa mpakani akomba POOOO (vijana mnaita)
 
Nilikua na njaa....baada ya kusoma hii hotuba neno kwa neno na mstari kwa mstari nimeshiba na imenigusa sana..nasema hivi Mheshimiwa Rais mtarajiwa Tundu Antipas Lissu una kura yangu tarehe 25 October 2020....na nitaamka mapema nikiwa hai na afya tele Mungu apokee dua zangu.

Niwaombe wapinzani mshirikiane bado mnahitaji nguvu ya pamoja kuiondoa CCM yenye dola na pesa.Mwisho TUME HURUTUME HURU TUME HURU JAPO MLICHELEWA KUIOMBA.

nasimama pamoja na Lissu.
 

Brother inaonekana hujui kuchambua hotuba za Wanasiasa na Watu makini! Hii ni kutangaza nia tu siyo kampeni ya Urais. Kwa sheria na taratibu mgombea Urais akishateuliwa na Chama chake ndipo atatangaza Sera na Ilani ya Chama chake.

Kuhukumu Sasa hivi eti hajaongea sijui kuhusu Uchumi, Elimu, Afya etc ni kuonesha hujielewi. Muda bado sana ni hapo Oktoba mbichi na mbivu zitajulikana!

TAL-2020 for Presidency✌
 
Hivi alikimbilia ubelgiji au alikwenda kutibiwa? Inakuwaje mnakosa maarifa nyinyi kizazi cha laana?
Kwa hiyo bado anatibiwa? Au ndiyo aneruhusiwa kwamba kapona
Au kule USA na Ujerumani alikuwa wodini?

Ndugu, tunaitaji presidential candidate wa maana, siyo huyo ambaye hata neno moja LA kukuza uchumi hajatamka kinywani mwake
 

Ndoto za ujima kbsa ila ni heri kufikirika kuliko kutofikiri kbsa, atarudi Kama kambona muombeeni heri.
 
Hana jipya,ngonjera zilezile tu.Eti lissu apambane na Magufuli? Kwa lipi kwanza? Ana legacy ipi Tanzania? Yule si mropokaji tu,hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kushabikia au kuchagua zwazwa kama lile.
 
Eti wana JF kuhusu wawekezaji boss Tundu amesemaje? Make JPM alivyozuia mchanga wao alisema taifa tutashitakiwa na kufilisiwa.
 

Nitarejea kuchambua hotuba hii, kifungu kwa kifungu, ila lililo wazi ni nia yake kulipiza kisasi kwa dhana/hisia kwamba Serikali ilihusika na shambulizi dhidi ya maisha yake na kuondolewa kwenye nafasi yake ya ubunge. Nanukuu:

Kwa sababu nimekuwa mmojawapo wa wahanga wakubwa wa Tanzania ya Magufuli, ninafahamu maana ya kuishi chini ya utawala wa aina hii ambao tumekuwa nao kwa miaka mitano sasa. Nina uwezo wa kuwafuta machozi wale waliofanywa wajane na yatima na vilema wa utawala huu. Nina uwezo wa kutibu majeraha na makovu mengi ambayo wamesababishiwa watu wetu wengi.

Spika Ndugai ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, licha ya dhamana hiyo kubwa ya uongozi aliyonayo kitaifa, yeye sio Baraza la Maadili, na wala sio Mwenyekiti au mjumbe wake. Kwa sababu hiyo, uamuzi wa Spika Ndugai wa kunifutia ubunge haujaniondolea sifa za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au nafasi nyingine yoyote ya uongozi.


Kwa ufupi, hotuba yake imejaa nadharia zisizoweza kuthibitishwa yaani ni ndoto ya kujenga nchi ya kufikirika. Kwamba hakuna nchi duniani yenye hali anayoizumngumzia na akitaka nchi ya aina hiyo atapaswa kuwa na watu zaidi ya malaika kwani hata Mungu huadhibu walio na makosa na ndiyo maana maisha baada ya kifo, kila mwanadamu atahukumiwa na kuwekwa milele motoni, toharani au ahera.
 
Mmeshakubaliana na Mwenyekiti Mbowe kwamba hatabadilisha gear angani?
Kwa mwenyekiti suala siyo kugombea peke yake. Issue ni kama ukigombea unaleta wabunge wangapi ndani ya Chama. Ndiyo maana biashara aliyoifanya na Lowasa ilikuwa na faida kubwa.

Swali, je Tundu Lissu anaweza kutuongezea wabunge? au ndiyo tunarudi enzi za wabunge watano?

Kumbukeni nyuma ya pazia kuna mtu anaitwa Mbatia.

Najua Mwamba atakuja na plan B kama alivyofanya 2015
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…