Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Watu wanakosea kuleta ushabiki wa vyama vya siasa kwenye mambo ya msingi ya taifa letu.

Ushabiki wa vyama umetufikisha pabaya sana umetuondolea mpaka uzalendo wetu kwa taifa letu.

Hii katiba siyo ya CCM, CUF, NCCR Mageuzi wala vyama vingine vya siasa ni katiba ya taifa letu.

moja ya sababu ya ujio wa vyama vingi ndo hiyo,tunagombana mpaka ngaz ya familia kwa tofaut za kisiasa,mtu wa chama fulan hata akiongea ponit as long mpo tofaut basi watu wanampinga
 
Jaji amesema hatua hii inamuondoa Rais kwenye bunge kwani kwa kuwa na Mawaziri ndani ya bunge Hilo kunalifanya bunge kushindwa kuisimamia serikali ipasavyo kwa kuwa serikali ni sehemu ya bunge Hilo.

Amesema Mawaziri watateuliwa na Rais NA kuthibitishwa na bunge . Aidha , rasimu ya Katiba inapendekeza kuwa Rais achaguliwe kwa kupata kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote .

Rais Mara baada ya uchaguzi na kutangazwa na Tume ya uchaguzi anaweza kufikishwa mahakama ya rufaa kuhoji uhalali wake na mgombea yeyote wa kiti hicho aliyeshindwa na Shauri hilo kuamuliwa ndani ya mwezi mmoja.

Jaji Warioba amesema Rasimu ya Katiba inapendekeza kuwepo NA ukomo wa wabunge wa miaka 15 ya kukalia kiti hicho mfululizo ili kuondoa dhana ya umiliki wa ubunge na kuimarisha uwajibikaji.

Hakutakuwepo na uchaguzi mdogo endapo Mbunge atafariki badala yake nafasi hiyo itazibwa na jina litakalokuwa kwenye orodha zilizoandaliwa NA vyama vya siasa vyenye wabunge husika na kuwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi.

Aidha, Spika na Naibu Spika hawatatokana na Mawaziri, Naibu Waziri NA wabunge ili kupata viongozi ambao hawataelemea upande wowote.
 
Mtakubali tu mtapinga vitu viko wazi; watanzania wote sasa wamesikia sijui mtapotoshea tena watu wapi. Mnamtukana mzee wa watu hadharani bila kosa, kisa kusema ukweli. Hii laana lazima iwatafune. Otherwise kina nape, majura, na wengineo mliomtukana waroba muobe msamaha mbe;le ya watanzania. Warioba amewakosea nini. Warioba amenifanya leo nijikute natokwa machozi, yaani nimelia km dakika tano hivi bila kujua nini kinaniliza. Da Mungu ampe maisha marefu mzee weu Joseph Sinde Warioba. Du kweli watz... bas tu.

Sijui ni hisia sijui nini, kwa kweli sijui, Mtanzania mimi leo nimesisimkwa na mwili kwa nondo ambazo mzee Warioba alikuwa anazitoa! Kuna wakati nilikuwa nasisimkwa na presentation hadi natokwa na machozi. Mwenzangu niliyekuwa nae akasema kaka unahisia, nikamwambia unajua hamna kitu bora kama facts. Unajua kwa sie wengine tuliosomea hesabu hamna jibu la kubahatisha, ni straight, na ndicho alichofanya leo mzee Warioba!
 
Lissu anahusika vipi na hotuba ya Warioba, lini wazenji walimchukia Warioba.
 
Vijana wenzangu tuwe macho sana na hawa wazee, hili swala la katiba tusiingie kichwakichwa matokeo ya serikali mbili au tatu yatalifaidisha kundi mojawapo ndani ya ccm na sio wewe wala ndugu yako, CCM imegawanyika mara mbili kuna wa serikali 2 na tatu kwa maslahi bnafsi ila wote ni marafiki na hawako tayari kuharibu chama wako pamoja, wanapambana kwa hoja jioni wanakula bata huku wakipeana tano. Cha msingi tuconcetrate na na maswala muhimu kwenye katiba yetu kama afya, miundombinu, elimu na malazi. katiba inasema nini juu ya haya, hata wao wakiamua nchi iongozwe na jaji mkuu au spika au jeshi hayo ni yao wanasiasa. Usifikiri Warioba,JK,Sitta,Lowassa +wana ccm kwa ujumla lao sio 1. chondechonde tuache mihemko kama wakenya sasa wanaandamana kila kukicha na watawala ni walewale wanabadilishana nyadhifa tu.:flypig:

karibu tujadili na kuelimishana kama vijana maana sisi ndo bado tuna safari ndefu kwa mstakabari wa nchi yetu.

Pamoja na mawazo yako kumbuka hoja ya serikali mbili au tatu haiepukiki kuijadili, kwani hayo uliyosema utayafanikisha katika serikali ipi 'fikiria tena'
 
haya ndiyo mawazo mgando sasa tunayosema. warioba hajaongea maneno kutoka kichwani kwake ww mbwiga hayo ni matokeo ya utafiti na mawazo ya wananchi waliosoma na wanaojua historia ya nchi na c washamba kama wewe
 
ndo kusema wameelewa wamechanganyikiwa or.......... malizia mengine........
 

Attachments

  • 1904051_609078335837488_469303939_n.jpg
    1904051_609078335837488_469303939_n.jpg
    6.8 KB · Views: 260
Warioba akzidi nifurahisha alipotoa mifano ya makundi yaliyosuggest serikali 3..akasema hadi taasisi za serikali na mihimili km Bunge....akasema na baraza la mawaziri la Zenj wote walikuwa ktk serikali ama 3 ama muungano wa mkataba ambao ujumla wake ni serikali zilezile 3... Maccm bado ulevi unawasumbua.
 
Mungu akubariki Ritz kwa kuutambua na ujasiri wa kuukiri ukweli.by the way vyama na sera zinapita lakini umoja na nchi yetu vitabaki milele. aidha hapa hakuna mshindi kama kalenga bali watanzania ndio tumeshinda kwa ujumla wetu

Hata mimi nawaomba wanaopost sasa wasiseme nani kashinda nani kashindwa ila tuiunge mkono Rasim tu ili ipite! Kwa dhati kabisa tume haikuwa na nia mbaya, na hayo yalikuwa maoni ya Wananchi!
 
Msalani siyo lazima uchangie kila thread. "Solid Food for Matured People Only, not for Babies". Unafahamu umafia wa Mahakama zetu? Sometimes zinaendeshwa kama "Kangaroo Courts" kwenye "Banana Republics"
 
JK atakacha majungu kesho kutwa km alivyowatosa CCM ktk maoni ya CDM ..CCM walikuja juu sana CDM walipoingia Ikulu na k umwacha JK akiwa na mawazo yao..CCM wakaishia kudai kuwa CDM wali enjoy juice ya ikulu...eti waliona wivu
 
Nimependa busara ya Tume ya Warioba. BMLK liige busara hizo:
Hata tulipopata matatizo ya kufikia uamuzi kwa suala lolote hatukukimbilia kupiga kura. Tulijifungia kwenye vikundi vya watu wenye mawazo kinzani na mwisho tukafikia maridhiano na muafaka. Dira yetu ilikuwa Maslahi ya Taifa. Hatukupiga kura hata mara moja kwa jambo lolote wala kuwa na mawazo mbadala. Kila Ibara iliyomo kwenye Rasimu ya Katiba ambayo ninaiwasilisha katika Bunge Maalum la Katiba, inaungwa mkono na kila mmoja wetu.

Hiyo haina maana kwamba kila mmoja wetu ameacha imani yake, itikadi yake na msimamo wake. Kuna mambo ambayo kila mmoja wetu amebaki na imani yake na msimamo wake. Kwa mfano, kwenye suala la Muungano tupo tunaoamini muundo unaofaa ni Serikali Moja, tupo tunaoamini Muundo wa Serikali Mbili, tupo tunaoamini Serikali Tatu na tupo tunaoamini Muungano wa Mkataba. Tunachoamini wote kwa pamoja ni umuhimu wa kuendelea kuwepo na kudumu kwa Muungano. Baada ya kuwasikiliza wananchi, dira yetu imekuwa ni maslahi ya Taifa na siyo maslahi ya makundi yetu au nafsi zetu.
 
Back
Top Bottom