Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,593
- 5,581
Watu wanakosea kuleta ushabiki wa vyama vya siasa kwenye mambo ya msingi ya taifa letu.
Ushabiki wa vyama umetufikisha pabaya sana umetuondolea mpaka uzalendo wetu kwa taifa letu.
Hii katiba siyo ya CCM, CUF, NCCR Mageuzi wala vyama vingine vya siasa ni katiba ya taifa letu.
Mtakubali tu mtapinga vitu viko wazi; watanzania wote sasa wamesikia sijui mtapotoshea tena watu wapi. Mnamtukana mzee wa watu hadharani bila kosa, kisa kusema ukweli. Hii laana lazima iwatafune. Otherwise kina nape, majura, na wengineo mliomtukana waroba muobe msamaha mbe;le ya watanzania. Warioba amewakosea nini. Warioba amenifanya leo nijikute natokwa machozi, yaani nimelia km dakika tano hivi bila kujua nini kinaniliza. Da Mungu ampe maisha marefu mzee weu Joseph Sinde Warioba. Du kweli watz... bas tu.
Kwa mahakama zetu hizi ..ambazo hata mwanasheria wa serikali..alishindwa na magaidi waliochoma kanisa hadharani?
Lissu ni mwanasheria mahiri sana. Namkubali sana, ana uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja, ni objective and very open-minded.
Vijana wenzangu tuwe macho sana na hawa wazee, hili swala la katiba tusiingie kichwakichwa matokeo ya serikali mbili au tatu yatalifaidisha kundi mojawapo ndani ya ccm na sio wewe wala ndugu yako, CCM imegawanyika mara mbili kuna wa serikali 2 na tatu kwa maslahi bnafsi ila wote ni marafiki na hawako tayari kuharibu chama wako pamoja, wanapambana kwa hoja jioni wanakula bata huku wakipeana tano. Cha msingi tuconcetrate na na maswala muhimu kwenye katiba yetu kama afya, miundombinu, elimu na malazi. katiba inasema nini juu ya haya, hata wao wakiamua nchi iongozwe na jaji mkuu au spika au jeshi hayo ni yao wanasiasa. Usifikiri Warioba,JK,Sitta,Lowassa +wana ccm kwa ujumla lao sio 1. chondechonde tuache mihemko kama wakenya sasa wanaandamana kila kukicha na watawala ni walewale wanabadilishana nyadhifa tu.:flypig:
karibu tujadili na kuelimishana kama vijana maana sisi ndo bado tuna safari ndefu kwa mstakabari wa nchi yetu.
Mungu akubariki Ritz kwa kuutambua na ujasiri wa kuukiri ukweli.by the way vyama na sera zinapita lakini umoja na nchi yetu vitabaki milele. aidha hapa hakuna mshindi kama kalenga bali watanzania ndio tumeshinda kwa ujumla wetu
Duh! Mkuu Kibanda alifanyaje?
Kama vipi Warioba avae miwani!
wamesemaje jamani?? tupeni nondo...wanataka govt 3 au moja?
Hata tulipopata matatizo ya kufikia uamuzi kwa suala lolote hatukukimbilia kupiga kura. Tulijifungia kwenye vikundi vya watu wenye mawazo kinzani na mwisho tukafikia maridhiano na muafaka. Dira yetu ilikuwa Maslahi ya Taifa. Hatukupiga kura hata mara moja kwa jambo lolote wala kuwa na mawazo mbadala. Kila Ibara iliyomo kwenye Rasimu ya Katiba ambayo ninaiwasilisha katika Bunge Maalum la Katiba, inaungwa mkono na kila mmoja wetu.
Hiyo haina maana kwamba kila mmoja wetu ameacha imani yake, itikadi yake na msimamo wake. Kuna mambo ambayo kila mmoja wetu amebaki na imani yake na msimamo wake. Kwa mfano, kwenye suala la Muungano tupo tunaoamini muundo unaofaa ni Serikali Moja, tupo tunaoamini Muundo wa Serikali Mbili, tupo tunaoamini Serikali Tatu na tupo tunaoamini Muungano wa Mkataba. Tunachoamini wote kwa pamoja ni umuhimu wa kuendelea kuwepo na kudumu kwa Muungano. Baada ya kuwasikiliza wananchi, dira yetu imekuwa ni maslahi ya Taifa na siyo maslahi ya makundi yetu au nafsi zetu.