Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hakuna uchaguzi mdogo chama ambacho kitampoteza mbunge wake kitapendekeza awe mbunge.

Wabunge wanapga kelele,Sitta anatuliza.

Nyambari naye anafuatilia JF.
 
Kuna hoja nzito sana anaziwasilisha Warioba kweli Wananchi waheshimiwa kwa Mawazo yao walioyatoa kwenye Tume.
 
Hatua ya baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupiga kelele na kulivunja jana wakipinga uvunjaji wa kanuni, imepokewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wasomi na wanaharakati, huku baadhi wakisema ilikuwa ni sahihi na wengine wakipinga.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Haji Semboja alisema kitendo hicho ni matokeo ya kutokufuatwa kwa kanuni na taratibu.

“Kama walikubaliana aanze kuzungumza Rais (Jakaya) Kikwete na baadaye Jaji Joseph Warioba na hilo likakiukwa, walikuwa na haki ya kufanya kile walichokifanya. Unajua Bunge hili lina watu wenye fikra na mitizamo tofauti na ambao wanataka kila jambo liende kwa kufuata misingi na kanuni zilizopo. Nadhani sasa tutaanza kuona umakini wa wajumbe wa Bunge hili.”

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni ya Bunge hilo, Profesa Costa Mahalu alishauri kuitwa haraka Kamati ya Bunge Maalumu la Katiba ili kunusuru vikao vya Bunge hili kuendelea.

Akizungumza baada ya kuvunjika kikao hicho jana jioni, Profesa Mahalu alisema hoja ya kuwa Mwenyekiti Sitta amevunja kanuni kwa kuanza kumpa nafasi Jaji Warioba badala ya kuanza na Rais Kikwete zitamalizwa kwa mazungumzo.

Profesa Mahalu alikiri kuwa kanuni zilizopitishwa ziliweka utaratibu, lakini akasema kwa kuwa suala la kanuni ni la kisheria, kila mtu anaweza kuwa na tafsiri yake.

“Kwa mazingira haya, siwezi kusema nani ana makosa kwani kila mtu anavutia kwake, lakini muhimu hapa ni kukaa na kufikia maelewano,” alisema.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Pandu Amir Kificho alipotakiwa kuelezea hatua zitakazochukuliwa baada ya Bunge kusitishwa, aliomba kupewa muda kwa sababu jambo hilo ni zito na walikuwa wakienda kwenye vikao.

Kwa upande wake, Dk. Hamidu Shungu wa UDSM aliwapongeza wajumbe kwa hatua hiyo akieleza kwamba wamefanikiwa kuzuia jambo hilo.

“Wajumbe walikuwa sahihi kwa kuwa Rais ni mkuu wa nchi anapohutubia mahali kama hapo, hiyo pia inatafsiriwa ndiyo uzinduzi, sasa Jaji Warioba kuwasilisha hiyo rasimu kabla Bunge halijazinduliwa inakuwa na maana tofauti,” alisema Dk. Shungu.

Alidai kwamba hatua hiyo ya wabunge imezuia mambo ambayo labda yalikusudiwa na ambayo pengine yangeegemea kwa kile anachokiamini au kukitaka Rais, hivyo kubadili mawazo ya wajumbe.

Sitta hakuwa tayari kuzungumzia utata uliojitokeza baada ya msaidizi wake kuomba waandishi wa habari kutokumhoji.
 
bila shaka wewe ni kula ulale hapa mjini umekosa kazi mpaka unaona hii nayo ni habari kwa GT, kama umemaliza chai kaoshe vyombo usijaze server.
Una akili wewe? unajua maana ya updates.Nani aliyekwambia mimi nipo mjin?
 
Rais kapunguziwa mamlaka ya uteuzi.

Pinda anabrowse JF

Bunge la muungano halitojadili mambo yasiyo na muungano.

Spika hatokuwa mbunge.

Wabunge hawatokuwa mawaziri.

Ukomo wa ubunge ni miaka 15.
Wananchi wanaweza kumtoa mbunge wao kabla ya uchaguz

Wajumbe wa Bunge la Katiba msichakachue hata point moja hapo ni maoni yetu Watanzania siyo ya Warionba.
 
Sasa jana walikataa nini na leo wanakubali nini!!
Kwa kawaida kanuni huwa zinatenguliwa kwa makubaliano na wajumbe. Yaani wajumbe hukubaliana kwanza kutengua kanuni ili jambo fulani lifanyike na sio mwenyekiti peke yake kutengua kanuni. Alichokifanya jana Sitta ulikuwa ni udikteta. Ilipaswa kabla ya kumwalika Warioba wajumbe wakubaliane kutengua kanuni ili Warioba aanze kabla ya rais. Na kwa kujua amelazimisha mambo ndio maana mwenyekiti alikuwa anakataa kuruhusu maombi ya miongozo kutoka kwa wajumbe. Hapo ndipo ndipo alipozima moto kwa petrol!
 
Haki za wanawake zinawekwa kwenye katiba?

Wanaume hatuna haki za kuwekwa kwenye katiba?

Haki za walemavu pia ndani ya katiba.

Mtu ana haki ya kumiliki mali na asinyang'anywe bila kupewa fidia stahiki.

Uraia ni mmoja tu,tena wa JMT
 
Wajumbe wa Bunge la Katiba msichakachue hata point moja hapo ni maoni yetu Watanzania siyo ya Warionba.

nawaza Ole Msendeka atafanya kaz gani baada ya Ubunge,na hapo kwenye komo wa ubunge,they have to bold,ila spika kutokua mwanachama inaweza isiwe na tija,si mmeona wajumbe walopitia asasi like KINGUNGE
 
Tbc fm na tbc tv wanarusha live.

Hapana sio tbc fm, ni tbc taifa ingawa inapatikana kwenye masafa ya fm. Pia kwa walioko mikoani hii tbc kuna baadhi ya mikoa huwezi kuipata kwenye masafa ya fm, hivyo itakubidi uitafute kwenye masafa ya AM.
 
Back
Top Bottom