Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

huyu mzee ana msimamo wa wanachokitaka wananchi haendeshwi na chama wala nini tungekuwa na watu thelathin kama yeye tungekuwa mbali
 
Serikali tatu uraia mmoja ndiyo nini hii au ndiyo kujenga hoja unakokuita wewe.

Mimi si muumini wa serikali tatu wala serikali mbili, kwangu napenda zaidi kuona serikali moja tu hata kama muungano utavunjika. Lakini ukitazama hoja zilizowasilishwa na warioba kuback up hoja ya serikali tatu naona wazi kuwa kuna kazi kubwa sana kuubadilisha mtazamo huo kwa hoja kwani Warioba ametoa hoja za msingi sana kutetea pendekezo hilo.
 
Nina mashaka juu ya gharama za serikali ya muungano. Hawa wazanzibari sijui kama watachangia. Pia sijajua kama gharama hizo zitakuwa sawa kwa sawa baina ya pande mbili hizi

Muungano ufe tu....
 
Serikali tatu uraia mmoja ndiyo nini hii au ndiyo kujenga hoja unakokuita wewe.

Ndio maana mnaambiwa uwezo wenu wa kuelewa ni mdogo. Kafafanua kuwa serikali ni tatu nchi ni moja. Hizi serikali mbili ni mamlaka ya pande za Muungano. Kwani sasa hivi serikali si ni mbili mbona uraia ni mmoja? Kaeni kimya Warioba awape vidonge vyenu. Naona viongozi wote walioko Bungeni wameny'wea kwa ukweli wanaopewa.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Tanzania%201962%20Kilimanjaro%20stamp%20Tanganyika.jpg

Hii kumbe ilikuwepo sasa imefutikia wapi?
 
Leo kila mjumbe wa bunge maalum la muungano alionekana aidha kuisapoti au kubaki kimya pale hotuba iliposomwa hadi Warioba aliposema uraia uwe mmoja. Hapo wabunge wa serikali mbili wakaanza kuzomea bila shaka ikiwashangaza wengi wao- ule mfumo unaopendekezwa itawezekanaje kuwa na muungano wa nchi washirika huku uraia ukiwa mmoja ndipo kizungumkuti kinapoanzia.
 
Serikali tatu uraia mmoja ndiyo nini hii au ndiyo kujenga hoja unakokuita wewe.

Marekani wana serikal 53 na uraia mmoja
Uingereza wana serikali zaidi ya tatu na uraia mmoja
urusi wana serikali nyingi na uraia mmoja.\

Wewe unaishi ulimwengu tulio wote au ulimwengu wako ni CCM tu?
 
Kwakweli Sidhani Kama Serikali Tatu Zitatatua Kero Za Muungano...Otherwise Kaongea Vizuri .....
 
Ndugu wana jamvi kila uchwao mmeona jinsi hawa wabunge tulivyowatuma kutuletea katiba mpya jinsi wanavyokula kodi yetu kwa makusudi tena bila aibu mradi kila siku wanaingiza laki tatu mfukoni huku siku bado zinaenda, uteuzi wa mh samweli sita kila mtu aliweke tofauti zake pembeni na kumchagua sitta kwa imani kuwa ataliweka bunge katika mustakabali unaokubalika na woote lakini kinachotokea sasa kwa kuzivunja kanuni na kufuata maelekezo ya chama sichelei kusema ndugu wilbrod silaa aliona mbali kwa kutokuwa na imani na mhe sita yetu macho ngoja tuangalie hii series inavyoendelea.
 
Wadau, kuna mtu anajua link ya kupata matangazo ya TBC online, kama ipo, kwasababu nimeitafuta mda sasa,
 
Rai wa nchi nyingine aruhusiwe kwenda kupiga kura na kugombea uongozi popote hii nayo imekaaje kisheria.

Uko Bungeni lakini haujamuelewa,ungekuwa nje kama sisi wasikilizaji ingekuwaje?Serikali ya muungano maana yake nchi ni moja with Serikali mbili zinazojitegema ,na sababu wote tupo ndani ya muungano basi wote tu raia wa ule muungano wa serikali hizo mbili.

Sijaona ubaya wa Mtu kutoka bara ameenda Zanziba asipige kura ati sababu ni raia wa Tanzania Bara,je hana haki ya kuchagua kiongozi amtakaye maeneo anayoishi?Msitugawe wanasiasa.
 
Hivi kwa masaa mawili ambayo Sitta alitaka ndo atumie Jaji Warioba je yangetosha kuwasilisha yale yote aliyosasilisha? au kuna kitu Sitta alitaka kisiongelewe kwa ufasaha?
 
Back
Top Bottom