Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Hotuba ya Warioba Bungeni Dodoma: Jumanne, Tarehe 18 Machi 2014 na Hoja ya Muungano wa Serikali Tatu

Ujumbe wake ni kuwa jadilianeni na mfikie muhafaka kwani swala la kura kuna lile kundi ambalo watafeel wameshinda na wale watafeel wameshindwa.. jambo ambalo sio zuri katika kuandika katiba...

Umenena mkuu
 
sendeka na wassira wasiojua kutafsiri data...sasa wapande ktk TV wakaseme tena kuwa hawajui warrioba na tume walifikia vipi maamuzi .Pengine TBC waandae haraka mdahalo leo
 
Kila kitu kinapangwa na kuwekwa kutegemeana na hali iliyopo. Ninyi wote nitawasifu kama mutaleta hoja inayoeleweka. Hamtaki Serikali 3, munasema haiwezekani kwa nini? Kenya kuna serikali za majimbo, munajuwa kuna majimbo mangapi na serikali ngapi? Amerika kuna serikali za majimbo mangapi? Nahisi tatizo lenu ni neno serikali au neno Rais. Munakuwa kama Idd Amini aliyezuiya mtu yeyote kujiita Rais hata kama ni wa chama cha waalimu.

Semeni hizo mbili ziweje? Mbona hamusemi moja? Semeni moja maana kama nchi moja serikali 3 ni tatizo kwenu, hata nchi moja serikali mbili ni tatizo! Tuondoe ujinga tusiwe watu tunaoweza kukumbuka tuliyoyasikia tu bila hata nafasi ya kujiuliza ya kwetu. Wengine mumekimbilia suala la gharama, huyu ambaye ni waziri mkuu mstaafu amewaonyesha jinsi serikali mbili zinavyoendeshwa kwa gharama kubwa kuliko hata hizo 3.

Waziri mkuu Pinda ni waziri mkuu wa serikali ipi? Z'bar wanamtambuwa? Serikali yake ni ipi?

Kuna kundi la Wa Zenj ambao wao wanapenda wawe na serikali lakini hawataki kuiendesha wenyewe. Wanataka serikali yao iendeshwe na bara, hiyo NO! kwa kuwa wana katiba yao, bendera yao, serikali yao lazima waiendeshe, kama hawawezi, wakope bara na walipe mikopo! Mambo ya kudeka hatutaki kabisa! Ukideka unaachiwa utembee mwenyewe, kama ni kilio, we lia baadaye ukinyamaza utakuwa na akili.

Bara wote hatuwezi kuwa kama akina Nape. Huyo Sitta naye analazimisha watu kufundishwa mambo ya muunganao eti na wale wanaoujua muungano. Akina nani hao walioujua muungano kwa miaka 50 bila kuwaeleza wengine, halafu leo ndo wanakuja kujidai kuwaeleza wengine.

Shit and stupid!
Mkuu umewahi kuona wapi mtu anatoka nchi nyingine na kwenda kupiga kura nchi nyingine au kugombea uongozi nchi nyingine.
 
Hili limekwisha sasa tunakwenda hatua nyingine tutafika tu hata iweje.
 
Warioba kamaliza sisi tutajua namna ya kufanya kile ambacho watanzania wanataka wala hatujali chochote ila ni matakwa ya watanzania basi.
Watanzania wapi tena...bado upo underground unakimbizana na thread za wana CDM?sisi tunamsikiliza warioba.
 
Sote tunajua kuwa ratiba ya Bunge Maalumu imempangia Rais JMT alizindue bunge hilo siku ya Ijumaa lakini bila kumung'unya maneno kutokana hotiba ya Jaji Warioba kuwa yeye ndiye amelizidua bunge.
NAWASILISHA

Hoja imepokelewa, umebaki utekelezaji
 
Ila JK akiwa na akili asijaribu kumchafua Judge Warioba,maana wengi wetu hatutamuelewa.
 
Uko sahihi kabisa. Hiyo ijumaa tunasubiri kusikia mipasho na kejeli dhidi ya Tume ya marekebisho ya katiba na hasa kwa Jaji Warioba na yale mamisukule ya ... Yatashangilia kwa vifijo.
Warioba leo ameonyesha umahiri wake na kuwa hayumbishwi na vijembe alivyokuwa anapewa na wanaopinga maoni ya Tume yake. Ameonyesha weledi na usomi wake katika uchambuzi wa kisheria na kitaalamu wala sio kisiasa.
HAWA JAMAA WA KIJANI SIJUI KWA NINI HAWAKUMSIMAMISHA HUYU 2005 ANASIFA ZOTE ZA UONGOZI SIO MAJUNGU.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Baba warioba nimekuaminia na bado naona una nguvu sana miguu iko fiti pambana naiona tanganyika yetu inarudi pia umesema vyema waasisi walituachia nchi moja serikali mbili na siyo serikali mbili na nchi mbili.
 
Sote tunajua kuwa ratiba ya Bunge Maalumu imempangia Rais JMT alizindue bunge hilo siku ya Ijumaa lakini bila kumung'unya maneno kutokana hotiba ya Jaji Warioba kuwa yeye ndiye amelizidua bunge.
NAWASILISHA
Mawazo yko ndio ujinga wako.
Div 5 mko wengi
 
vibaraka wa ccm walikuwa wamenuna sana.
warioba hongera.
ukweli umewapa kwa hiyo waukatae tena kama miaka ya nyuma walvyofanya
 
Mkuu, nimefanikiwa kupata nakala ya Kanuni za Rasimu zikiwa kwenye hard Copy. Nafuatilia kupata softy copy. Kuhusu hotuba ya Warioba, ilikuwa ni kwamba niliisaka tangu jana lakini imekuwa adimu. Nadhani kwa vile ilikuwa haijawasilishwa. Hata wabunge hawana nakala za hotuba hii. Ila tunawasiliana na wadau wengine tuweze kuiweka humu

Aliogopa msije mkaichakachua.
 
Warioba kamaliza sisi tutajua namna ya kufanya kile ambacho watanzania wanataka wala hatujali chochote ila ni matakwa ya watanzania basi.
Watanzania wameshasema kupitia maoni
Waliomwakilishia warioba .wewe unaenda kwa
Wananchi wepi au ni wale walanchi wa ikulu?
 
Mawazo yko ndio ujinga wako.
Div 5 mko wengi

Kwa taarifa yako nilisoma enzi ambazo shule za serikali ndizo zilikuwa zinatoa elimu bora zaidi. Ukweli unabaki pia wazi kuwa wewe ndiye unaonyesha usivyotaka kuona zaidi ya pua yako.
 
Baada ya wasilisho la Mzee Warioba leo bungeni, Nimejua ni namna gani nchi hii imebarikiwa kwa kuwa na wasomi wachache wenye uzalendo na wanao jua kusimamia ukweli wa wanayo yaamini, Kwa hoja makini zenye maswali na majibu aliyotoa mzee huyu, nashindwa kuelewa JK anaenda kuongea nini kinyume na hoja makini zenye uchambuzi mujarabu kiasi kile.

Shikamoo Mzee Warioba, Nimejifunza kitu kipya kwako leo.
 
Back
Top Bottom