Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
kuna mambo ambayo ccm inafanya hata shetani ANASHANGAA !
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wadau, naamini mmeamka salama na akili zimetulia baada ya yale yaliyotokea jana.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum ambayo ameyatoa jana usiku, ni kwamba Bunge litaendelea na kikao chake leo saa tatu kamili asubuhi. Kwamba, baada ya dua, wabunge ambao walikuwa hawajaapa watakula kiapo. Baada ya kiapo hicho ndipo Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Sinde Warioba atakapowasilisha Rasimu ya Katiba. Na kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ni kwamba Warioba ataongea hadi atakapomaliza hotuba yake.
Nami kama kawaida kwa kushirikiana na wadau wenzangu akinina Skype, MaishaPesa, Simiyu Yetu, Deo Corleone, kbm, Mkuu ya Kaya na wengine tutaendelea kuwaletea yatakayojiri. Hadi wakati huo, Stay Connceted.
-================================================================
UPDATES
Mwenyekiti anaeleza kilichotokea jana. Kwamba baada ya kutokea kile kilichotokea, ni kwamba waliitisha kamati ya mashauriano. Katika kikao hicho wamekubaliana mambo yafuatayo.
*Kwamba baada ya kiapo watampokea Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
*kwamba Warioba atahutubia kuanzia saa tatu na nusu hadi atakapomaliza
*semina zilizokuwa na utata zimefutwa badala yake semina ya kanuni itafanyika leo jioni na kesho
*Siku ya Alhamisi kutakuwa na semina itakayoongozwa na Wakenya.
*Semina juu ya historia ya Tanzania Bara, Zanzibar na Muungano imefutwa kwa vile kwa kadri utakavyoteua watakaoendesha semina hiyo, hawataonekana kama wamesimama kati kati
*Siku ya Ijumaa asubuhi, Mwenyekiti atatangaza Kamati 12 za Bunge Maalum
*Siku ya Ijumaa saa 10 jioni, Rais atakuja kulizindua Bunge
==================================================================
UPDATES
Jaji Joseph Sinde warioba ameanza kuhutubia bunge mnamo saa tatu na nusu. Katika hotuba yake amepitia sehemu zote za Rasimu ya Katiba. Masuala muhimu aliyoeleza ni kama ifuatavyo
Baada ya hayo na mengine, akiwa amewasilisha hotuba yake kwa dakika 85, Jaji Warioba alipumzika kwa dakika tatu. Na baada ya hapo anazungumzia muundo wa Muungano. Kwamba muundo uliopendekezwa ni wa Serikali tatu. Warioba anasema kuwa wamefanya utafiti juu ya muungano wetu na utafiti huo umeibua malalamiko kadhaa kwa pande zote za muungano. Ni kutokana na malalamiko hayo ndipo walipofikia uamuzi wa kupendekeza muundo wa serikali tatu.
- Mihimili ya dola itaendelea kuwa serikali, mahakama na Bunge
- kuhusu Serikali, Rasimu inapendekeza kuwa matokeo ya Rais yanaweza kupingwa mahakamani na mgombea urais na si mwingine.
- madaraka ya Rais yamepunguzwa hasa kwenye suala la uteuzi
- Mawaziri hawatatokana na wabunge
- Rais hatakuwa sehemu ya Bunge
- Kuhusu Bunge, ukomo wa wabunge ni awamu tatu ya miaka 5
- Spika na naibu Spika hatatokana na Wabunge
- Warioba pia kazungumza juu ya Uraia na amesema kuwa uraia ni wa aina mbili nao ni wa kuzaliwa na wa kujiandikisha. Pia imeelezwa kuwa hakuna uraia wa nchi mbili
======== Updates ==========
Baadhi ya Malalamiko ya Zanzibar;
4.Kutokuwa na Uwazi wa Mapato na Matumizi wa Fedha za Jamhuri ya Muungano,
5. Kutokuwa na Akaunti ya Pamoja.
6. Uwepo wa Mkanganyiko wa Mapato jinsi ya kuchangia gharama uendeshaji wa Serikali zote mbili.
7. Kuwepo kwa Tume mbili zinazoshindana katika Nchi moja.
8. Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu na Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mchakato wa kupata misaada kutoka kwa Nchi za nje.
9. Malalamiko kuwa Viongozi Wakuu wa Zanzibar wanachaguliwa Dodoma na sio Zanzibar
10. Zanzibar kulalamika kuwa kuna baadi ya mambo yamefanywa kuwa ya Muungano kupitia kutungwa kwa Sheria ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na baada ya hapo mambo hayo huwa katika utatanishi.
Kwa Upande wa Tanzania Bara baadhi ya malalamiko ilikuwa kama ifuatavyo;
1. Zanzibar imekuwa nchi huru, inabendera yake, inawimbo wa Taifa,Serikali yake na imebadili Katiba yake kutambuliwa kama Nchi.
2. Zanzibar imebadili masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo inasema Sheria za Muungano zinazotungwa na Bunge hilo,zitumike sehemu zote, badala yake Katiba ya Zanzibar inaelekeza kuwa ili Sheria
itumike Zanzibar Sharti ipelekwe kwenye Baraza la Muungano.
3. Zanzibar imetunga Sheria kuhusu Fedha, ambalo ni suala lililopo kwenye Katiba ya Muungano.
4. Zanzibar imetunga Katiba ambayo imechukua Madaraka ya Rais yaliyopo kwenye Jamhuri ya Muungano,inaeleza kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano anamadaraka ya kugawa Nchi katika maeneo ya Kiutawala, mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 yametambua kuwa Zanzibar ni Nchi na yamempatia Rais wa Zanzibar mamlaka ya Kuigawa Nchi katika meneo ya Muungano.
5. Katiba ya Zanzibar inaeleza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi mbili lakini Katiba ya Jamhuri inaeleza kuwa Tanzania ni Nchi moja.
6. Masharti ya Katiba yaliyowekwa kwenye Katiba ya Zanzibar kuhusu Mchango wa Zanzibar katika mambo ya Muungano yamepingana na masharti ya Muungano.
7. Muundo wa Muungano uliopo umepoteza kutambulisho Kihistoria Tanganyika kuhusu watu wa Tanganyika kupitia maslahi yao.
8. Wananchi wa Tanzania Bara, kutokuwa na haki ya kumiliki Ardhi,wakati wenzano wa upande wa Zanzibar wanahaki ya kumiliki Ardhi Tanzania Bara.
9. Wabunge wa Zanzibar huchangia mijadala ya Muungano na ambayo kwa uhakika wake ni mambo ya Tanganyika na kwamba Wabunge wa Tanganyika hawana nafasi ya kuchangia katika Baraza la Wawakilishi.
10. Kwa mujibu wa Sheria ya Mzanzibari ya mwaka 1985 Watanzania ambao ni Watanzania wa Bara kutakiwa kutimiza masharti Maalum ili kupata haki ya kiraia wakati Mzanzibari hutakiwi kupata haki hiyo bila masharti
yeyote,haki hiyo ni pamoja na kugombea Uongozi.
Tume iliamua kufanya uchambuzi wa kina kuhusu malalamiko haya na endapo malalamiko ya Zanzibar yakipatiwa ufumbuzi na ya bara yatakuwa yamepatiwa Ufumbuzi.
JAJI WARIOBA AKIWA NJE YA UKUMBI WA BUNGE
Vijana wenzangu tuwe macho sana na hawa wazee, hili swala la katiba tusiingie kichwakichwa matokeo ya serikali mbili au tatu yatalifaidisha kundi mojawapo ndani ya ccm na sio wewe wala ndugu yako, CCM imegawanyika mara mbili kuna wa serikali 2 na tatu kwa maslahi bnafsi ila wote ni marafiki na hawako tayari kuharibu chama wako pamoja, wanapambana kwa hoja jioni wanakula bata huku wakipeana tano. Cha msingi tuconcetrate na na maswala muhimu kwenye katiba yetu kama afya, miundombinu, elimu na malazi. katiba inasema nini juu ya haya, hata wao wakiamua nchi iongozwe na jaji mkuu au spika au jeshi hayo ni yao wanasiasa. Usifikiri Warioba,JK,Sitta,Lowassa +wana ccm kwa ujumla lao sio 1. chondechonde tuache mihemko kama wakenya sasa wanaandamana kila kukicha na watawala ni walewale wanabadilishana nyadhifa tu.:flypig:
karibu tujadili na kuelimishana kama vijana maana sisi ndo bado tuna safari ndefu kwa mstakabari wa nchi yetu.
Huwezi amini CCM ni aibu zaidi ya tunavyodhani.Eti kwa miaka 50 hawakuwahi kuwa functional zenj..kwani rais na waziri mkuu wa muungano hajawahi kuwa na uwezo wa ku operate zenj..yet.Kwa miaka 50 ya uhuru wa nchi yetu CCM ilishindwa zaidi..ilishindwa ongoza na kuleta maendeleo Tanganyika. Abu kubwa sana...CCM ni mbovu kuliko tulivyodhani.Wameishia kuwa wezi n wafujaji wasicholima. cc:Ritz
Huwezi amini CCM ni aibu zaidi ya tunavyodhani.Eti kwa miaka 50 hawakuwahi kuwa functional zenj..kwani rais na waziri mkuu wa muungano hajawahi kuwa na uwezo wa ku operate zenj..yet.Kwa miaka 50 ya uhuru wa nchi yetu CCM ilishindwa zaidi..ilishindwa ongoza na kuleta maendeleo Tanganyika. Abu kubwa sana...CCM ni mbovu kuliko tulivyodhani.Wameishia kuwa wezi n wafujaji wasicholima. cc: Ritz
Mwenyezi Mungu azidi kumsimamia na kumlinda katika yote kwa kuendelea kwake kusimama na kunena ukweli.
Ni kushinikiza mbona imeweza kushinikiza maswala makubwa tu ikiwepo la katiba japo mchakato unazegwe....cdm waliangalie hili swala kwa jicho la tatu..hata ukubalike na kuwa na hamasa kiasi gani bila kuwa na wapiga kura waliojiandikisha ni kazi bure na chama kinapimwa kwa kushinda chaguzi sio hamasa nk..Dr. unafikiri Chadema ifanye nini? Maana wenye wajibu wa kufanya hivyo ni selikali chini ya tume ya uchaguzi.
Chabruma, jioni hakuna bunge?Mwenyekiti anaeleza kilichotokea jana. Kwamba baada ya kutokea kile kilichotokea, ni kwamba waliitisha kamati ya mashauriano. Katika kikao hicho wamekubaliana mambo yafuatayo.
- Kwamba baada ya kiapo watampokea Mwenyekiti na Makamu mwenyekiti
- kwamba Warioba atahutubia kuanzia saa tatu na nusu hadi atakapomaliza
- semina zilizokuwa na utata zimefutwa badala yake semina ya kanuni itafanyika leo jioni na kesho
- Siku ya Alhamisi kutakuwa na semina itakayoongozwa na Wakenya.
- Semina juu ya historia ya Tanzania Bara, Zanzibar na Muungano imefutwa kwa vile kwa kadri utakavyoteua watakaoendesha semina hiyo, hawataonekana kama wamesimama kati kati
- Siku ya Ijumaa asubuhi, Mwenyekiti atatangaza Kamati 12 za Bunge Maalum
- Siku ya Ijumaa asubuhi, Rais atakuja kulizindua Bunge
Wasiwasi wangu zaidi,ukapatikana hapa,ktk hotuba hiyohiyo,ukurasa wa 12,,,"Zanzibar,wananchi karibu wote waliotoa maoni walijikita kwny suala la Muungano",,"Kati ya wananchi karibu 38,000 waliotoa maoni,Wananchi 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wa Muungano"
SASA ZANZIBAR,KWA MUJIBU WA SENSA YA 2012 INA WATU WAPATAO 1,303,569..WATU 38000 WALIOTOA MAONI,NI SAWA NA ASILIMIA 2.9 YA WAZANZIBARI WOTE,NA HAO 19000 WALIOZINGUMZIA MUUNDO,NI ASILIMIA 1.45 YA WAZANZIBARI WOTE....Je,HIYO INAYOSEMWA KWAMBA PALIKUWA NA MJADALA MKALI,,ULIKUWA UKALI WA ASILIMIA 2.9 YA WAZANZIBARI WOTE AU HII 1.45 YA WAZANZIBARI WOTE???. . .KWANGU MIMI,HAPA NDIPO NINAPOTILIA SHAKA UPACHIKWAJI WA NAMBA HIZI,KWA MALENGO YA KUIPATA SERIKALI YA TATU..NA NDIPO HAPAHAPA,NAJIKUTA,NAUNGANA NA CCM,JAPO WENYEWE WANAWEZA WASIWE WAMESIMAMIA KTK HOJA SANJARI NA HIZI ZAKWANGU,,,NA NI KATIKA HILI,NDIPO BINAFSI,NINAAMINI KUNA JAMBO NYUMA YA SHILINGI,AMBALO EITHER TUME,AMA WARIOBA PERSONALLY,ANALO,DHIDI YA MUUNGANO HUU
Kalenga ndio ilikuwa dis functional zenj, na miaka 50..hata bara kwenyewe kuna sehemu nyingi CCM haikuwa functional na hizo sehemu zimekuwa na maendeleo kuliko ilipokuwa CCM.yaani umeandika hayo yoote kisa kalenga, mbona siku zote ulikuwa ujasema?? cdm wametumia sh. ngapi kumlipa Mboye kwa kuwakodishia chopa Kalenga?? ni sawa kwa mwenyeti wa chama kujipa tenda ya kukodishia chama chopa???