Hotuba yangu jimboni Kigoma


What about DOWANS?
 

Mh. Zitto,

Naomba nisiongelee kuhusu hao wabunge wa CCM Kigoma na hayo madai yako dhidi yao. Ningependa kuongelea kuhusu mambo kadhaa:

Mosi, nina tatizo na hayo mazungumzo, kama nilivyoonesha concern hapo awali.

Pili, suala la kufumua bajeti seems very unprofessional to me, labda ungeweka wazi zaidi, maana umesema wewe ulikuwa kinara wa ufumuaji wa hiyo bajeti mpaka ukapata pesa ya barabara yako. Je huoni ulichofanya ni usaliti kwa wananchi wa maeneo mengine na kujifikiria wewe peke yako ubunge wako na wananchi wako pekee? Utaalamu wa kufumua bajeti umejifunzia wapi? Waamini ulichofanya ni sahihi?

Fingers crossed.
 

Kaka I salute you.

Hapo umenena. Nakukumbuka sana pale mlimani. Ulituongoza kwenye mgomo mpaka nikaonja virungu na mabomu ya machozi. Lakini at the end of the day tulipewa haki zetu na hata kufikia kuongezewa Boom.

I really respect you from loong time ago.

Nimefurahi tu ulivyo ainisha objectives zako na achievements kwa hizo objectives. Sijui ni wabunge wangapi wanaweza kutupa muhtasari wa yalioahidiwa na walicho fanya. Ni wachache sana. Wengi WAONGO WASANII watupu.

Bravo Bro.
 


Mkuu mimi sijui wewe ni mwenyeji wa wapi..lakini kama umekulia 'porini' kama wengi wetu ungemuelewa Mh. Zitto. Kwa mtu wa Kigoma hiyo barabara ina manufaa zaidi kuliko ya kwenda Tabora. Why? kwa sababu mtu wa Kigoma anafanya biashara na mtu wa Burundi na Congo..wengine wanazaliwa mpaka wanazeeka hajavuka mkoa wake wa Kigoma. Ingawa Burundi, Congo nk anakujua vyema kabisa. The same applies kwa mikoa mingine..kwa mfano mtu wa Ngara, Karagwe, Sirali nk..wanazijua nchi jirani kuliko watanzania wenzao. Na hii ni historical kwa sababu hiyo mikoa imesahaulika..viongozi wanaenda huko kuomba kura na kutoza ushuru tuu. .

Hivi unajua wakati mimi nakua..radio niliyokuwa naipata kwa uhakika ni KBC ya Kenya? ndo maana akina Mambo Mbotela mpaka leo nawakumbuka sana kuliko watangazaji wetu (majira ilikuwa inatufikia ila kwa taabu sana, mpaka uweke radio juu ya kichuguu). Sasa hapo unategemea nini?

Ukweli ni kwamba Tanzania haina vipaumbele..huwezi kudumisha 'umoja na mshikamano' kama watu hawana fursa sawa. Alichoongea Zitto si rahisi kumuelewa kama hujaishi hayo maisha in practical terms. Infact enzi hizo..ukienda Kigoma..hata bidhaa za Tanzania zilikuwa hazifiki...(hata siku hizi bia nadhani wanakunywa Primus ya Burundi zaidi kuliko bia za Tanzania..) kila kitu kilikuwa kinatoka Burundi na biashara ilikuwa inavuma sana. Muulize Zitto atakwambia... Kwa mtu kama huyo ukimuwekea barabara...mmemalizana..maana atafanya biashara zake...after all huko Tanzania iliko alishasahauliwa.

So in real world..barabara ya Mwandiga-Manyovu ina umuhimu mkubwa sana. Sasa hao wabunge wa mikoa ya kati ndo na wao wangehangaika wakapata barabara za kuwaunganisha na mikoa ya pembezoni kusudi wapiga kura wao wafanye biashara. Sijua RA mbunge wa Ndugu Sikonge anasikia huu ushauri wa bure?
 
kweli tumelogwa, anawezaje kuwasifia wakati ule ulikuwa ni wajibu wao, anawasifia kanakwamba walikuwa wanamfanyia yeye favour!!

Jamani Zitto anawakilisha Jimbo na ni lazima awe makini kwa kile anachosema. Kama asipochangua kile anachosema anaweza kuwaumiza watu wa jimbo lake. Kwa mfano 1995-2000, majimbo yaliochagua wapinzani hayakupa kitu chochote na matokeo yake wakati wa uchaguzi watu wakarudi CCM.
 
hatuwezi kuendelea kubembeleza mafisadi , walahela zetu kwa jasho letu...lazma tuseme HAPANA HADHARANI
 
hatuwezi kuendelea kubembeleza mafisadi , walahela zetu kwa jasho letu...lazma tuseme HAPANA HADHARANI

Ndio huwezi kubembeleza mafisadi lakini mkono mtupu aulambwi. Ni lazima utoe mchango wako. Zitto anatoa mchango wake kule na hata hapa JF anatumia jina lake. Wewe unayetaka mapambano hata jina lako unashindwa kulitumia hapa JF?
 
Ndio huwezi kubembeleza mafisadi lakini mkono mtupu aulambwi. Ni lazima utoe mchango wako. Zitto anatoa mchango wake kule na hata hapa JF anatumia jina lake. Wewe unayetaka mapambano hata jina lako unashindwa kulitumia hapa JF?
kwahiyo wewe jinalako ni zakumi?? kama ni kweli kwanini unalazimisha wengine tuwe na majina utakayo wewe
 



Haya ndio matatizo ya viongozi fulani kutaka kutaka kuonekana bila wao mambo fulani yasingefanyika.................na Mkuu Zitto akaingia katika huo mtego........

Wakati wa ujenzi wa barabara ya Jimboni mwako ulifika na hao watu wakatumia hiyo nafasi kuonyesha kama they played some role........NOOO ishukuru serikali yako kutambua kuwa barabara ilyoko jimboni mwakoni strategic......

Barabara ya Jimboni mwako Mh ni strategic....wala haikuwa na ubishi au uhitaji wa juhudi za watu uliowataja na kuwashukuru......it was a matter of time.........
 

UUUUUUUUWIIIIIIIII. Sometimes JF kuna wachangiaji... ngoja nisiendelee moods wasinifanyizie.
 
Nadhani tumelogwa.

Kwa mtazamo wangu hapo Zito alimshukuru Chenge kama Waziri wa Mmiundominu wakati huo pamoja na Zakia kama waziri wa fedha wakati huo kabla ya baraza lao kuvunjwa hakufanya vibaya ingaw ni wajimbu wa wizara hizo mbili kushirikiana ktk masuala ya maendeleo na Tanroads kumtaja Mrema sioni ubaya maana ndiye muhusika wa tanroads.

Ndugu yetu Zito hongera sana umefanya mengi mazuri na ya maendeleo kimsingi Kigoma ilikuwa gizani tangu tupate Uhuru lakini kwa kujakwake Zito kuufanya mkoa wa Kigoma kusikia na kuonekana. Narudia tene na tena hongera sana Zito kwa kuitoa Kigoma gizani jitahidi uweke na umeme wa kueleweka sio simu peke yake hao SISIEM waone haya.
 
UUUUUUUUWIIIIIIIII. Sometimes JF kuna wachangiaji... ngoja nisiendelee moods wasinifanyizie.

utachemsha ndugu yangu.......wengine hatubahatishi au kufuata mkumbo au ushabiki na tunayoyaandika.......watch out
 
UUUUUUUUWIIIIIIIII. Sometimes JF kuna wachangiaji... ngoja nisiendelee moods wasinifanyizie.


Shapu,

Huyu ndugu Ogah msamehe..namuamini waga ni mtu makini sana. Sijui hii hoja leo ameingalia kwa kutokea kipande ipi. Otherwise hoja zake ni makini.

Nadhani muungwana Ogah hajawahi fika Kigoma na hii mikoa iliyo pembezoni mwa nchi yetu ajue hali halisi.

Ogah umeshaambiwa... tangu uhuru almost nusu Karne..Kigoma haijawahi kuwa na barabara ya lami!!!!!..sasa sijui kama hiyo serikali unayoisema ilikuwa likizo ama vipi.
 
yet hakupaswa kuwashikuru kina zakia...walikuwa wanatimiza kilishowaweka humu maofisini mwao
 
Wabunge wa CCM wa mkoa wa Kigoma walienda delegation kwa Waziri kumshawishi kuwa barabara zinazopita jimboni kwangu zicheleweshwe mpaka baada ya uchaguzi.

Is this ''political'' game happening somewhere else in this world?
 

Kwa nini asishukuru wizara ya miundombinu na tanroads pekee???!! kuwashukuru watu ni kuonyesha ni kwa jinsi gani ukaribu wao ndio uliopelekea kupitishwa kwa maamuzi ya kujenga barabara.

Kwa nini amesema amefanya mazungumzo na THA na sio maboss wa THA? I dont get it.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…