Katika shuguhuli za Bunge lobbying ndio kazi haswa ya Mbunge. Mabunge yote duniani hufanya hivyo. Mnakumbuka miswada ya Obama kuhusu miundombinu jimboni kwake kutoka federal funds.......? All politics is local.
Nimewashukuru kina Chenge sio kwa sababu ninawapenda, bali kwa sababu walisaidia sana barabara hizi kujengwa Jimboni kwangu. Wabunge wa CCM wa mkoa wa Kigoma walienda delegation kwa Waziri kumshawishi kuwa barabara zinazopita jimboni kwangu zicheleweshwe mpaka baada ya uchaguzi. Chenge akaniita ni kunieleza na kuniambia amekataa. Pia kulikuwa ni 'deal'. Mtakumbuka mwaka 2007 Hazina ilitenga fedha kiasi kidogo sana kwa Wizara ya Miundombinu. Bajeti ile ilikuwa inalipa madeni tu ya wakandarasi na kusingekuwa na miradi mingine. Wakati huo mimi nilikuwa Mjumbe wa Kamati ya fedha na Uchumi ya Bunge na waziri kivuli wa Uchumi. Kamati ya Miundombinu ikamtuma Mbunge wa Sumbawanga mjini Mzee Kimiti kuja kamati ya fedha kutuomba tuzuie Bajeti yote mpaka Fedha za Barabara ziongezwe. Wabunge wakaniteua mimi kuandaa paper ya fedha zitapunguzwa wapi. Mimi niliongoza timu ndogo ya Wabunge kufumua Bajeti ile na tukaja na wazo la kupunguza bajeti ya 'matumizi mengineyo' kwa asilimia 15 na fedha zote kwenda katika barabara. Katika mazungumzo haya ndipo nilipofanikiwa kupata fedha za Barabara ya Mwandiga Manyovu (kutoka 800m mpaka 7bn mwaka ule, na imekuwa hivyo kwa miaka iliyofuatia). Ilikuwa ni mazungumzo binafsi ya Waziri wa Fedha (Zakhia Meghji) na Waziri wa miundombinu (Andrew Chenge) kwa msaada mkubwa wa Dkt. Bukuku yaliyopelekea kupatikana kwa mradi. Chenge alikataa ushawishi wa Wabunge wenzake wa CCM kuchelewesha lakini pia ndugu Mrema wa TANROADS alikataa ushawishi wa wabunge hao hao kuchelewa kutangaza tenda.
Nimewashukuru watu hawa kwa sababu mbili
1. Uungwana wa kushukuru (mnyonge mnyongeni, Haki yake mpeni)
2. Kutuma ujumbe kwa CCM na wabunge wake na Waziri Mkuu Pinda kuwa mradi ule haukushuka tu. Kuna kazi ilifanyika na wao hawajui. Ninaamini wamekwenda kumwuliza Chenge!
Mwisho, naomba nieleweke kuwa siasa zangu sio za Kinafiki. Ninasema ninachofikiri na ninachomaanisha. I am not choosing words to fit the political wave. Tumezoea wanasiasa wa aina hiyo. Mimi sipo hivyo! What you see in Zitto is what you get - Mkandara once said!
What about DOWANS?