BEN MKAPA. Andie rais fisadi kuliko wote kuwahi kutokea
nitakumbuka baadhi ya kashfa za ufisadi awamu yake.
Mzee Ben Mkapa kama angeliweza hata hata siku moja akapata ujasiri na kujitokeza mbele ya vyombo vya habari na kuzungumzia kashfa zako angetisha sana.Lakini Mzee Mkapa alijikausha kama vile jina la Ben William Mkapa siyo lake hadi siku anafariki.
Hakuwahi kutuomba radhi kwa ufisadi wake na serikali Kupitia TanPower Resources Limited, anahusishwa na dhamana ya serikali ya kupata mkopo Sh. 17.7bn kutoka CRDB kuendeleza mgodi wa mkaa mawe Kiwira.Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini iligundua 2015 kwamba, fedha za mkopo zilizodhaminiwa na serikali (Sh. 17.7 bilioni) hazikutumika ilivyokusudiwa.
Jenereta moja ya kuzalisha umeme ilichakaa hadi kutoweza kufanya kazi; na nyingine ilikuwa na uwezo wa kuzalisha megawati moja kutoka megawati sita.TanPower Resources LTD ilitakiwa kuzalisha MW200 za umeme awamu mbili. MW50 awamu ya kwanza kufikia Julai 2007 na MW150 ifikapo Machi, 2015.
Mzee Mkapa alibinafsisha mgodi wa makaa wa mawe wa Kiwira na kuumilikisha kwa watu waliokaribu na Rais. Nitawapitisha kidogo katika jambo hili.Nyaraka Mtendaji Mkuu Kiwira Coal and Power Limited (KCP), Francis Tabaro, alikabidhi bunge zinaonyesha ilikuwa inamilikiwa na Mkapa.
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ilikwenda mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira 16 Januari 2009 katika hatua ya kutaka kujua usahihi wa mmiliki wa mgodi huo.Bunge lilielezwa na Mtendaji Mkuu wa Kiwira Coal and Power Limited (KCP), Francis Tabaro, kuwa mgodi huo ulikuwa ukimilikiwa na watu walio karibu na Mkapa.Waliotajwa kwa mujibu wa taarifa hizo, ni mtoto wa kuzaa wa Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Nick (Nicholas) Mkapa na mkewe Foster Mkapa, Hawa wanamiliki kampuni ya Fosnik Enterprises, moja ya makampuni inayomiliki mgodi. Mkurugenzi mwingine ambaye ni mmiliki alitajwa kuwa ni D. Maembe.Kampuni hiyo nu kati ya kampuni nne zilizoungana na “kumilikishwa” mgodi wa Kiwira ambao ulikuwa mali ya serikali kwa 100%. KCP ilianzishwa Julai 2005.Ingawa, mzee Benjamin William Mkapa alikana kumiliki Kiwira wakati alipoongea na wakazi wa Lupaso, wilayani Masasi, mkoa wa Mtwara, mwaka 1999.Hata hivyo, 2003, serikali ilikiri bungeni kuwa mgodi wa Kiwira ulikuwa unamilikiwa na Mkapa; lakini ikasema, mipango iko mbioni kuurejesha mgodi serikalini
.Mkapa akiwa ikulu, alimpa mkewe, Anne, mamlaka ya kukusanya fedha na kuendesha, “Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote” (EOTF). Akajilimbikizia mali nyingi.Hadi wanaondoka ikulu, siyo Mpaka wala mkewe aliyesema fedha za kuendesha mfuko ya EOTF zilitoka wapi. Mafanikio na wala hesabu za mfuko ni siri yaoMuda wote Mkapa akiwa ikulu, “Mfuko wa Mama Mkapa,” huu ulikuwa unaendeshea shughuli zake katika majengo ya Ikulu. Ulianzishwa Novemba 1995.Gharama za bili ya maji, umeme, simu na mishahara ya wafanyakazi vililipwa na serikali. kuna mengi ya kushangaza yamefanyika chini ya utawala wako.Misaada na michango iliyotolewa na wafadhili, mingi ilitolewa kwa kuwa mwenyekiti wake ni mke wa Rais. Mfuko uligeuka, ingawa siyo rasmi, kuwa wa umma.Ulingiza nchi katika mikataba ya kinyonyaji katika uchimbaji madini, ukiwamo mgodi wa Tulawaka, Bulyanhulu, North Mara na Geita Gold Mine.Uijiuzia mgodi wa makaa ya mawe, Kiwira, mbeya kwa Sh700 milioni kwa kushirikiana na Waziri wako wa Nishati na Madini wakati huo, Daniel Yona.
Baadae mliukodisha mgodi wa makaa ya mawe, Kiwira, mbeya kwa makaburu kutoka Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka 100. Ajabu kabisa.Mgodi wa makaa ya mawe Kiwira ulijengwa na Serikali ya China kwa kwa US$4 bilioni na kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania mwaka 1988 na Baadaye mgodi wa makaa ya mawe Kiwira (Kiwira Coal Mine) uliuzwa kwa Mkapa na Yona kwa Tsh. 700 milioni. Hadi Mei 2008 walilipa Tsh. 70 milioniWamiliki wa mgodi huo walikuwa Kampuni ya ANBEN Limited ambayo wamiliki wake ni Mkapa na mkewe Anna, Kampuni ya DEVCONSULT LimitedHii ni kampuni ambayo ilikuwa ni mali ya Bw. Daniel Yona mwenye hisa ya asilimia 90 na mtoto wake Danny Yona mwenye hisa asilimia 10.Wanahisa wengine ni Universal Technologies Limited mmiliki wake ni Evans Mapundi na Wilfred Malekia, na Choice Industries Limited mali ya Joseph Mbuna.Wamiliki wengine walikuwa ni Kampuni ya Fosnik Entreprise Limited ya Bw. Nicholas Mkapa na Bi. Foster Mkapa ambao wana hisa ya 50% kila moja.Mzee Mkapa tunakumbuka pamoja na mkewe, walianzisha kampuni ya biashara – ANBEM Co. Limited – kwa kutumia rasimali za umma.
Mkapa alimiliki kampuni ukiwa bado Rais (ANBEN Limited) wa nchi na hivyo alitumia nafasi yake kujinufaisha binafsi na kampuni yake.Kwa kuwa alikuwa bado madarakani na uamuzi wa kuuza Kiwira ulifanyika ndani ya Baraza la Mawaziri aliloliongoza, uamuzi ulikuwa wa upendeleo.Mkapa aliuza nyumba za serikali. Akajimilikisha baadhi ya nyumba hizo. Akaruhusu waziri wako, John Pombe Magufuli, naye kujimilikisha. Ndiyo.Kwa pamoja, wanashutumiwa kuziuza nyumba 8,288 za Serikali kwa mikakati mingi iliyogubikwa na rushwa na ufisadi wa kila aina. Inasikitisha.Akasimamia uuzaji unaofanana na utoaji bure mashirika ya umma, ikiwamo “utoaji bure” iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC). Benki mashuhuri.Benki iliyokuwa na matawi nchi mzima na mtaji kedekede, iliuzwa kwa bei ya kutupwa kwa benki ya ABSA ya Afrika Kusini. Ajabu kabisa.NBC iliyoelezwa inauzwa kwa wenye uwezo wa kuiendesha kuliko wazalendo, iko hoi kibiashara. Imepoteza mtaji; sasa inaendeshwa kwa hisani ya BoT.Aliuza shirika la ndege (ACT); migodi na mashamba. Mkataba wa kampuni yake kuuza umeme kwa Tanesco ulifungwa akiwa madarakani (Septemba 2005).Jambo linaloonyesha upendeleo kwa kampuni yake. Kampuni ya Benjamin William Mkapa ingelipwa ($3.65 milioni sawa na zaidi ya Tsh. 4 bilioni kila mwezi.)
mzee Mkapa ni wakati wake akiwa kiongozi mkuu wa umma na mkuu wa Serikali mashirika ya umma yalibinafsishwa, kama shamba lisilo na mwenyewe.Mzee Mkapa aliingiza kampuni ya kigeni kutoka Afrika Kusini – Net Group Solutions kuikabidhi shirika la umeme (TANESCO), kuvuna wasichopanda.Kazi ya Net Group ndani ya TANESCO, haikuwa kuzalisha; kuwekeza mtaji; kutafuta vyanzo vya umeme. Kazi ilikuwa kukusanya mapato na kukamua wananchi.Katika kipindi cha miaka saba ya mkataba kati ya serikali na Net Group, Tanesco ikashindwa kuzalisha umeme unaoendana na mahitaji. TANESCO ikashindwa kuwekeza katika miradi mipya ya umeme.Matokeo yake, miundo mbinu ya umeme ikachakaa. Taifa likatumbukia katika giza la milele. TANESCO iliyokuwa imara, haraka ikatumbukia katika mikataba ya kinyonyaji ya kuzalisha umeme wa dharula. Shirika la umma likawa Shirika la nyuma.TANESCO iliyokuwa inajiendesha kwa faida inayoridhisha, ikatumbukia katika madeni makubwa yanayohatarisha hata uhai wa shirika lenyewe.
Ni Serikali ya Ben Mkapa ilikwenda kumtafuta na kuingia mkataba wa kinyonyaji wa kuzalisha umeme wa RICHMOND na dada yake DOWANS.Makampuni mengine; Aggreko; Symbion; Songas na “ndoa ya mkeka” iliyofungwa kwa mara ya pili na kampuni ya Independent Powel Tanzania Limited (IPTL).Mkataba wa kwanza kati ya IPTL na serikali ulifungwa Septemba 1994, serikali ilijifunga kulipa IPTL Sh. 6 bilioni kwa mwezi kwa umeme usiokuwepo.Januari 2015, mkataba wa TANESCO na IPTL kupitia kampuni ya Pan African Power Solutions (PAP), ulifungwa katika mazingira yenye utata.Mzee Mkapa ni wakati wako uliamua kunyamazia kimyaa ukwapuzi wa mabilioni ya shilingi serikalini na ndani ya Benki Kuu ya taifa (BoT).Fedha za umma zilizochotwa (siyonkuibwa tu) kupitia akaunti ya madeni ya nje (EPA), katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2005.Mabilioni mengine ya shilingi yalikwapuliwa na makampuni ya Tangold Limited, Deep Green Finance Limited, Meremeta na Mwananchi Gold Ltd.Kampuni ya KAGODA Agriculture limited, ilipewa “zawadi” ya kiasi cha Sh. 70 bilioni kati ya Sh. 130 bilioni zilizochotwa Benki kuu ya Tanzania.Ushahidi wa Ben Mkapa kushiriki au kunyamazia wizi katika akaunti ya madeni ya nje ya EPA, uliwekwa wazi na Bhyidinka Michael Sanze, Bhyidinka Michael Sanze alikuwa wakili msomi kutoka katika kampuni ya mawakili ya Malegesi Law Chambers ya jijini Dar es Salaam.Bhyidinka Michael Sanze alishuhudia mkataba kati ya Kagoda na serikali. Na anakiri alishuhudia mikataba na makampuni mengine ya nje
.Ben Mkapa kitabu cha “MY LIFE, MY PURPOSE” anatueleza wahuni walitumia uaminifu wake kwa CCM kutumia pesa za umma kwa ajili ya CCM.Ben Mkapa anakiri kwamba, wahuni ndani ya Serikali walitumia uaminifu wake kumshawishi akubali kutumia Tsh. 230bn kutoka akaunti ya madeni ya nje (EPA).
Anasema watakaonunua hayo madeni walikuwa tayari kuchangia mfuko wa kampeni za uchaguzi wa CCM. Mzee Mkapa alistahili kuwepo gerezani.Kwa maneno yake Ben Mkapa anasema “Ninajisikia kuwa nilitumika na kusalitiwa. Ukweli ni kwamba mimi binafsi sikufaidika na sikupata chochote”Ni kwamba CCM walituibia pesa za EPA zaidi ya Shs. 230bn ili wazitumie kwenye kampeni za uchaguzi 2005. Na hakuna kitu tulifanya.
Utawala wa MKAPA.Aliruhusu polisi; vikosi vya (SMZ) vikosi vya (JKU); Kikosi cha (KMKM) – kuendesha mauaji makubwa Visiwani Pemba na Unguja, 26 na 27 Januari 2001.Katika tukio hilo lililoweka doa baya taifa hili, wanakaokadiriwa kati ya watu 30 na 75 waliuawa kwa kuteswa, na kupigwa risasi. Mbaya sanaNi afadhali jambo hili katika kitabu chake cha MY LIFE; MY PURPOSE, amekiri kwamba ni tukio linaloacha doa katika utawala wake wa kifashisti.Nyerere alifariki kabla Mkapa hajamaliza ngwe yake ya kwanza, Oktoba 2010. Vinginevyo, asingeruhusu Mkapa kushika madaraka kwa vipindi viwili mfululizo. Nyerere alifariki dunia 14 Oktoba 1999. Mwalimu alimpenda sana Mkapa na hata baada ya kushindwa kura za maoni alishawishi CCM waende naye.Kama Mkapa una kinga na mkeo na mwanao na washirika kwenye makampuni yenu nao wana kinga? Au ni yale yale ya ufalme wa mlango wa nyuma?Endelea kupumzika Mzee Big Ben. Sisi bado tupo, tunasukuma gurudumu. Pole kwa wote ambao nitakuwa nimewakwaza kwa kutoa historia ya marehemu.