Housegirl alipwe Mshahara wa elfu 80 hadi laki 3

Wanajichukulia points sana za kuwatetea hao mabinti wanahisi wanaonewa kila mahali, kuna wafanya kazi wa masuper markets wananyanyasika daily wamewafanyia nini?

Wanawatesa ndio, wakija kwenye media wanatetea ushenzi tu!
 
Sio kila mtu anaweza kuishi na mtu hivyo! Wengine hatujaumbw ahivyo! Lazima utampatia mahitaji tu! Kuna binti tulipata anaumwa sijui nini miguu na mikono ana mapele makubwakubwa meusi yamejaa, kuoeleka vipimo tu 170k utamuacha mtu anaumwa kwa sababu sio ndigu yako? Hapo bado dawa si chini ya 70k na clinics mara moja moja! Sio wote wanawez akuishi na mtu kwa kubagua eti atajijua mwenyewe huko!
 
Mkuu tunacho angalia ni uhalisia wa maisha ya mtanzania,na mishahara ya waajiriwa wengi..

Watumishi walio kwenye kundi kubwa hulipwa kati ya laki 5 mpaka 8..

Unataka kwa kipato hicho amlipe dada laki 3??

Kumbukeni kuna vibarua kwa wahindi wanalipa mpaka elf 3 kwa siku,,hyo buku 3 ni kila kitu nauli,matibabu na chakula ni ujibane hapo hapo..unatoboaje?
 
Huwa haitoshi kabisa, ndiomaana kuna maboss wanawalipa hizo laki ngapi ila cha moto wanakipata! Unafanya kazi na huli kazini! Kwanini usijishushe ukaishi kama upo nyumbani, fanya kazi kwa malengo toka na kamtaji kako! Kutaka makubwa wanadanganya sana mwisho wa siku mambo yanawaharibikia kisa tamaa!
 
Sahihi mkuu,nilicho jifunza mabinti wengi wana ongozwa na tamaa hivyo hupelekea kulaghaiwa haraka na watu..
 
Wanajichukulia points sana za kuwatetea hao mabinti wanahisi wanaonewa kila mahali, kuna wafanya kazi wa masuper markets wananyanyasika daily wamewafanyia nini?

Wanawatesa ndio, wakija kwenye media wanatetea ushenzi tu!
Nasikia huko kwa wahindi viwandani hulipwa mpaka buku 3 per day,,yaani ni kazi kuanzia asubuh mpaka jioni..hyo buku tatu ikave kila kitu msosi,nauli,kodi ya nyumba na uache mezani kwa wanao baki.
Na watu wanagombania hizo kazi.
 
Nasikia huko kwa wahindi viwandani hulipwa mpaka buku 3 per day,,yaani ni kazi kuanzia asubuh mpaka jioni..hyo buku tatu ikave kila kitu msosi,nauli,kodi ya nyumba na uache mezani kwa wanao baki.
Na watu wanagombania hizo kazi.
Sijui wanazigombania za nini! Ila wabongo kuna muda sijui tunakuwaje! Kuna kazi hivi nilienda kufanya kwa mtoto wa muhindi, nikakuta dadaake wa kazi kakaa na kale katoto, ndio nikamuuliza akasema yaani basi tu lakini wanasumbua mno na analipwa 150k sjui wanapenda kukaa kwenye yale maghorofa ya ukonga! Au wawasindikize supermarket! Nahisi wanapenda kuwa around hayo maisha tu mimi siwaelewagi!🙌🏾
 
we unalipwa laki 7 kwenye kibarua chako,utoe laki 3 then?...serikali ianze kuboresha maisha ya watumishi kwa kuwalipa vizuri,automatically na wao watawalipa wasaidizi vizuri.
Sijazingatia mshahara!
Kwa tunaoishi vizuri na dada ile aishi kama yupo kwao ukipiga gharama kwa mwezi anatumia zaidi ya 300k bado mshahara unampa.

Sasa si bora nimpe 300k ajitegemee kila kitu ndo hapo mwezi haujaisha yeye hela imeshaisha.
 
Pamoja na hayo ni mtu mwenye ndoto zake hayupo kwako kwaajili ya kula, ni mtu anayetafuta mafanikio sasa umlipe 3000 kwa siku atafanikiwa lini? Ingekuwa ni wewe au mtoto wako ungejisikiaje? Pamoja na mahitaji yote angalau 5000 kwa siku japo nayo ni kidogo sana. Kama hauna uwezo huo wa kumlipa ujue hujafikia hadhi ya kuwa na mfanya kazi fanya kazi zako mwenyewe
 
Kwamba hakuna watu wanaofanya kazi kwa kulipwa mishahara midogo isiyowapeleka popote au mmeona wasaidizi wa kazi za ndani tu? Mishahara inazidiana wapo wanaolipwa mpaka laki 8! Ukianza na 80k unamnyonya mwenye uhitaji na hana majukumu ya kumlipa mtu laki3! nina chumba kimoja na mtoto asiyeshinda nyumbani, nikakulipe sijui laki ya kuangalia tv au? kuna kazi gani mpaka nilipe pesa kujilinganisha na boss mwenye bungalow?
 
Hapo saaa ni makubaliano yenu ninyi wawili, umlipe 100k ila kila kitu ajitegemee cha kwako ale chakula tu ila matumizi binafsi kama hizo losheni, pedi, sijui kisuka afanye mwenyewe. Wewe unakuwa unafanya mara mojamoja ukipata nafasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…