Housegirl alipwe Mshahara wa elfu 80 hadi laki 3

Housegirl alipwe Mshahara wa elfu 80 hadi laki 3

Unajua kuna kazi mtu hata akilipwa kidogo kujiongeza ni rahisi sana. Mfano mtu anayeuza duka la dawa anaweza kujiongeza akawa anauzia dawa zake binafsi hapo hapo kwenye duka la boss wake. Wengine pia wanataka walipwe commission kulingana na mauzo(ni rahisi zaidi kudai nyongeza ya mshahara au commission dukani kwa sababu tofauti ya mauzo inaonekana). Pia kama ni duka kubwa sana lenye bidhaa mchanganyiko na mauzo makubwa mtu akichomoa hata elfu kumi kila siku boss hatakaa ajue wala hakuna shoti yoyote itaonekana.
Kumbe mwizi hiloooo...!
 
Nyie wamama corporate acheni ujanja wenu, kuolewa hata wadada wa Bar wanaolewa tu wakiwa wazuri. Mnamlipia mdada wa watu flight sio kwa sababu mnapenda sana bali kwa sababu mnamuamini zaidi na watoto wenu au msingependa abaki kwenye mjumba peke yake, pia ni kama asali kumbakiza loyal muda mrefu zaidi😁
mimi sina u-corperative wowote! naongelea watu wanaofanya hivi! sawa kila mtu na mtazamo wake, si unajua eeh!
 

Shirika la kutetea haki za Wafanyakazi wa majumbani la Wote Sawa chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Angela Benedicto, limesema Serikali imetoa tangazo ambalo utekelezaji wake umeshaanza ambalo linamtaka mwajiri aliyeajiri mfanyanyakazi wa nyumbani (house girl) na haishi kwako, umlipe mshahara wa kima cha chini Tsh.160,000 na kama anaishi kwako utamlipa mshahara wenye kima cha chini shilingi elfu 80.

Mfanyakazi wa ndani aliyeajiriwa na Maafisa wenye stahiki (Majaji, Wabunge, Mawaziri na Viongozi wengine wa juu wa Serikali atalipwa kima cha chini cha mshahara cha Tsh. 265,000 na walioajiriwa na Wanadiplomasia (wakiwemo Mabalozi) na Wafanyabiashara wakubwa watalipwa kima cha chini cha shilingi 328,000. ‎ ‎

Haya yamebainishwa na Jackline Ngalo, Mwanasheria wa Shirika la kutetea Wafanyakazi wa majumbani la Wote Sawa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wafanyakazi wa Majumbani yaliyofanyika jijini Mwanza yakiwa yameandaliwa na Wote Sawa, ambapo tangazo hilo linataka Mfanyakazi wa nyumbani apewe stahiki zake kama Wafanyakazi wengine wa ofisi mbalimbali ikiwemo likizo, mapumziko, kuwekewa fedha kwenye mifuko ya hifadhi za jamii, kupewa NIDA n.k. ‎

‎Angela amesema “Kwa zaidi ya miaka 10 sasa Shirika la Wote Sawa linashirikiana na Serikali na Wadau wengine katika kuimarisha ulinzi wa Watoto, Wanawake na makundi yaliyo katika mazingira hatarishi, katika kipindi hicho Wote Sawa imefikia Wafanyakazi wa majumbani elfu 10, Wananchi laki 3 katika kuwapa elimu na wamehudumia Manusura takribani 1500." ‎ ‎

Kwa upande wao Wafanyakazi wa majumbani kupitia Wawakilishi wao wamepaza sauti wakielezea changamoto mbalimbali zinazowakabili, huku Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela, Wakili Mariam Msengi, ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda kwenye maadhimisho hayo akatoa maagizo ya RC Mtanda ya kuwataka Maafisa wa NIDA Mkoa na Wakuu wa Wilaya wote wa Mwanza kuwasaidia Wafanyakazi wa majumbani kupata vitambulisho vya NIDA.
Hili suala ni mtambuka linapaswa kufanyiwa mchakato sana, sipingani na hoja ila modality ya utekelezaji ndo ikoje?.
Kuna baadhi ya familia dada wa kazi ni sehemu yao, analipwa labda 50K lakini anatibiwa, ananunuliwa mavazi, anapewa hela ya kusuka, anapewa hela ya vocha kwa kuwa simu yake inatumika kama ya nyumbani (ofisini kwake), anasaidiwa familia yake ikiwa na shida, akienda kwao anapewa nauli ya kwenda na kurudi na zawadi. Wengine wamesomeshwa ufundi, wameendelezwa kimasomo mpaka wengine wamewezeshwa mitaji wakajitegemea baada ya muda fulani.
Kwa hiyo lisiwe swala la uwana harakati tu.
 
Anajifurahisha huyu
Serikali yenyewe kima cha chini cha watumishi wake mia 3 sitini afu huyu anayelipwa 360 ndo amlipe mfanyakazi wa ndani 160 hiyo familia wanakula hewa?
 
Na ndivyo inavyotakiwa kuwa, utashangaa humu kuna waajiriwa ambao kutwa kuilalamikia serikali iwaongeze kima cha salary, wakati huo wao wanawalipa wafanyakazi wao wa ndani pesa ambayo kiuhalisia haitoshi hata kununua mifuko 5 ya simenti.

Hovyo kabisa, roho mbaya na ubinafsi wa watanzania ndio unaorudisha nyuma maendeleo ktk jamii, hivi kama unajiona huna pesa kwanini utoe ajira kwa mtu usiyemmudu mpaka mpigishane makelele?, na kuna watu hata kula yao shida lkn wanataka wawe na wafanyakazi ndani.

Kuna hawa ambao wanalipwa pesa nzuri kazini/ktk biashara zao lkn hawawalipi vizuri wafanyakazi wao, ndiomaana mnaibiwa waume wenu na wengine kutiliwa sumu/kuibiwa/kuchawiwa na kila aina ya matukio kisa ushenzi wenu wa kuwanyanyasa mabinti wa watu.

Kama mnaona rahisi kwanini msifanye wenyewe hizo kazi?, au kwanini msiwape ndugu zenu wazifanye?.

Kuna ulazima wa kudeal upya na sheria zitakazosaidia kuwalinda waajiriwa wote nchini bila ubaguzi.
 
Hili la wafanyakazi wa ndani wangeachana nalo, muhimu wahakikishe usalama wao upo vizuri. Waache wakubaliane wao na wanaowasaidia majukumu ya ndani
Ili muwanyonye mabinti wawatu?, hili ni jukumu la serikali kulinda maslahi ya kila raia, na kila mfanyakazi anatakiwa alipwe kiuhalali hailajishi uchumi wako uko vipi.

Kama unaona huna pesa za kuwalipa vzr mabinti wa kazi kwanini usizifanye mwenyewe?, au kwanini usiwape ndugu/watoto wako wazifanye bure, suala la ukoloni/utumwa tunalisema limekwisha lkn kiuhalisia bado linafanywa na watu wamehalalisha, kisa serikali haijatilia mkazo wa sheria zinazodhibiti ukiukwaji wa haki za kila mwananchi.

Acheni utapeli, lipeni vizuri mabinti, hizo 50k-100k mnazowapa hazitoshi hata kuanzia maisha wakirudi makwao, pesa ngumu sawa! Kwanini ukimbilie majukumu yaliyokuzidi?
 
Ili muwanyonye mabinti wawatu?, hili ni jukumu la serikali kulinda maslahi ya kila raia, na kila mfanyakazi anatakiwa alipwe kiuhalali hailajishi uchumi wako uko vipi.

Kama unaona huna pesa za kuwalipa vzr mabinti wa kazi kwanini usizifanye mwenyewe?, au kwanini usiwape ndugu/watoto wako wazifanye bure, suala la ukoloni/utumwa tunalisema limekwisha lkn kiuhalisia bado linafanywa na watu wamehalalisha, kisa serikali haijatilia mkazo wa sheria zinazodhibiti ukiukwaji wa haki za kila mwananchi.

Acheni utapeli, lipeni vizuri mabinti, hizo 50k-100k mnazowapa hazitoshi hata kuanzia maisha wakirudi makwao, pesa ngumu sawa! Kwanini ukimbilie majukumu yaliyokuzidi?
Ukikaa na kutulia utaelewa nilichosema, nyumba hazifanani, na wanaokaa na hawa mabinti hawafanani vipato. Wengine wanataka watu wa kubaki nyumbani, hakuna kazi ngumu zaidi ya kufagia nyumba na kuosha vyombo. Serikali haitaweza kulisimamia hili zaidi ya kuleta vurugu.
 
Huko liliko kusuduwa ombi la mahausi girl na sie waajiri wao tumepeleka maombi yetu ili tuongezwe mishahara watuvumilie kidogo
 
Hapo saaa ni makubaliano yenu ninyi wawili, umlipe 100k ila kila kitu ajitegemee cha kwako ale chakula tu ila matumizi binafsi kama hizo losheni, pedi, sijui kisuka afanye mwenyewe. Wewe unakuwa unafanya mara mojamoja ukipata nafasi
Atakuwa mwizi balaa, kwenye mafuta ya mtoto, na vijisent vya dukani vikibaki.
 
Back
Top Bottom