Asante kwa topic hii naona itanisaidia.
Ni mama wa watoto kadhaa. Nina work mate wangu (baba wa watoto kadhaa) ambaye tulikuwa tukiflirt kwa muda wa miaka 2, ila saa za kazi tu, kuanzia saa mbili hadi saa kumi jioni, na wakati mwingine usiku kama tupo safarini. Hatuendi lunch pamoja wala hatuna tabia ya kuwa pamoja. Mara nyingi tunakutana kwenye vikao. Mapenzi yetu ni kwa simu tu.
Majuzi kati hapa aliomba kuvunja amri ya sita. Moyo unataka ila mwili unakataa. Nimeamua kumwambia tusitishe mawasiliano, tunajaribu lakini inashindikana kwa vile tuko ofisi moja. Tukionana tu ndo unakuwa mwanzo wa kuanza kupigiana simu za mapenzi. Je kuna mapenzi kati yetu au ni tamaa za mwili? Nitajuaje au nimpe test gani kugundua kuwa ananipenda kweli.
Hapa nimejifunza kuwa hakuna mwanaume mwenye mke utakayekuwa naye kwenye uhusiano wa dhati. Atakutumia kumaliza tamaa zake za kimwili na stress za nyumbani kwake aka kipoozeo.
Asanteni sana.