Haya masuala ya rangi ni tata sana, yaani yanachanganya vichwa mno! Nimekereka sana na tangazo la hao Wahindi hapo juu. Tungetukuza utaifa na kusahau rangi zetu.
Moshe,
We jivunie tu kuwa Mtanzania bila shida yoyote, ni Mtanzania halisi na unastahili haki zote za kuitwa Mtanzania. Unastahili kuheshimiwa, kuthaminiwa utu wako, kumiliki mali, kupiga na kupigiwa kura na haki nyingine ambazo raia wa nchi anastahili! Tupilia mbali rangi yako na muonekano wako, tukuza Utanzania wako. Nimesikia na kusoma toka katika magazeti ya Udaku kwamba hata Richard aliyeshinda big brother eti si Mtanzania, kisa? Mababu zake ni wahamiaji toka kusini mwa Afrika! Nikashangaa sana. Mie mwenyewe nimekulia mahali ambako nilikuwa nikicheza na waarabu na Wazungu ambao wamezaliwa Tanzania na wanajisikia fahari kujiita Watanzania, ukiachilia mbali rangi zao! Rangi sio hoja sana.
Hapa nilipo ninaishi jirani na Wazungu wa Afrika Kusini (sipendi kuwaita makaburu), sijawasikia hata siku moja wakisema wao ni wazawa wa hapa na kujiona sawa na wazungu wa huku, wao wanajiita Waafrika! Inashangaza lakini ndio hali halisi.
Mfano mwingine, kuna Warabu ambao wanapatikana kule Usangu Mbeya, wale kiasili ni Wapakistani! Lakini wapo pale miaka na miaka wakijiita Watanzania na wengine hata Pakistani hawajawahi kufika na mwaka jana mmoja wao kachaguiwa kuwa Mwenyekiti wa sisiemu wa mkoa ule.
Kw hiyo ndugu Moshe jisikie fahari tu kuwa Mtanzania.