Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wewe ndio umetumia neno wazawa.. so wewe ulidefine! ili nijue unazungumzia nini. Mmetoka kwenye rangi, mnaenda kwenye kupachikwa... si mseme tu hakuzaliwa TAnzania tujue! na wazazi wake siyo raia!
Bubu, hujaniambia Richa amekosea nini? WEwe umeng'ang'ania wahindi hivi wahindi vile.. je we unaendaga kwenye misiba yao!? Unaendaga kwenye harusi zao? HIvi kuna mtu humu ambaye anarafiki wa kihindi na aliwaalika kwenye harusi au sherehe fulani na hawakutokea?
Tena mmenikumbusha, kulikuwa na mwalimu fulani Mwanza alikuwa anaitwa Mwalimu Mbiti, mweusi, (watu wa Mlimani, Bugando/Pamba primary wanaweza kumjua), yeye mbona alioa mhindi?
Na kama wewe MWANAKIJIJI unadhani wahindi wanapaswa kupewa nafasi za taifa pale tanzania, basi kuanzia leo ufunge mdomo wako na mikono yako kutoandika chochote sijui RA, sijui Manji sijui nani!
Nasikitika kwamba mijadala ambayo inahitaji uchambuzi wa kina tunaijadili kwa mitizamo ya ki layman mno.Mada hii imeanzia kwenye makala ya mwanakijiji, ukiisoma vizuri mbali ya kuwa alilenga kujadili suala la Ms tz, kajenga hoja kwa mifano mingi ambayo kimsingi ina rise maswali magumu kuliko majibu.Nina hakika hata yeye kuna mambo mle ukimstukiza hawezi kukujibu kwa haraka. We need to think beyond the horizon, suala la uyu dada halina ubishi ni mtanzania na ana haki zote za kutuwakilisha. Tunaweza lakini kwenda mbali ya hapo na kujadili mambo mapana zaidi kuhusu ili suala nje kabisa ya huyu dada. kwa kizungu naweza sema 'we take the topic in broad context and discuss it objectively'' si suala la ubaguzi kabisa hilo ila kujielimisha zaidi, mimi napenda kutumia msemo wa 'think big' Msinifanye niamini JF ni mahala pa 'kupiga soga tu'(quote from http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=66652#post66652) au kutafute easy answers to hard questions,we can do more than that wazee.
Juzi juzi tu tulikuwa na msiba wa dada yetu Amina Chifupa, pamoja na kuwa alikuwa na umaarufu mkubwa lakini hao 'dada zako na kaka zako' hatukuwaona kwenye msiba huo hilo wewe hulioni. Angalieni vizuri mjue ni nani mbaguzi!
Mimi nilivyoelewa ni kwamba hawa ndugu zetu wanapitia njia nyingi ili kuweza kuonesha ubora wao katika mwafrika na kuonesha kwamba kwa kusoma katika shule za maana, kuandaliwa kwa mbinu mbalimbali na mengine, bado wataendelea kutumia mgongo wa mtanzania asilia kufanikiwa katika mambo yao.
Hili suala ni zito na linahitaji uchambuzi yakinifu kama alivyoainisha bwana Mjengwa.
Kwa kuongezea ni kwamba ni lazima kuanzishwe vijikampuni vingine vya kushindanisha mabinti na bwana Lundenga ili tuweka ushindani katika sekta hii inayoonekana ina ulaji.
Wizara husika pia iwe inatumia macho mambo kama haya yanoyogusa jamii kubwa ya watanzania ambayo ni vijana.
Pia nafikiri huyu dada alikuwa ashinde ndio maana amepoozwa kwa zawadi ingine angalau kutua roho.
Mambo Bongo ni mazito!
Rwabugiri, Katiba ya Tanzania inatoa sifa za nani anaweza kuwa Rais, je Rostam anatimiza sifa hizo? Kama hatimizi basi hawezi na hastahili kuwa Rais, kama anatimiza why not?
naona sasa ubinadamu wako ndio umekamilika, manake bila kutumia hiyo lugha wewe bado ni nusu mtu..........Its sad to see members reducing/lowering JF to the status of a chat room.It leaves me wondering at times what are all the intelligent people doing arguing with fools.Its a thankless job trying to educate those who are so narrow minded and shortsighted that they cant see beyond their noses.
Somebody with the rules and conditions for paticipants in this Miss Tz kindly post them here so we can figureout whether Richa ( Rachael )qualified to take part and more importantly WIN.
Had the award been a bicycle I dont think the question of her origin or colour would be a matter for discussion/argument today,I can assure you.
Richa amefanya yapi kati ya hayo? Na hawa Watanzania Asilia ni wapi?
Kama nilivyomuuliza mtu mwingine hapo juu niwaulize hivi Mtanzania Asilia = Mtanzania Mzawa?
hizi zote ni Bla Bla Bla... Miye nashauri huyu Binti ajiuzulu ili wampe mtu mweusi!
Huyu Shyrose Banji utamiita naani ?? Get a life man.
Kwenye hili mstari umechorwa, na pande mbili ziko dhahiri. Kuna wale ambao wamekubali na wanatetea ubaguzi wa rangi Tanzania kwa kisingizio chochote kile na wale ambao wanatetea usawa, uhuru, na nafasi sawa kwa kila Mtanzania bila kudali rangi, dini, nasaba, au mahali au asili ya Utaifa. Katika pande hizi mbili wapo wale wanaotaka kumhukumu Richa kwa rangi na asili yake na si kwa LOLOTE ambalo yeye alifanya au ametuhumiwa kufanya. Hakuna ambaye amekuwa na ujasiri wa kusema Richa amefanya hiki au kile ambacho kinamfamfanya asistahili kuwa Miss Tanzania. Tatizo ni kile ambacho hana uwezo nacho! Ni bora tuwe na Miss Tanzania ambaye amejitahidi kufikia pale kuliko kupewa Miss Tanzania ati kwa vile ni mweusi tu! Wabaguzi endeleeni kubagua, na sisi tutaendelea kuwaonesha kuwa ninyi ni wabaguzi, hakuna cha uzalendo wala utaifa mnaotetea!