Wakati nafanya kazi sehemu fulani nilikua naingia kwenye panel kama interviewer. Nilikua najikuta nakua na huruma na mwanaume mwenye miaka kuanzia 25 kupanda au fresher yeyote.
Hii ni kwakua mimi ni mwanaume na nishakua fresher. Naelewa struggle, so nilikua nauliza maswali ya kuwafanya waonyeshe strengths zao zaidi.
Kama unajitolea sehemu kwa miaka 3 na hujatengeneza connections na watu wa same industry ili wakupe shavu hapo inabidi ujitazame zaidi wewe kuliko kumlaumu HR na MD. Pia ukitaka kusurvive vizuri ofisini jitahidi watu waone potential at the same time uwe very genuine katika compliments na ushauri.
Anzia kwa anayefagia hadi huyo HR. Nilisurvive private kwa mtindo huu, yaani ilikua nachelewa kufika kazini ila watu wakiniona wanafurahi, nazidisha siku za likizo HR anapiga kusema wamenikumbuka.