HR na Maboss punguzeni ukabila wakati wa usaili

Kaka unazungumza kama utani binafsi yangu ukabila mara ya kwanza nilikutana nao bording unakuta wenzako wanadiscuss wa kabila moja, ukienda wewe kujiunga nao wanabadili lugha, yaan wanakubali kuongea kwa lugha yao ili mradi wewe usiwepo pale, atakayekuambia Tanzania hakuna ukabila anakudanganya!!!
 
Inaniuma sana unakuta una vigezo vyote lakini unakosa,alfu anakuja mtu anapata hiyo kazi na hana vigezo kisa ni kabila moja na HR .inauma sana hakika inakatisha tamaa
Hayo ni maelekezo toka CCM ambayo inateua watoto na wake wa familia zao kiasi kuwa akifa baba inabaki kopi yake.
 
Hii kesi lakini inaanzia mbali kidogo, mana mfumo uliokuwepo ni advanced u, lakini ulipoasilia kabisa ni ukoloni. Mana mkoloni ndiye alieacha maendeleo yaliyokaa kikabila ya leo hii. Kuna makabila yana access resources nyingi sana hasa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Haya hata enzi za ukoloni yalibebwq kwq kupata elimu na mashul3 mengi tu, na ndio hayohayo yana wasomi wengi leo, pia yalikuwa na idadi nzur ya wasomi enzi za ukoloni
 
siku hz hakuna wakuyasemea hayo ukabila umetapakaa kila kona.
 
Usitegemee sana maamuzi ya watu ili kutoboa, usitegemee sana kufurahisha watu ili waone na kukubali unachofsnya wakupromote.

Jinsi tunavyodhani wao wanatuwazia mema sisi, kumbe wao wanaona kua ni cheap labour. Hata usipolipwa ni sawa, wao wanaona kama wanakusaidia wewe na sio wewe kuwasaidia wao.
 
Duniani kote hayo mambo yote,ni wewe umwshindwa kanuni za mchezo.ulidhani ukiwa intern kwa muda basi usha jihakikishia.
Kuna mahali umezungua,may be kwa kuchukulia mambo poa.
Kila kitu katika maisha ni jitihada na politics
 
Hapo lazima uishiwe pawa.....
 
Inaniuma sana unakuta una vigezo vyote lakini unakosa,alfu anakuja mtu anapata hiyo kazi na hana vigezo kisa ni kabila moja na HR .inauma sana hakika inakatisha tamaa
Maswali haya yanakuhusu?
Uliingiaje kwenye kampuni inayoendekeza Ukabila kama unavyosema?
Kama kuna mwamba alikubeba mahusiano yake na hao uliowataja yakoje?
Tabia zako kuanzia Mdomo na mahusiano yakoje kiasi kwamba kile kilichofanya mwanzo wakupe nafasi kwa sasa hawakioni?
UnaHang out na watu wa aina gani hapo kazini maaana nyie watu kuna wakati wewe ni Intern lkn wewe ndie data base ya umbea kazini na majungu?
All in all usikate tamaa
 
Toa mfano wa hayo makabila Mkuu.
 
Du Kuna mda watu awaelewi hata uwe na potential, wanasema damu nzito kuliko maji
 
ukitaka ufanikiwe katika maisha lazima ujue who matter to you. Kama umeajiriwa mjue who matter katika Ajira yako (mwajiri). Ukiishi kWa ndugu angalia who matter katika familia ile na uwe karibu naye, ili mambo yako yanyooke. Mfano kuna familia ambayo mwanamke ndiyo mwenye sauti, hata ukiwa ndugu wa mwanaume, kila wakati jiegemeze na kuwa mnafiki kwa mama. Ukimdharau, utafukuzwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…