Huawei kuzindua mfumo wake wa uendeshaji simu janja mbadala wa Android

Huawei kuzindua mfumo wake wa uendeshaji simu janja mbadala wa Android

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Kampuni ya Teknolojia ya China, Huawei inaanzisha mfumo wake mpya wa uendeshaji wa simu za janja (smartphones) unaojulikana kama HarmonyOS baada ya Marekani kuizuia kufanya kazi na kampuni ya Google.

Huawei inatarajiwa kuzindua mfumo huo leo kwa baadhi ya vifaa kama simu za janja, vishkwambi (tablets) na saa za smartwatch. Kampuni hiyo bado imewekwa katika kizuizi cha kutumia huduma za Google ambazo ni maarufu zaidi katika kuendesha mifumo ya simu janja kwa watu wengi duniani, pamoja na kutumia vifaa vya kutengeneza simu kutoka kwa makampuni ya Marekani baada ya kutangazwa kuhusika katika mpango wa China wa upelelezi wa kukusanya taarifa za watumiaji duniani.

Hata baada ya kukanusha tuhuma hizo, Huawei haijaruhusiwa kufanya biashara na makampuni ya Marekani. Zuio hilo la kibiashara ni pigo kubwa kwa kampuni hiyo inayotegemea biashara na Marekani kwa kiwango kikubwa. Huawei imeporomoka kutoka kuwa kampuni inayoongoza kwa utengenezaji wa simu janja duniani hadi kufikia nafasi ya saba, ikipitwa na mshindani wake wa karibu, Samsung ya Korea Kusini.

Mfumo wa HarmonyOS ni mbadala wa kukosa huduma za Google katika simu janja za Huawei, hasa simu zinazouzwa nje ya China. Simu zilizouzwa kabla ya vikwazo vya kibiashara zitaendelea kutumia huduma za Google.

Kama suluhu ya vikwazo hivyo, Huawei ilizindua huduma zake zilizoitwa Huawei Mobile Services (HMS) ambazo zinawaruhusu watengenezaji wa programu tumishi za simu kuweka programu zao katika mfumo huo, na sasa Huawei inasema ina zaidi ya programu tumishi 120,000 katika hifadhi yake. Changamoto kubwa ya huduma hizo ni kukosekana kwa programu tumishi maarufu nje ya China kama vile Facebook, Instagram na Twitter.

Watumiaji wa mfumo huo mpya wa Huawei hawataweza kutumia huduma za Gmail YouTube, lakini Huawei inatoa mbadala wa huduma hizo. Huduma za Google hazipatikani nchini China hivyo watumiaji wa Huawei wa China hawataathirika na mfumo huo wa Huawei.

Huawei ina kazi kubwa ya kuwashawishi watumiaji nje ya China kukubaliana na mfumo wa simu janja ambao hauna huduma za Google kutokana na umaarufu wa huduma zake kama YouTube na Gmail.

Makampuni mengine kama Microsoft yaliyokuja na huduma za Windows za simu hayakuwahi kuwa na historia nzuri ya mafanikio.

Hata hivyo wachambuzi wanasema ikiwa HarmonyOS haitafanikiwa kinyume na matarajio, inaweza kutumiwa na wafanyabiashara wengine ambao hawatakuwa na uwezo wa kutengeneza mifumo yao wenyewe.

Chanzo: ABC News

1622637080427.png
 
Huawei hatimaye leo wameachia Harmony Os yao rasmi. Muda sio mrefu wameachia smartwatch yao ya kwanza yenye Harmony Os. Zaidi ya simu zao millioni 300 zitapata harmony Os kote duniani.

Hebu tuangalie kwanza hizi smartwatches kabambe. Jamaa wako live wakiendelea kutupa vitu vitamu kupitia Twitter,Facebook na YouTube.
Screenshot_20210602-155010.jpg
Screenshot_20210602-154952.jpg
Screenshot_20210602-154935.jpg
 
Tayari washaachia smartwatches kabambe huko. Wako live.
Screenshot_20210602-154952.jpg
Screenshot_20210602-154935.jpg
 
Kivipi mkuu..?
Kama vyombo vya dunia leo vinaongelea uzinduzi wa harmony Os halafu bado kuna watu tunabeza,duuh. Ngoja tuone mwisho wake.
Sio tetesi mkuu ni kitu ambacho kipo proved Harmony os ni android, kama mdau hapo juu alivyo sema wamebadili tu jina na muonekano ila code ni zile zile za Android.


Na ili kuficha emulator ya Harmony ina run kwenye server za Huawei mpaka uwe developer wanaekutambua ndio wa nakupa access, mimi na wewe haturuhusiwi kuchungulia.
 
Sasa kwa sisi wapenda you tube na kutumia Gmail na Google tukinunua itakuwaje
 
Sio tetesi mkuu ni kitu ambacho kipo proved Harmony os ni android, kama mdau hapo juu alivyo sema wamebadili tu jina na muonekano ila code ni zile zile za Android.


Na ili kuficha emulator ya Harmony ina run kwenye server za Huawei mpaka uwe developer wanaekutambua ndio wa nakupa access, mimi na wewe haturuhusiwi kuchungulia.
Mkuu mimi sio mtaalam kabisa wa IT,lakini nasikia hata Android Os kuna vitu vya linux. Na hata Windows Os pia. Kwa mtazamo wangu naona pengine ni njia ya kuwavuta wateja wajue kuwa kumbe Harmony Os ni Android tu,ili baadaye warekebishe kidogo kidogo na hatimaye kujitegemea kabisaaaaa.
 
Back
Top Bottom