Paulsylvester
JF-Expert Member
- Oct 15, 2021
- 1,464
- 3,379
Hali ni mbaya katika hospital za serikali,
Huduma ni za taabu sana, Jamani, binadamu kukaguliwa na homa, ni hali ya kawaida, Ila Inapotokea hali hiyo mtu umekaguliwa, basi angalau ukutane na huduma ya haraka!
Kwa sasa, mgonjwa kukaa masaa 6 mapokezi ni hali ya kawaida na masaa manne akisubiri vipimo ni hali ya kawaida! Na ninpoongea hili Niko hospitali moja ya (W) na ninayoandika haya, ndiyo nayaona na yananitokea nikiwa na mgonjwa akiwa na hali mbaya sana, nimefika SAA 1:30 mpaka muda huu wa SAA 4:53 bado sjahudumiwa chochote! Inauma sana!
Na Kwa macho yangu nikiwa hapa hapa, kaletwa mgonjwa, Kwa huduma kucheleweshewa, amefariki akiwa mapokezi! Maana yake inaonyesha hali hii imekita mizizi! Hili halikubaliki jamani.
Hali hii inaweza kumfanya mgonjwa afie mapokezi au akisubiri kipimo Kwa muda mrefu, na inakuwa mtu akiwa na mtu anayefahamiana naye, unaona tuu anachukuliwa katikati ya foleni, Mara tu unaona anatoka amekwisha hudumiwa,na hii hali, inashawishi utoaji wa rushwa!!
Wahudumu kupiga story wakiwa ofsini na wasijali kama kuna watu wanapaswa kuwahudumia imekuwa ni kawaida.
Lakini unajiuliza: Je, wao hali kama hiyo ikiwakuta na wao kutokuhudumiwa watajisikiaje?
Lakini, Kwa nini tunarudi nyuma kwenye kero ambazo tulikuwa tumeanza kuzisahau?
Je, Ni kweli sisi ni watu wa kusukumwa ili tufanye kazi na ndiyo maana ajira za nje zinatutema.?