Huduma mbovu za Mtandao wa TTCL: Malalamiko ya wananchi

 
Huku ndo rudi nyumbani kumenoga!

Hebu imagine nakaa katikati ya mjini centre napata mateso sana na huu mtandao.

Ushauri wa bure kama wewe ni mtu ambaye unafanya mishe zako mtandao au majukumu mbalimbali ambayo yanaitaji mtandao au unahitajika kila muda fulani uwe mtandaoni kwa muda muafaka usitumie TTCL.

Mtandao wao umekuwa wa ajabu sana unarudi na kupotea.

Kibaya ni kuna siku unaamka unakuta inasoma E tu na 3G yenye x hapo hata text za Whatsapp haziendi.

Tatizo limekuwa sugu na linajirudia kila siku yaani inamlazimu mtu kuwa na bando la ziada la mtandao mwengine maana wao hawaaminiki saa yoyote wanapotea na kuzingua mpaka masaa 6.

Customer care yao ndo jangaa unasubiri simu dakika 45 ndo wanapokea wanaboa kinyama.

Nimepata hasara sana kazi nyingi zinakuwa pending mtandaoni mtu anasema nafanya kusudi.

Wewe fikiria ndo nimejiunga bando la buku 5 kwa week halafu kutokana na mtandao wao kupotea potea nalazimika kuwa na bando jingine la mtandao mwingine ila wakipotea nitumie huko.

Hili ni bando la mwisho nikimaliza natupa line yao chooni hawana tofauti na continental decoder king'amuzi HD lakini no signal kila saa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simu ina gb 8 ram itakuwa 1:mkuu tatizo ni simu sio TTCL Kwa storage hiyo lazma ije E . ...MAPS GO....GOOGLE GO ogopa hizo simu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…