Ndio Christina Shusho analo kanisa lake (linaitwa The dreamer centre, liko Dar maeneo yq Manzese Tiptop), lina miaka zaidi ya saba sasa, wakati linaanzishwa ndio sekeseke la kuachana na mumewe lilipoanza kusemwa (maana Christina ndipo alipoanza kuonekana kutokuvaa pete ya ndoa na hakuonekana hata siku moja akihudumu na mumewe huku swaga zake zikiwa za usingle mother na sio kilokole) lakini Christina Shusho akapiga kimya. Muda umepita, kanisa halijalipa sana (waumini wachache na maokoto yakutafuta kwa tochi), sasa muelekeo umebadilika na kuwa kutafuta followers kwenye social media, kutrend kibongo flavour, kutengeneza kick na kuupiga chini ulokole mazima.