Huenda kuna waislam wengi duniani wameshazikwa wakiwa hai

Huenda kuna waislam wengi duniani wameshazikwa wakiwa hai

Hizo ni fikra potofu, ukizikwa mzima uelewe kua ndio majaaliwa yako au ndio njia uliyojichagulia ukiwa hai.

Jifikirie wewe mwenyewe kwanza, hivi sasa unafanya nini ili usizikwe ukiwa mzima? Wengi wenu mnajizika wenyewe mkiwa wazima bila kujielewa.

Ni vyema ukatoa somo/elimu ili wengi tusijizike wazima bila kujielewa...kama hautojali lete somo tujifunze..
 
Nisiseme mengi picha inajieleza
FB_IMG_1646570544749.jpg
 
Unaweza ukawa sahihi. Nilishawahi shuhudia tukio la jilani yetu binti wa kiislamu akizikwa kwa muda usipoungua masaa mawili tangu afariki baada ya kuanguka alipokua anapika chakula jikoni. Mbaya zaidi hata mama yake aliyekua sokoni hakuwahi kuzika.
Hahahaaaa wazee tupunguze basi uongo hata kama ndio kuponda Uislam isiwe kwa kujitoa ufahamu hivi.
Yaani hapo unamaana kaburi lilishachimbwa na mwili ulishaandaliwa ndani ya muda huo!!?.
 
Unaweza ukawa sahihi. Nilishawahi shuhudia tukio la jilani yetu binti wa kiislamu akizikwa kwa muda usipoungua masaa mawili tangu afariki baada ya kuanguka alipokua anapika chakula jikoni. Mbaya zaidi hata mama yake aliyekua sokoni hakuwahi kuzika.
katika Uislamu Mtu akishakufa hana lake tena duniani anatakiwa aharakishwe kuzikwa hata uyo Mama ake ata angewahi asingemsaidia chochote zaidi ya kulia
 
Ni utaratibu mzuri sana wa kuwahi kuzikana, ukikata moto asubuhi mchana tunazika

Ila nina hakika kuna watu wengi wameshazikwa Ili hali wakiwa wamezimia au wakiwa kwenye coma, hasa vijijini pasipo na hospitali na daktari wa kuthibitisha kifo.

Kuchelewa kuzika ni mbaya ila ina faida zake, maiti inaeza kupiga chafya. Mwaka 2012 mchezaji Fabrice Muamba wa Bolton wakicheza dhidi ya Spurs alianguka uanjani na moyo wake ulisimama kwa dakika 78.

Referee Howard Webb aliahirisha mechi huku machozi yakimtoka, uwanja mzima ni huzuni madaktari wa kizungu na kudra za Mungu jamaa akaamka bwana na kustaafu mpira rasmi.

Angekuwa Afrika tungeshamsahau na mke wake angekuwa single mother tayari, ila jamaa anakula bata tu.
Mtume Muhammad (sala ana amani ziwe juu yake ) ametufundisha kuwa kuna mambo matatu tunatakiwa tuyafanyie haraka, la kwanza ni swala kwa wakati wake , jambo la pili ni katika kuzika na la tatu ni kumuozesha kijana pindi anapotaka kuoa.


Uislamu umekataza MAOMBOLEZO ,kwani huwa yanapelekea kukufuru. So as long as ndugu wa marehemu wameshapata taarifa na wapo au wametoa idhini kuwa azikwe basi maiti itazikwa tu ...unaweza ukafa saa kumi jioni na ukazikwa saa 4 usiku.
 
Ila wakristo pamoja na kuchelewesha kuzika ila mwili si unakuwa kwenye friji tayar, sasa hiyo chafya hata ukiipiga ndani ya friji kunakuwa na faida gani.
Na waje na ushuhuda je kuna mtu ambaye alishafufuka baada ya kukaaa mda mrefu au kuchelewa kuzikwa.
 
Kwenye mchakato wa kuoshwa maiti pia wanakamua tumbo hadi wajiridhishe uchafu wote uliopo tumboni umetoka.
Dah yni mtu kauliza swali jingine ww ata sijui umemjibu nn kma hujui kitu ni bora kunyamaza
 
Back
Top Bottom