OffOnline
JF-Expert Member
- Apr 23, 2022
- 644
- 478
===
Baada ya kumsikiliza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan hapo juu,Naomba nidondoe kidogo haya,
Wakati wowote kuanzia Sasa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anakwenda kufanya mabadiliko makubwa Serikalini na kwenye Chama, Mimi Wacha niwalaumu kidogo nyie maboss na endapo Kati yenu atasalia basi rekebisha hili,
Viongozi wetu, Miongoni mwenu mmegeuka mabubu mara tu baada ya kifo cha Hayati Dkt John Joseph Pombe Magufuli , leo hii mmebaki na mama wala hakuna anayemtetea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Wala Serikali yake /yetu, Karibu wote mmepiga kimya,Sijui hili ni kwa bahati mbaya au ni kwa kusudio au mmechoka kuongoza,!!
Viongozi wetu, Wengi wenu mmekuwa mkijifanya nyie ni Wana-Serikali zaidi ya kuwa wanachama hata sare za Chama wengi wenu hamnazo na hamvai eti kisa nyie ni Serikali na wana wa Serikali tu,
Viongozi wetu, Tunakumbuka wakati wa JPM mlikuwa wasemaji wazuri sana wa miradi ya Serikali Ila leo mmegeuka mabubu ghafla kwa vigezo eti Mama hataki kusemewa vizuri kwa wananchi,Najiuliza hili nani kawaambia na lini?
Viongozi wetu, Sisi Wananchi tunahitaji viongozi walio Watendaji na Wasemaji, Haiwezekani Mkuu wa Mkoa au Waziri hana hata akaunti moja mtandaoni yeye kazi yake ni kuzurula tu na V8.
Viongozi wetu,Hivi hamfahamu Leo zaidi ya Watanzania milioni 25 wanamiliki simu Janja,Wewe kiongozi wao huna akaunti hata ya kupost barabara inayojengwa kwenye eneo lako kisa eti Wewe ni RC au Waziri unatuchelewesha sana na ni vema Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan wazingatie sana hili kwani hii dunia imebadilika sana inahitaji Viongozi kuwa wabunifu sana,
Viongozi wetu,Mtakumbuka Rais wa nchi kubwa kama Donald Trump alitumia mtandao wa tweeter tu kuongoza nchi kubwa kama Marekani why Wewe mwenye Wilaya uko busy kupiga dili tu ili siku ziende.
Sote tunafahamu Rais wa JMT Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan anayo akaunti Official kule tweeter Wewe DED huna ata akaunti moja kisa eti ni boss hakika kwenye karne hii 21 Wewe haustahili tupishe kwani Tanzania hii ya vyama vingi inataka kiongozi mwenye kutoa taarifa,
Sasa, huenda mabadiliko makubwa yakafanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ndani ya Serikali muda mfupi ujao nyie Mawaziri, RAS, DCs, DAS, DEDs baadhi yenu mmekuwa mizigo kwa nchi, Wengi wenu Mmegeuka mabubu ghafla baada ya kifo cha JPM huu si Uzalendo,
[Kidumu chama cha Mapinduzi]