Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Wananchi wengi watakuwa wanatumia bidhaa zilizoisha muda wake kwa kuuziwa na wauzaji wa maduka madomadogo maarufu kama maduka ya mangi na waha. Wauzaji wa bidhaa hizo aidha hawafatilii muda wa mwisho wa matumizi wa bidhaa zao ili wazitoe dukani au wengine hujua na kufanya kusudi kuwauzia watu huku wakijua kuwa hazifai tena kwa matumiz ila hujali wao kupata faida tu.
Si mara moja nimenunua bidhaa katika maduka mbalimbali na kukuta imeisha muda wa matumizi, na ukimwambia muuzaji anashangaa na kusema hakujua huku akishukuru kwa kumshitua kuna bidhaa imefika mwisho wa matumizi.
Huwa najiuliza ni watanzania wangapi wana utamaduni wa kusoma bidhaa kila wanaponunua? Kwa mazingira ya kawaida watu hununua na kuanza kutumia bila kuangalia muda wa mwisho wa matumizi na kutumia bidhaa ambazo ni sumu kwa afaya zao.
Jana usiku nilifika kwenye duka moja kununua bidhaa 3 za aina tofauti, mbili kati ya hizo zilikuwa zimeisha muda na hata alipojaribu kutafuta kama kuna ambazo zitakuwa bado zipo ndani ya muda ili anipatie hakupata alikuta kila bidhaa ya aina hiyo imeisha muda, wakati nipo hapo alifika mtoto mmoja na kutaka kununua bidhaa kama hiyo akiwa kaandikiwa kikaratasi ivyo sikuwa nimejuwa mtoto kaagizwa kitu gani.
Bila hata aibu muuzaji alitaka kumpa yule mtoto bidhaa hiyo, na alikuwa anafunga haraka kwenye mfuko kwa bahati akadondosha ile anaokota nikaona, nikamwambia mbona una roho ya ajabu ivyo huoni unamuuzia mtu kitu kisichofaa? Hakujibu akarudisha pesa za mtoto na zangu nikaondoka na nikamuacha na biashara yake.
Hivi mamlaka ya chakula na dawa huwa wanafanya ukaguzi wa bidhaa kwa hawa wauzaji wadogowadogo? Au ndio watajijua wenyewe liwalo na liwe, nani anasimamia kumlinda mlaji wa mwisho ukizingatia wengine hata maneno yaliyoandikwa wanakuwa hawayajui yana maana gani. labda ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa yanatokana pia na ulaji wa vitu vilivyoharibu na kutokufaa kwa matumizi ya binadamu, tuwe makini jamani.