Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Habari za jioni!
Sheikhe Pembe alikuwa akitoa maoni yake kama watu wengine lakini akasahau cheo chake cha usheikhe na dini aliyomo ambayo ni uislamu inamtaka awe mwingi wa tahadhari anapozungumza mbele ya Umma kwani anaweza kuudhalilisha uislamu na waislamu wa Tanzania.
Pembe alikuwa anajaribu kueleza hoja yake kuwa Bila Amani hakuna haki. Kwamba zile siku tano ukosefu wa Amani(vurugu ) kulipelekea haki zingine kama haki ya kupata huduma za kijamii kama elimu, afya na chakula.
Wakosoaji wa mtandaoni ambao wengi wanatumia majina ya kiislamu na walijitambulisha kama waislamu walisikitishwa sana na kauli hiyo na kuona kama shekhe anawatia aibu na kuifanya dini ya kiislamu yenye heshima kuonekana ni duni.
Sisi ambao sio waislamu mara nyingi tunasikia Waislam wakisema Uislamu ni DINI ya Haki. Na kwa namna hiyo uislamu ni dini ya Amani.
Waislamu wote duniani huonekana wakorofi pale haki zao zinapovunjwa.
Tumeona mpaka adui za waislamu huko duniani wakiuchafua uislamu na kuingiza propaganda kubwa ni ugaidi kisa na mkasa waislamu wakidai Haki zao.
Tunaona Palestina wakipigana kila siku ili wapate ardhi yao na wanaitwa magaidi na wavuruga amani.
Sheikhe Ponda kwa kuona aibu hiyo nafikiri akatumia nafasi yake kusawazisha ili kuwafanya waislamu wasiwe wanyonge na kuona viongozi wao wameshindwa kusema na kusimamia ukweli na haki.
Ingawaje Sheikhe pembe yawezakuwa alitoa maoni yake binafsi kama pembe na sio kama sheikhe na sio kwa kuusemea uislamu lakini ni vizuri wakati mwingine ukishakuwa kiongozi wa kidini kuwa mwangalifu ili usije ukawa sehemu ya kuwakwaza waumini wako na kuwarudisha nyuma kiimani.
Hivi inatupa funzo gani?