Kila mahali pana utaratibu wake, na hivyo hivyo unapokuwa chuoni sitarajii kila kitu kitakwenda vile unavyotaka. Hivyo ushauri wangu, wahusika wawasiliane na uongozi unaohusika kuwapangia mabweni ambao wako kwenye kila bweni kujua sababu za kuhamishwa ili kutafuta muafaka kabla ya kuanza kuandika mitandaoni. Hakuna jambo linafanyika bila sababu, ni vema tukawa watu wa kutatua changamoto zaidi badala ya kuleta taharuki ambayo haina msingi