Huku mtaani Rais Samia hakubaliki kivile, Upinzani wangekuwa na Mikakati 2025 wangeichukua nchi

Ukiachana na tabia za watanzania lakini nchi hii ilifika mda tupate raisi ambaye atakuwa anafanya maamuzi magumu kwa ajili ya manufaa ya taifa na RAISI Magufuli alipendwa sababu ya kuwaweka sawa watu wa hali ya chini na wajuu kwenye kundi moja bila mmoja kupewa kipaumbele, zamani ilikuwa tajiri anaweza kukwepa KODi lakini sio mtu wa kipato cha chini..mama samia hawezi kupendwa na watanzania SABABU yy anawatumikia wenye kipato cha juu na kuwakandamiza wenye kipato cha chini... kusema wawachie wafanyabishara wenye madeni account zao halafu kuja kuwabana wenye kipato cha chini kwenye TOZO hilo ni jambo ambalo hakuna ataweza kumpenda kingine Magufuli katengeza Nchi na watu wameona hata kama kuna mapungufu lakini samia alivyoingia kupitia sag akataka kumchfua huwezi ondoa MAPENZI YA WA TANZANIA KWA MAGUFULI KAMWE

Sent from my Pixel 4 XL using JamiiForums mobile app
 
NAJUA anatusoma au wanatusoma na nivizuri ili wajue tuliwaambia sasa ni hivi; to light up, ni kweli ujue sie wananchi wa kitaa na mkanyageni ndio tunajua mengi na kuyaona kwa kuyashuhudia na kuyaishi si tu kuyasikia. Ni UKWELI usiofumbika inabidi CCM na mamlaka husika ijipange na ifanye kazi ya ziada kuweka mambo mswano, to be honest approval ratings ya SSH imeshuka kwa kasi sana na kwa muda mfupi tofauti na alivyoingia.

Si mijini si mikoa ya kati si kaskazini si kusini si pembezoni si vijijini (tena huko ndio hawaelewi kabisa mambo yanavyoenda: mind you aisee kuna watu vijijini wana uelewa mkubwa sana kuliko wa mjini) si visiwani si vizimbani na chakushangaza kabisa na kabisa si wanawake na akina mama ambao tulitegemea wao wawe mstari wa mbele na wakwanza kumlinda na kumshangilia ila ndio wanaoongoza kutomkubali.

Katika siasa ni suala la kawaida ila likiachwa sana litakififisha chama na si yeye. Nikirudi nitakuja na kipi kifanyike.
 


Umenena sahihi kabisa.
Tunakusubiri
 
Endelea kusubiria meli jangwani.
 

Hakuna watu wasiolipa Kodi Kama Masikini
 
Hizi tunaita makala fyongo kutoka kwa watu fyongo. Hata upinzani ungekuwa na ushawishi gani, uchaguzi ukiendeshwa kama ulivyoendeshwa 2020 unadhani kutakuwa na mabadiliko? Zanzibar upinzani unashinda karibu chaguzi zote zilizopita na 2015 walishinda hata watoto wadogo walijua. Ni nini kilitokea? Bla bla bla nyiiiiingi lakini akili zero.
 

Upinzani ukiwa na ushawishi mkubwa kwenye jamii hakuna upuuzi ungefanyika take it from me.

Hao polisi wasingekuwa na uwezo wa kusogeza pua zao kuonea watu kisa wametumwa kwani wanajua hatari ya kufanya hivyo
 
Point yako ipo sahihi ,huyu bibi hakubaliki mtaani .anayebisha abishe.
 
Upinzani ukiwa na ushawishi mkubwa kwenye jamii hakuna upuuzi ungefanyika take it from me.

Hao polisi wasingekuwa na uwezo wa kusogeza pua zao kuonea watu kisa wametumwa kwani wanajua hatari ya kufanya hivyo
Nimekuuliza: Kule Zanzibar walikoshinda tena kwa kura nyingi kabisa hawana ushawishi? Wewe huna hoja yoyote ya maana.
 
Nimekuuliza: Kule Zanzibar walikoshinda tena kwa kura nyingi kabisa hawana ushawishi? Wewe huna hoja yoyote ya maana.


Unajua maana ya ushawishi lakini??

Kama Upinzani ungekuwa na ushawishi ZANZIBAR isingetawalika amini nakuambia
 

kwan wanaopinga chanjo ni watanzania tu? mama taikon πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Unajua maana ya ushawishi lakini??

Kama Upinzani ungekuwa na ushawishi ZANZIBAR isingetawalika amini nakuambia
🀣 🀣 🀣 🀣Huna hoja yoyote. Kinachofanya CCM iweze kutekeleza uhuni wote huo ni kalba ya watanzania. Tukiacha siasa za kuingia Ikulu toa mfano wowote wa kitu ambacho wananchi walishahamisika kwa ushawishi na kuipinga serikali. Mfano mdogo tu ni huu wa ongezeko la tozo. Watu wanapiga kelele chini chini tu lakini hakuna wanaojitokeza kuchukuwa hatua yoyote. Mbona Kenya wananchi wako very sensitive kwa mambo mengine nje ya siasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…