Huku mtaani Rais Samia hakubaliki kivile, Upinzani wangekuwa na Mikakati 2025 wangeichukua nchi



😃😃😃😃😃

Mkuu siku zote namna Bora ya kudili na mjinga ni kumdanganya.
Na masikini basi mdhulumu.
 
HAWA wananchi uliowakusudia wamekaa lini kikao Cha kumkataa? Wananchi hawa ninao wafahamu tokea kipindi kile Cha kikombe Cha Babu? au wale wa enzi za nyungu? au unamaanisha wale waliogomea Chanjo lakini Leo wapomakini kujaza mkataba ILI wachanjwe? Utakuwa umekosea kuona tafuta miwani mfano mzuri vuta kumbukumbu Mpaka enzi za wajumbe hapo utabaini rangi ya wananchi wa Bongo.
 


Mkuu, nilichoandika ninauhakika nacho.
Sipo kumfurahisha wala kumkwaza yeyote.
Isipokuwa kuandika Hali halisi
 
Chama kikuu cha upinzani ni Chadema.
 
Usichokijua ni kuwa, huhitaji huo ushawishi koko unaodhani. CCM tayari wanayo machinery ambayo hata wakimpa kiti Pierre Liquid anapita tu.
 
Sasa hao wapinzani wangeshinda kwa tume ipi hii ya akina Mahera. Wewe unaota ndoto huku unatembea.
 
Ndio maana mi huwa nashauri ukiwa Rais ni lazima uwe na ngozi ngumu kweli kweli. Fanya kile unachoamini ni sahihi basi, na wala usisubiri feedback.

Rais Magufuli alikuwa tough baadhi ya watu hawakupenda utough wake.
Rais Samia ni a bit soft and compromising bado kuna watu hawakubali namna zake.
Ukisimama nchale, ukikaa nchale, wtf?

Samia akiwa principled, akafanya kazi na matokeo yakaonekana, umpende usimpende kazi zake zitaimba sifa zake.

Leo Magufuli ni miezi karibu sita, lakini bado yupo kwenye vinywa vya watu.

We unafikiri watu wanamsema sema Magufuli kwa sababu wanataka kumsema? Wanamsema kwa sababu wanalazimika kumtaja.
 
Usichokijua ni kuwa, huhitaji huo ushawishi koko unaodhani. CCM tayari wanayo machinery ambayo hata wakimpa kiti Pierre Liquid anapita tu.
Kwa sababu wao ndio refa na ndio wachezaji, hivyo kwa kifupi ni kwamba hakuna uchaguzi Tanzania ni uhuni tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…