Huku ni kukomoana, sijawahi kuona wala kusikia kama hili duniani, TRA mjiangalie

mahindi hayaoti mjini

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2022
Posts
2,120
Reaction score
2,709
Pamoja na umachinga wangu, bado nikasema nisaidie nchi yangu kwa kulipa kodi, nimechukua tin namba nikakata leseni nikafungua kiosk, nikakadiriwa nilipe laki nne kwa mwaka, kila miezi mitatu 100,000/=.

Nimelipa vizuri mara tatu, mara ya nne nimechelewa kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu ikiwemo biashara kuchechemea,

Wiki iliyopita nikakopa ili nilipe deni la serikali nakuta kuna 100,000/= principal,
1500/= riba na 150,000/= adhabu au faini ajili ya kuchelewa kulipa,

Hivi kweli mimi nitafanya biashara halali tena?

Serikali na nyie tra mjiangalie sasa
 
Wewe unasema hivyo mm nililipa 1 million kwa biashara ambayo haijawah ku operate hata siku moja..
Niliumia sana sitasahau isee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…