Mkuu unakitu flani,. Naomba tueleweshe tena tafadhali
Mkuu, Afisa TRA kazi yake ni kukusanya au kutengeneza fedha kupitia kodi, hili ndo lengo kuu na anapimwa nalo.
Mara nyingine japo si mara zote maafisa esp wanaosimamia small na medium tax payers huwa wanatoa majibu ya midomoni kukidhi miongozo ya malengo yao waliyopewa. Hawakuambii wazi ukitaka usilipe ni nini cha kufanya.
Hii mbinu wanaipenda mno sababu sisi huwa tunachukua majibu ya midomoni ya maafisa kama majibu rasmi ya serikali kupitia TRA kumbe afisa wakati anakujibu alikuwa anawaza target zake alizopewa na incharge wake.
Sasa tukichukulia mfano wa mleta mada, adhabu na interest zipo kisheria na ni halali, ila sheria hiyo hiyo inaruhusu kusamehewa adhabu kwa makubaliano ya kulipa principle na wafanyabiashara wanaendelea kusamehewa adhabu na riba kwa utaratibu huu.
Sasa, hakuna haja ya kubishana na afisa maana yeye ana uwezo wa kutumia kutokujua kwako kufikia malengo yake aliyowekewa.
We unajiuliza tu maswali:
Hii adhabu ni halali kusheria? Ndio
Naweza kuilipa? Hapana.
Nina haki ya kutokuilipa kisheria pamoja na uhalali wake? Ndio.
Unapambania jambo lako.
Njia pekee ya kupata haki yako ni majibizano kwa njia ya barua. Hata ikitokea incharge au manager kesi yako imemfikia, akiitisha file anapata historia nzima si bla bla za niliambiwa hivi, nikaambiwa vile.