Huku ni kukomoana, sijawahi kuona wala kusikia kama hili duniani, TRA mjiangalie

Huku ni kukomoana, sijawahi kuona wala kusikia kama hili duniani, TRA mjiangalie

Yote hayo nafanya mkuu na niko makini sana sana sana,.

Nadhani Ilitokea tu mistake nilichelewa nayo ilikuwa ni kwasababu ya mtandao,. Na sikuwa nafahamu mpaka nilipoenda kuomba Tax clearance ndio nikakutana nalo hilo na wamekaza inabidi nilipe licha ya kujitetea na kuomba kufutiwa,.
Itakuwa figisu tuu mara ya mwisho nimeomba Tax clearance na kampuni ilikuwa na deni la 140mio plus na wakanipa mbona
 
Pamoja na umachinga wangu, bado nikasema nisaidie nchi yangu kwa kulipa kodi, nimechukua tin namba nikakata leseni nikafungua kiosk, nikakadiriwa nilipe laki nne kwa mwaka, kila miezi mitatu 100,000/=.

Nimelipa vizuri mara tatu, mara ya nne nimechelewa kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu ikiwemo biashara kuchechemea,

Wiki iliyopita nikakopa ili nilipe deni la serikali nakuta kuna 100,000/= principal,
1500/= riba na 150,000/= adhabu au faini ajili ya kuchelewa kulipa,

Hivi kweli mimi nitafanya biashara halali tena?

Serikali na nyie tra mjiangalie sasa
Ungeuliza watu kwanza. Ohh ona sasa kimekulamba.
 
Mbona unakuwa kama Mkopo 😅
 
  • Thanks
Reactions: apk
Ila naona serikali wanazingua sana kazi tu kujifungia maofisini, unajua nini, unaweza kuongea mengi mwisho wa siku ukawa unapigia mbuzi gitaa. Tutaenda nao hivyo hivyo wanavyo taka. Hii nchi watu wake wamezoea wizi.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Halafu eti Huwa wanashangaa kwanini nchi hii walipa Kodi ni 9% tu ya watanzania wote... Hawajui kwamba tatizo la idadi ndogo ya walipa Kodi linaanzia kwao.
Hivi mtu na akili zake na usomi wake na unakuta katokea maisha ya chini utasema wanashangaa kwamba hawajui, wanaelewa sana kodi wanazo kadiria wananchi sio rafiki kabisa
 
Ndio maana nafunga biashara nianze kukimbizana nao na mie angalau nitajirike sasa
Kwa nini ufunge biashara? Hapa kilichotokea ni kukiuka sheria kwa kutolipa tarehe husika. Hesabu hiyo ni hasara lipa hiyo fine pamoja na wanachostahili.

Cha kukushauri kwa kuwa tayari una faini kwa kuwa umevusha mwezi Unaweza amua kuizungusha hiyo pesa mpaka tarehe 28 huko ndio uwalipe pmoja na fine ila usivushe kwenda mwezi wa pili utakutana na penalty nyingine. Huenda ndani ya wiki mbili inaweza kuwa imekuletea hata 40,000 au zaidi ikitegemea biashara yako.

Kufunga biashara kwa changamoto ya siku moja utakuwa uzembe wa hali ya juu.
 
Yaani wanavyowakomalia hivyo utafikiri wako serious wanatafuta hela ya serikali kumbe wanatafuta hela ya ada za watoto wao na kumalizia nyumba zao.
Nishafunga biashara moja. Hii iliobaki nawasubiri siku ya discussion hawataamini nikiwaambia hio hela mnayotaka nilipe sina, fungeni boashara.
Kaka ukiwakuta hao wakusanya Kodi walivyo na juhudi za kukerembesha watu hili walipe Kodi, unaweza ukasema ni watu wenye uchungu sana na taifa hili... Kumbe ni majizi tu yanayotumia uniform za utumishi kuwaibia wanainchi... Na pesa yote inayokusanywa inaibwa kimatabaka, kwanzia Kwa Mwigulu nchemba mpaka Kwa vidagaa wa chini(Tax officers).

Halafu Huwa wanafikiria kumfungia mtu biashara ndio sululisho sahihi, hawajui kwamba waathirika wakubwa ni wenyewe Kwa kukosa mapato na pesa za kuiba
 
Na wewe unakadiriwaje kodi kubwa unakubali kulipa? Hio kodi kwa hio biashara ni kubwa
 
Tra inasababisha wananchi wanakua wajanja,mambo yanayofanyika na vijana wa tra ni balaa,kodi inaumiza
Double taxation nayo ni tatizo
TRA kuweni na mipango mizuri ya kuwasaidia wafanyabiashara ili mkusanye mapato mengi zaidi na si kukandamiza,
Kuna ujinga mwingi sana unafanyika na kina zakayo na tunajua ,na mpaka kwa majina lakini jirekebisheni
 
HAWA JAMAA NI BURE KABISA KWANZA HAWAKUPI ELIMU ILI UWEZE FANYA BIASHARA NA KULIPA KODI KIRAHISI WANACHOTAKA WAO NI UKOSEE ILI WAKULIME

HAWA JAMAA NI BURE KABISA KWANZA HAWAKUPI ELIMU ILI UWEZE FANYA BIASHARA NA KULIPA KODI KIRAHISI WANACHOTAKA WAO NI UKOSEE ILI WAKULIME
Mkuu Mimi Niko kwenye biashara na mwaka wa 3 huu Mimi nachojua kwenye makadirio inategemeana na wewe kwenye maelezo yako na jamaa anaekukadiria una haki ya kukataa kama umekadiriwa kodi kubwa ambao huwezi kulipa
 
Back
Top Bottom