Huku tukijivunia ndege zetu, wanafunzi 52,000 hawana madarasa ya kusomea

Hii taarifa umeiandika kiumbea umbea sana, ndege lazima zinunuliwe na SGR inajengwa na mambo mengine yanafanyika na yataendelea kufanyika vilevile
acha mahaba shida sio ndege wala reli sheedah ni balance ya ufanyaji wa hayo mbona lipo wazi jiulize ni kwa nini mtu akipata pesa angalau anampeleka mtoto shule binafsi ACHA MAHABA ifike mahali kwenye ukweli tuungane na uongo tuungane kuupinga
 
Tatolizo hapa ninaliliona ni wizara ya elimu,Yule mama Prof ndalichako hajaweza kutumia elimu take kunisaidia elimu ya Tanzania,na hata hajaweza kumsaidia mh Rais kwenye sekta ya elimu. Wanafunzi 52,000 wanakuja kukosa madarasa wakati wamechaguliwa,wizara haikuweza kufanya projection kabla ya watoto kuchaguliwa ili waanze kujenga madarasa kabla? Automatically Kama watoto 52,000 wamekosa madarasa, tayari watoto hao hawana madawati,hawana viti,hawana vitabu,hawana vyoo vya kuwatosha,hawana maabara,hawana library,hawana mabweni,hawana vitanda,hawana walimu je amejipangaje kwa hayo yote? Prof ndalichako viatu ulivyopewa na Mh Rais sio saizi yako unamwangusha usiku na mchana,jifunze kwa waziri ummy mwalimu alivyo boresha sekta ya afya.Prof ndalichako jitadhimini utendaji wako.Hali ya sekta ye elimu sio nzuri hata kidogo.jiulize kila Halmashauri unao maafisaelimu wawili wawili (elimu msingi na elimu sekondari) Ila Mambo hayaende na wanalipwa mishahara mikubwa bila hata wewe kujua malipo yao,wizara ya afya kila Halmashauri Ina mkuumomja wa idara ya afya Mambo yanaenda vizuri jiulize.muundo na mfumo wa elimu ya msingi na sekondari ni mbovu,haifai,ni wa kufanyiwa marekebisho makubwa.kila Halmashauri inatakiwa uwe na bosi au mkuu mmoja anayehusika na elimu ya msingi na sekondari na mwenye qualifications na uzoefu mzuri.mchezo unaofanyika Sasa afisaelimu msingi wafaulisha watoto anampeleke afisaelimu sekondari ,wakati huo huo afisaelimu sekondari jana taarifa na wanaoletwa sekondari na Hana kumbukumbu za idadi ya walioko msingi kabla ya kumaliza darasa la Saba na kufaulu.mwisho afisaelimu sekondari anakuja kutaaruki idadi ni kubwa mwisho na Hana miundombinu yeyote na muda umemalizika wanafunzi wahitaji huduma na Hana Wala hakufanya projection ya mwaka unaofuata.hivyo ni muhimu afisaelimu see mmoja ili kuunganisha mfumo na mawasiliano.mfumo ulipo na inayotumika sio rafiki kwa walimu,wanafunzi na miundombinu ndani ya Halmashauri moja.Ndani ya Halmashauri moja mkurugenzi ni mmoja,walimu Wana mabosi wawili ndani ya Halmashauri moja yenye mkurugenzi moja,maelekezo pia yanatofautiana kuwafikia walimu.
Ninadhauri kututwa kwa idara ya elimu msingi na elimu sekondari na kuundwa kwa idara moja itakayojulikana Kama Idara ya elimu ,kwa Sasa utata uliopo ni mkubwa sana na unaliletea serikali hasara ya raslimali watu na Mali zao.
 
Hii ni kaz ya serikal unatak achangie nn sasa ? Yeye ashachangia kodi
 
Umeonesha umbumbumbu wa mwendokas ya SGR
 
Mkuu hatupingi kununuliwa ndege au kujenga sgr.
Kwa uoni wako lipi nimuhimu?

Ndege kwa ajili ya kukuza utalii? Au madarasa kwa ajili ya watoto wetu?

Kuna siku ulishindwa kusafiri/kusafirisha kwaajili kuwa hakuna sgr?

Sio kushangilia tuuu.. kila kitu, kwa faida ya nani?
Hii taarifa umeiandika kiumbea umbea sana, ndege lazima zinunuliwe na SGR inajengwa na mambo mengine yanafanyika na yataendelea kufanyika vilevile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
si ni ametoa/Amelipa/Analipa/Atalipa kodi...
Billions Unanunua ndege
Maji hakuna
Elimu majanga

Tatizo wananchi ni wa,,,,
mje mnirushie maneno
 
Hili tatizo linajitokeza kwa kuwa Serikali inashindana na Sekta binafsi badala ya kushirikiana. Hizi kauli za waliosoma shule za binafsi kunyimwa mikopo ndizo zinafanya baadhi na miundo mbinu ya sekta binafsi kuwa tupu huku watoto wakijazana shule za Serikali.

Kama ni vipi Serikali ifuate utaratibu ule ule wa kugharamia hospitali za binafsi DDH kwa kupeleka ruzuku na kuwapanga wanafunzi kwenye shule zisizo na wanafunzi wa kutosha ila miundo mbinu ya kufundishia ipo
 
Pitia hesabu zako kuhusu wanafunzi 500 na madrasa 20
Tatizo nini? Mbona kwa hao 500 unahitajj madarasa 10 tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo elimu tu afya nako hali ni tete. Wazee kinamama wajawazito ambao kisera wanatakiwa wapate huduma bure wote wanatakiwa kulipia dawa na huduma zingine. Huwezi utajiju sisi tunasonga mbele na SGR, ndege, nadaraja ya flyover, umeme n.k. Haya ndiyo tuayotaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.....kinachotakiwa ni kuwajengea uwezo na kuwawezesha
Kwa hiyo haumini kuboresha na kujenga mindombinu mipya ni moja ya mkakati wa kuwajengea uwezo na kuwawezesha wananchi!? Kazi ipo kweli ya kuwawezesha watu kufikiri kwa mapana.
 
Kwa hiyo haumini kuboresha na kujenga mindombinu mipya ni moja ya mkakati wa kuwajengea uwezo na kuwawezesha wananchi!? Kazi ipo kweli ya kuwawezesha watu kufikiri kwa mapana.
Mkuu kuna stage tunaziruka, huwezi kuacha watoto katika mazingira duni ya kusomea kama yale then unasema unawawezesha kwa kununua ndege. Huwezi kuwatelekeza wakulima na wafugaji kiasi kile ukasema unawajengea uwezo kwa ndege na SGR. Chukua muda wako kidogo upitie hizi terms mbili kwa ufupi tu 1. Economic growth 2. Economic development.
 
CCM ya Magufuli ni LAANA. Tuikatae Tanganyika na Zanzibar. Imekuaje hili wameshindwa kupiga tantalila tanzania mpya. MATAGA.

Nchi ya wajinga sana hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…