Huku tukijivunia ndege zetu, wanafunzi 52,000 hawana madarasa ya kusomea

Hivi Ule mkakati wa kutengeneza madawati wa 2016 uliishia wapi.....!? Au hawakutua kuwa hilo zoezi linatakiwa kuwa endekevu na siyo zima moto...!!?
Mkuu wa mkoa ndio aliouua baada ya kujaribu kutumia mwanya ili kukwepa kodi
 
Kumbe uko lindo. Nakupa tafu leo..Ha ha ha aa!
===
Mkuu wapangeni vijana wenu sawa sawa, wanaleta hoja za kudhalilisha " chama cha akili kubwa" Ajibu hayo maswali tuone ukubwa wake wa 'akili' maana ndiyo kauli zenu hizo.Ha ha haa!
Anachangia kwa kulipa kodi, halafu achana na maswali ya kilofa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wacha kutafuta mitaji ya kisiasa,elimu bule ilikuwa wakati ule baada ya uhuru ,dalasa moja la watoto 45 daftari bule ,wino na nibu, vikausho bule lugha ya mabeberu ilikuwa moto,.Kwa sasa wale wazazi wasiotambuwa ubora wa elimu ya watoto wao ndio wanapeleka mtoto shuleni bila kumpa chai asubuhi,kule shuleni hakuna uji wazazi wasichangishwe ela yoyote .Hapa nikujidaganya matokeo hili asome vizuri wazazi wakazanie lishe ya watoto ndipo watoto wao watasoma kwa furaha na mafanikio.
 
"Adui no.1 wa ccm ni ELIMU".kamwe hawawezi kaa pamoja na mdadisi,mwelewa na anayetumia "ubongo" wake vizuri.RUNGU NA VIPIGO havichelewi kutembezwa.
 
Kipaumbele chetu ni kununua ndege hayo mengine hayatuhusu!!
 

''Hapa Kazi Tu. Nataka Watanzania mtembee vifua mbele nchi iko kwenye ze laiti tlaka!! Fyatueni watoto wengi Serikali ya Magufuli itawasomesha bure kwerikweri'' Rais Dk. John Joseph Pombe Magufulications.

Kuna jambo moja la kujifunza hapa ya kwamba tawala nyingi za Kiafrika na Kibongo bongo kama hii ya Magufuli zina kasumba moja kubwa. Ili waendelee kukutawala daima jambo la kwanza ni KUWANYIMA ELIMU WANAO WATAWALA.
Kwa Tanzania huu ni utamaduni wa CCM wa zaidi ya miongo 5 sasa. CCM wanatumia sana mtaji huu wa kuendelea kuwafanya Wadanganyika kuwa vilaza ili wawatawale bila mikwaruzo wala kelele..!!! CCM wanajua ukimwelimisha mtu akaelimika hatakubali tena huo upuuzi wako wa kuendelea kumtawala, kumnyanyasa, kumdhulumu na kumkandamiza!!

Na ndiyo maana ukiangalia mfumo au Mtaala wa Elimu ya Tanzania uko kimaghumashi zaidi. Shule za private zinatoa wanafunzi bora zaidi ilihali hizi za Asante Kayumba zinashika mkia. Hakuna mtoto wa Kigogo kuanzia Magufuli mwenyewe, Waziri, Katibu Mkuu, RC au DC mabaye mtoto wake anasoma shule za Kata...!!!Kama haitoshi watoto wao wakishatoka shule za Private wanakwenda kusoma Vyuo Vikuu vya nje na wakirudi ndio wanaopewa nafasi kubwakubwa ili kuendelea kuwatawala Wanyonge na Vilaza wa Tanzania...!!!

Kwa maana hiyo Watz wasitegemee Serikali ya CCM ikasimamia Elimu katika ubora unaotakiwa...!!Haitatokea hata siku moja. Mambo haya yataisha kama zimamoto kwa kujenga madarasa ya dharura yasiyo na ubora, bado hawatakuwa na Waalimu wa kufundisha hiyo idadi iliyoongozeka...!!!
 

Wewe kama TUJITEGEMEE, unatoa mawazo gani kutatua changamoto hii ili kumsaidia Rais Magufuli kutatua tatizo hili la upungufu wa madarasa?
Mleta mada ameleta hoja hii akionesha kushindwa kabisa kwa Utawala huu kuhusu kusimamia VIPAUMBELE VYA KITAIFA! Mtu anapohoji kwanini Serikali imenunua midege ya Mabilioni ilhali imeshindwa kujenga vyumba vya madarasa ambavyo thamani yake ni some few hundred millions tayari anaonesha njia!!! Hivi kwa akili yako kama wewe ni baba nyumbani unakwendaje kununua gari ya bei kali wakti watoto nyumbani hawana chakula? Hiyo ni akili gani kama siyo ubazazi?
 
Ni sawa kabisa na yule baba katika familia ambaye ana afya tele na kipato kimono lkn ni mwenye uchu wa kununua magari ya kifahari, huku anajitupia suti na unyunyu wa bei ghali wakati familia yake inapigika ile mbaya na maisha ya kila siku na watoto wake wana utapiamlo wa kufa mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitu sensitive Kama hivi alafu mtu analeta ushabiki
Uhaba wa madarasa vyumba siyo jambo dogo. Ni tatizo/changamoto. Lakini kitendo cha kuleta changamoto hii kwa mtindo wa hoja hapa jukwaani kwa lugha za dharau, kibri, na kebehi..HAKIKUBALIKI. Na kwa maneno mengine mleta mada haoni changamoto hii kama senstive issue. Huwezi kuelezea issue senstive kwa lugha za namna hii ambazo zina'lengo' la kugawanya badala ya kujumlisha.
Wapigeni msasa vijana wenu mnaowapanga kuleta hoja jukwaani, ili walete hoja sensitive wakiwa wamezivisha 'nguo' safi...!
 

Bwana wee mbona unakurupuka kujibu hoja?
Hivi umeelewa hoja iliyoko kwenye mada? Hapa tunazungumzia WANAFUNZI 52,000 kukosa vyumba vya madarasa na siyo 52,000 kama idadi ya vyumba...!!Watu huwa mnafeli hata mitihani vivi hivi. Soma swali, elewa na ndipo ujibu! Acha kukurupuka!!
 
Mkuu nowdays jiwe amekufanya kuwa kibogoyo wa hoja pole sana! sijui ulitaka mleta hoja awasilisheje ikiwa mtawala wako anasema maendeleo ni ndege huku anaowaita wanyonge hawana vyumba vya madarasa au anafanya kusudi wasisome ili aendelee kuwaita wanyonge maana inaonekana ndio mtaji wake
Sent using Jamii Forums mobile app
 



Tuuze midege tujenge MADARASA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…