Tetesi: Huku wachina kule mvua, njaa na maradhi vinatuua watanzania

Tetesi: Huku wachina kule mvua, njaa na maradhi vinatuua watanzania

Wachina wanajenga mradi gani?
Maana Stiglers ni Wamisri na SGR ni Waturuki,
kwa taarifa yako mchina kajenga hata nyumba ya baba yako! ulipo yupo hata kama humuoni
 
Sawa,logic iliyopo ni kuwa hakuna uhusiano wa miradi inayoendelea nchini na mvua kutokunyesha.Ukame wa huko ni mazingira ya asili.Hivyo basi hapa nchini mvua kutokunyesha ni mabadiliko ya mazingira kiasili zaidi pasipo na uhusiano wowote wa kuwepo utekelezaji wa miradi nchini chini ya Waturuki na Wachina,hawachawii wala kupiga mabomu kutawanya mawingu ya mvua.Waza nje ya box men.

Mfano ukiumwa tumbo baada ya kula kiporo cha wali maharage,wakati kisababishi kikuu ni wewe kufakamia mivyakula ovyo ulipokuwa unakuja Dsm kutoka kwenu Ramadi-Magu kwa basi la Najimunisa.Je,utaanza kumlaumu yule mchepuko wako wa jirani ndio amekuchawia ili udhurike na urudi haraka kumliwaza au ni ufakamiaji wako wa mivyakula ovyo njiani?Logic hapa itakuwa ni ulaji wako wa ovyo na sio kiporo cha wali maharage.

Kwa hiyo sio Wachina au Waturuki wanaokataza mvua kunyesha,bali ni majanga ya asili yanafanya kazi.Majanga yasiyo ya asili ni uharibifu wa mazingira unaosababishwa na sisi binadamu.Waza nje ya box men.
Turkana ni kame miaka nenda rudi sasa wewe unaleta ya jangwa la sahara hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiografia ya kule ni tofauti kabisa na huku, kule kuna asili ya jangwa na imekuwa climate ya pale over mostly
Hata huku mazingira yanaweza kubadilika kutokana na daily human activities(nadhani unazijua) na kusababisha mvua kutokunyesha.Kwa hiyo Wachina na Waturuki tunawasingizia tu.Jiografia ya mahali "can change at any time and not static at all the time"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nachofahamu ni kuwa hali hii si tz peke yake, kwa wafuatiliaji wa mambo wanajua kuwa ncha ya kaskazini (North Pole), imekua na mgandamizo mkubwa wa hewa huku South Pole ikiwa na mgandamizo mdogo wa hewa. Wanavyodai wataalam wa maswala ya hali ya hewa hii imepelekea pepo kuvuma kuelekea baharini baadhi ya naeneo, ndio chanzo cha majanga yaliyo sababisha maafaka kwa nchi za Msumbiji, Malawi na Zimbabwe.

Wataalam watachambua vema, maana mchina anasingiziwa bure. Maana hali hii wataalam wanasema iliwahi kutokea miaka kadhaa nyuma (sikumbuki vizuri mwaka walioutaja).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa,logic iliyopo ni kuwa hakuna uhusiano wa miradi inayoendelea nchini na mvua kutokunyesha.Ukame wa huko ni mazingira ya asili.Hivyo basi hapa nchini mvua kutokunyesha ni mabadiliko ya mazingira kiasili zaidi pasipo na uhusiano wowote wa kuwepo utekelezaji wa miradi nchini chini ya Waturuki na Wachina,hawachawii wala kupiga mabomu kutawanya mawingu ya mvua.Waza nje ya box men.

Mfano ukiumwa tumbo baada ya kula kiporo cha wali maharage,wakati kisababishi kikuu ni wewe kufakamia mivyakula ovyo ulipokuwa unakuja Dsm kutoka kwenu Ramadi-Magu kwa basi la Najimunisa.Je,utaanza kumlaumu yule mchepuko wako wa jirani ndio amekuchawia ili udhurike na urudi haraka kumliwaza au ni ufakamiaji wako wa mivyakula ovyo njiani?Logic hapa itakuwa ni ulaji wako wa ovyo na sio kiporo cha wali maharage.

Kwa hiyo sio Wachina au Waturuki wanaokataza mvua kunyesha,bali ni majanga ya asili yanafanya kazi.Majanga yasiyo ya asili ni uharibifu wa mazingira unaosababishwa na sisi binadamu.Waza nje ya box men.

Sent using Jamii Forums mobile app

Siamini kuandika kote huku ni kiporo na mchepuko ndio kilichokukalisha kwa key board or ur smart phone any way ndio akili ilivyokupeleka
 
Kuna taarifa zisizo rasmi kwamba kutokana na ujenzi wa miradi mikubwa mikubwa hapa Tanzania na miradi hiyo ikiwa chini ya wachina basi inasadikika jamaa hawa kutoka Asia wameamua kufanya yao ili wasisumbuke na ujenzi.

Nimejikuta najiuliza mengi na nikajiuliza sasa maisha yetu yanakwenda kuwaje. Joto limezidi kila kona, ardhi imekauka na mazao yamekaukia mashambani. Kwingineko magonjwa pia yamechachamaa mno kwasababu miili imechemka kupita kiasi

Kama hii kweli ni wachina ndo wanahusika basi hawa watu watatuletea majanga makubwa. Wanatakiwa kujua kwamba nchi yetu iko katika ukanda wa joto kali la tropic ambako kwa kiasi kikubwa kutofautiana na ile ya china, kama kwao wanafanya hivyo ni sawa lakini kwa Tz si sehemu sahihi kwani kijiografia tayari sie tuko kwenye tanuru na hatuitaji tena kuchochewa kuni na mkaa

Tuiombee nchi yetu watanzania, asubuhi njema!
Katika Nchi za Afrika , Tanzania imechukua pesa chache sana toka kwa Wachina.
 
Tatizo moja tunalopambana nalo baada ya kuwa tumepata vielimu vyetu ni kuanza kudharau kila kitu na kudhani mambo mengine ni hadithi za abunuwasi.

Nataka nitoe angalizo na kisha assignment alafu mwende mkalete hayo majibu yenu ya kisayansi kuupinga ukweli huu. Sidhani kama mnafahamu kwamba mvua inawez kuitwa, kuondoshwa na kuhamishwa uelekeo. Kwa wasiolijua hill na bado unaamini sayansi yako basi ziko sayansi zenyewe.

Nataka mnijibu ni kwanini maiti haisafirishwi hadi mambo ya kiasili (wanaojua wanajua) yawekwe sawa.

Nenda kwenye ujenzi mkubwa mtwambie ni kwanini kunatakiwa kafara za maana na hii si bongo tu, kama ni mfatiliaji anza kufatilia Chanel ya discovery science utanielewa

Tunaomba mtujibu haya maswali yenu na elimu ya darasañi alafu ntarudi na facts za ziada
 
Naona hatimaye mmekubali baada ya kukosa majibu ya maswali yangu. Sina udhubutu kabisa wa kuidharau elimu zetu lakini hatuna budi kuheshimu sanaa za mababu zetu. Wanao uwezo mkubwa na usiomithirika pale wanapoamua, wanao uwezo wa kuisimamisha hii dunia na watanzania tukatembelea magoti. Kama haya yanayofanyika sahivi ni moja ya uwezo wao ijapo ule wa Mungu uko juu zaidi.

Mitaa ya Soga hapa kwa waturuki kila wiki kondoo wanakula visu na damu inaleta neema, usiniulize mengi ila unakaribishwa kwa utafiti.

Usiwadharau wale wanaitwa wazee, ukisikia kijana usiwakojolee wazee elewa usiwape tabu.

Cc Mshana
 
Back
Top Bottom