Tetesi: Huku wachina kule mvua, njaa na maradhi vinatuua watanzania

Tetesi: Huku wachina kule mvua, njaa na maradhi vinatuua watanzania

Kuna taarifa zisizo rasmi kwamba kutokana na ujenzi wa miradi mikubwa mikubwa hapa Tanzania na miradi hiyo ikiwa chini ya wachina basi inasadikika jamaa hawa kutoka Asia wameamua kufanya yao ili wasisumbuke na ujenzi.

Nimejikuta najiuliza mengi na nikajiuliza sasa maisha yetu yanakwenda kuwaje. Joto limezidi kila kona, ardhi imekauka na mazao yamekaukia mashambani. Kwingineko magonjwa pia yamechachamaa mno kwasababu miili imechemka kupita kiasi

Kama hii kweli ni wachina ndo wanahusika basi hawa watu watatuletea majanga makubwa. Wanatakiwa kujua kwamba nchi yetu iko katika ukanda wa joto kali la tropic ambako kwa kiasi kikubwa kutofautiana na ile ya china, kama kwao wanafanya hivyo ni sawa lakini kwa Tz si sehemu sahihi kwani kijiografia tayari sie tuko kwenye tanuru na hatuitaji tena kuchochewa kuni na mkaa

Tuiombee nchi yetu watanzania, asubuhi njema!

Mbona hawazuiii kwao mvua kibao pili huwezi kishindana na mungu yeye huleta mvua kwa kadri yake na anapotaka yeye na kwa kipimo, unajua wingu la mvua lina tani ngapi za maji akitaka kudondosha yote duniani kwa mara moja dunia itapotea ndio maana anaiteremsha kwa kadri kidogokidogo
 
Back
Top Bottom