Ubinafsi wa wabantu umekita mizizi mpaka kwenye familia, Baba kapambana kuwa na biashara iliyofanikiwa lakini hashirikishi watoto, akifariki familia haijui lolote kuhusu biashara, umasikini unaanza kuinyemelea familia.
Nimeicheki hii interview ya kijana wa miaka 25, Abdullah Mahmoud
Ni boss wa kampuni ya malori 90 yanayosafirisha mafuta Zambia, Congo, Rwanda, n.k.
Yeye ni kizazi cha tatu cha biashara ya familia, biashara ilianzishwa na babu yake, ikarithishwa kwa baba yake na sasa ni yeye kizazi cha tatu anaisimamia.
Alianza kuzoeshwa biashara ya familia akiwa na miaka 6 (sita), kufikia 20 tayari alikuwa kaiva, tayari ana ujuzi wa malori, anavijua vibali husika vya biashara na kujifunza nidhamu ya fedha kwa kujionea jinsi pesa inavyotafutwa.
Inasikitisha kuona waafrika hasa hii asili ya wabantu bado tupo na huu ujinga wa kila mtu ajitafute kivyake, halafu tumekuwa brainwashed na huu utamaduni wa kumuona mtu alierithishwa biashara sio chochote, tunamsifu yule aliejipambana kutoka sifuri, tunapenda kuona mtu aliefanikiwa kwa kupitia mikiki na msoto.