Huku Watanzania tunajisifu ujinga kila mtoto ajipambanie from scratch, kijana wa kisomali miaka 25 anasimamia malori 90 biashara iliyoanzishwa na babu

Sasa sijui huyu kijana wangu nianze kumfundisha kuendesha boda boda na kunywa visungura asije akashindwa kusimamia hii biashara yangu🐼
šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚šŸ˜‚
 
Kwa hiyo huyu Dogo badala ya kwenda International School yeye akazama na Malori?
 
Walianza na lori 2 ndo zimefika 90
 
Huenda mori yalikuwa hata 200
 
Pamoja na vita , Ukraine imeandikisha rekodi ya kuuza mazao ya Kilimo Kwa Wingi sawa na kabla ya vita.
 
Sasa ukioa unawezaje kukaa na watu wanaozaa kama panya huku wana uwezo mdogo na wewe bado unajitafuta utawalisha nini?
 
ā€œUrithi ni elimuā€ kauli inayotumika na wazaz ambao wanakwepa kuwaachia au wanaona hamna la kuwaachia watoto.

The fact hata bila huyo mzazi, kwa mifumo ya sasa mtoto angepata elimu.
Succession plan wanakuwa nazo baadhi ya wafanya biashara ndo maana zinaish biashara zao

Nadhani nipo sawa brother Mzee wa kupambania
Blood Ibn Unuq
Lakini kwa upande mwingine shida kubwa ipo kwa watoto wenyewe wa kuweza kurithishwa hizo mali, watoto wengi akili zao ni mbovu Sana. Hawawezi kabisa kusimamia mali za urithi wanazoachiwa na wazazi wao hata Kama wazazi wenyewe walijitahidi kuwashirikisha watoto wao katika usimamizi wa hizo mali wakati walipokuwa bado wapo hai. Watoto wengi Sana wa Sasa akili zao ni mbovu Sana, linahuzunisha Sana suala hili. Vijana wakiachiwa mali za urithi wanakuwa wafujaji Sana, wanazitapanya hovyo hovyo kwa kuhonga wanawake au kuhonga wanaume, hatimaye wanafilisika na kuwa na hali ngumu Sana ya maisha.
Nakumbuka miaka ya nyuma Sana ya 1990's wakati huo nikiwa naishi Mjini Morogoro, kulikuwa na familia moja (family friend) ambayo kwa kweli ilikuwa inajiweza kiuchumi, nakumbuka familia hiyo ilikuwa inamiliki vitega uchumi vingi Sana hapo Morogoro ikiwamo na jengo moja la biashara (kama sikosei lilikuwa linaitwa Ghorofa la Luna) lilikuwa lipo jirani kabisa na Jengo la Makao Makuu ya Benki ya NMB Mkoa wa Morogoro wakati huo, tawi la Wami. Mwishoni mwa miaka ya 2000's niliporejea nchini Tanzania kwa mapumziko ya mwisho wa Mwaka kutoka nje ya nchi, siku moja niliamua kuwatembelea waliokuwa marafiki zangu wa zamani huko Morogoro, nilipofika huki nilikuta mambo mengi yamebadilika Sana, wale marafiki zangu wengi wao sikufanikiwa kuwaona kwani baadhi walishafariki dunia na wengine walirudi vijijini baada ya kushindwa maisha ya mjini licha ya kwamba wazazi wao waliwaachia mali nyingi Sana. Mali nyingi waliziuza na pesa kufanyia starehe, wakiwamo na baadhi ya wanafamilia wamiliki wa hilo Ghorofa la Luna. Nilipopata Habari hizi kwa kweli nilisikitika Sana.
 
Pamoja na vita , Ukraine imeandikisha rekodi ya kuuza mazao ya Kilimo Kwa Wingi sawa na kabla ya vita.
Na tunaouziwa Ngano n9 Tanzania Kisiwa cha Amani.

Ngano itoke Ukraine isafirishwe ije iuzwe kariakoo Mama wa Bukoba atengeneze maandazi na Chapati


Kwei hiki sio kisiwa cha amani bali kisiwa cha ujinga.

Hivi Tanzania Kilimo Cha Ngano hakiwezekani?
 
ā€œUrithi ni elimuā€ kauli inayotumika na wazaz ambao wanakwepa kuwaachia au wanaona hamna la kuwaachia watoto.

The fact hata bila huyo mzazi, kwa mifumo ya sasa mtoto angepata elimu.
Maisha yenyewe tu mtaani ni Elimu Tosha. Labda kama.unataka Elimu ya Kusolve Quadratic Equation
 
Once you are born in Africa life is automatically leading you 1-0.

If your parents are poor that's 2-0.

If you are not educated that is 3-0.

At this point you have no option. You will hustle like a donkey.
 
Ili kupata watoto wa aina hiyo mzazi anatakiwa awaandae kuanzia utotoni. Si mtoto hujamshirikisha na kumuandaa then utu uzima ghafla unamuachia lazima azile

Mfano familia ya mo-dewji

Imagine asingehusishwa na mzazi wake , gafla akapewa metl at age ya utu uzima? Ingekuwepo?
 
Sasa miaka 20 tz ni umri wa kwenda disco huo nilipokua huo umri nilikuwa nawaza kupata videmu🤣tu Miak
 
Mzee nikwambie tu kibongo bongo ukifanya biashara ukafata kodi zote kama zinavotakiwa na sheria zote mkubwa utabaki kama mimi hela ya Kula tu mzee, nothing big Ila kama unataka kuwa giant lazima ufanye umafia vunja sheria za nchi dhulumu, ua, nyonya, iba, manipulate kwenye mifumo rasi, kuna Ile principle ya kutukolipa kodi Can
 
Ni kweli kabisa unachosema, lakini bado watoto wengi Sana wa Sasa Wana tatizo baya la kuwa na akili mbovu. Unaweza ukafanya hivyo ulivyoeleza lakini mwisho wa siku bado watoto wenyewe wanaweza kuwa na tatizo hilo hilo baya la kusimamia mali za urithi au kushindwa kabisa kusimamia miradi ya wazazi wao. Mfano mwingine mzuri zaidi kwenye hili ni kufa kwa Kampuni ya Usafirishaji Abiria ya Mabasi ya Hood (Hood Company Ltd). Kwa taarifa za uhakika nilizopata ni kwamba Mzee Mmiliki mwanzilishi wa Kampuni hiyo ameamua kuachana na biashara hiyo baada ya kuona kwamba hakuna hata mtoto wake mmoja mwenye nia au hamasa ya kuendeleza uendeshaji wa Kampuni hiyo aliyoianzisha. Hivyo, kutokana na umri kumtupa mkono ameamua bora aachane na hiyo biashara na apumzike baada ya kukosekana mtu mwenye nia ya kuendeleza uendeshaji wa Kampuni yake hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…