Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Mgeni akifika Zanzibar, Watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
Waulize Mchamba wima maana yake nini??

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Wanasema maeneo hayo yalikuwa na majani yenye miiba (mbigiri) enzi hizo kabla ya maji ya mfereji kuna, walikuwa wanachamba kwa kuburuza Makarios mchangani , sasa eneo hilo walishindwa kwasababu ya miba miba; Hivyo ikabidi wawe wanachamba wima kwa majani kama tissue! NDO PAKAZOELEKA MCHAMBA WIMA
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
What?!
7659090.jpg
 
OK!!!MKUU asante kwa ufafanuzi wako

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Eti n'tie dole hapo.
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
Kwa kauli hii ya ntie dole nmeamini hakuna right and wrong lakini inategemeana na jamii husika ina define vipi jambo husika.
 
Back
Top Bottom