Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Mzee ananihadithia kuwa wazenji waliuana sana enzi za vita vya Idd Amin; unakuta wamejificha basi mwenzake akikohoa tu anaambiwa "webwana wataka twonekane tena wakohoa nini bwanaa?" Baada ya kusema hivyo anamshuti
 
Zile canter zimewekewa ma bench ndani bado zinasafIrisha abiria!!?
 
K
Yes kwa nchi nyingi sana kuna maneno yanaingiliana ila tu yanakuwa na maana tofauti unakuta neno fulani kwa lugha fulani lina maana nzuri kwa lugha nyingine lina maana mbaya! Mfano South Africa neno "mkundu" (ashakum si matusi) ni jina la mtu na lina maana nzuri tu!
Kwenye tamthilia ya ISIDINGO Kuna actress alikuwa anaitwa "Mthombeni".
Sasa shida Ni kwamba hiyo "tho" haitamkwi Kama ilivyoandikwa, inatamkwa "To"
 
"Konda nishushie poro langu au wanasema kiporo"😂😂 poro ni mzigo kama vile unga wa kilo 25 au mchele.. akienda dukani kununua mchele wa kilo 25 au unga wanaita poro la sembe au poro la mchele.. for the first time kwenye gari kuna mama alikuwa anashuka akamwambia konda nishushie kiporo changu 😂😂 mi nikajua uporo chakula kilicholala hatari tupu.😅
 
Nilifumania mpira wa miguu ukichezwa Sasa ndugu aliekuwa na mpira alikuwa kwenye kona mwenzake akawa analalama kwambi "tia tia tia!" Akiwa na maana apige krosi ije gorini afunge..😂😂
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
Hauvumi lakini umo[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mgeni akifika Zanzibar, Watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
Daaah umenikumbusha mbali aisee, ila nimecheka Sana'a [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] shusha hapo ikipindaa
 
Back
Top Bottom