Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi
[emoji1787][emoji12][emoji12]

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Huku hurambi bila usipoangalia unaweza rudi mkavu bara
Kuna chupi na hafu na ni tofauti kwa hapa umeongopea.

We we round about nienglish sasa unataka waseme English wakat kiswahili kipo?
 
Lkn zinaenda kupungua mkuu Kuna mi kosta yakutosha.. hizo mbavu za mbwa zitakuwa za kubeba mizigo,lkn hata hivyo zile gari zipo njema sio mbavu za mbwa tu bali ziitwe roho ya paka.
Basi siku hizi safi, zamani gari za mizigo ndio ziliwekwa mabench kwa ajili ya kibeba abiria.!
 
Sie nyanya huku twaita tungule. Soko twaita marikiti. Mpenzi twamwita babibi
 
Mzee ananihadithia kuwa wazenji waliuana sana enzi za vita vya idd amin; unakuta wamejificha basi mwenzake akikohoa tu anaambiwa "webwana wataka twonekane tena wakohoa nini bwanaa?" Baada ya kusema hivyo anamshuti
Hizo fix sasa kaka
 
Askari wa Zanzibar
_ akija kukukamata anakwambiya utangulie kituoni,,,tena
anakukabidhi gegeje ukifika pale police umsubiri nje,,
Yeye anamalizia kula urojo..
Kkkkkk askari wa Zanzibar ...
Halafu nasikia wanavaa shati la police wanachomekea msuli na kubazi..na kofia ya balaghashea..
_mwanamke akipanda bodaboda haruhusiwi kumshika kiuno mwendesha bodaboda,,,anapaswa akae upande upande..
Halafu majina yao sasa!!
Chamba wima.
Mfereji maringo.
Chokocho.
Kiembe samaki.
Kiembe ladu..
Nasikia akikamatwa mwizi hapigwi,,,bali anamwagiwa vumba la samaki,,,akaliwe na paka huko aendako.
 
Si afadhali hata wangekuwa wanasema "shusha" sasa, wengi wanasema "tia"! Kuna sehemu inaitwa Dole konda akisema "Dole" anayeshuka hapo anasema "tia", au utasikia n'tie Dole hapo!

Yaani wale maneno mengi wanayoyaongea ukiyaleta kwa tafsiri ya bara unakuta ni Matusi

Wanafanya kusudi kutukana
Kuna kituo Chao kimoja kinaitwa 'ikikuuma seema'
Konda mkifika anasema 'kikuuma'..

Wanapenda lugha za matusi sana
 
Mgeni akifika Zanzibar, Watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
Nyanya maji wanaita TUNGULE,

Afu mademu wa huko wanatuchukia sana vijana wa huku bara,yaani wanatuona Kama TAKATAKA ila kaka zao wanawala freshi tu dada zetu..
 
Back
Top Bottom